Utajiri ulipo kwenye makundi ya WhatsApp

Utajiri ulipo kwenye makundi ya WhatsApp

bongodili tele

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2024
Posts
1,519
Reaction score
3,048
UTAJIRI ULIOMO KWENYE MAGROUP YA WHATSAPP

Idadi ya wanakundi zidisha kwa Tsh 1000

Huu ni mchango wa siku moja kwa kila mwanakundi

Kisha zidisha kwa wiki

Kisha zidisha kwa mwezi

Kisha zidisha kwa mwaka

Hapo utaweza kupata jibu la watu waliomakini kwenye kutumia fursa utaona ni kiasi gani cha pesa kwa mwaka wanaweza kukikusanya kama mtaji

Mfano:

▶️Kundi la watu 200

(WNC = 257)

▶️Kila mtu kwa siku atoe 1000

▶️Itakusanywa 200,000

▶️Kwa siku 7 hitakusanywa 1,400,000

▶️Kwa wiki 4 itakusanywa 5,600,000

▶️Kwa mwaka itakusanywa 67,200,000

Jambo hili huweza kufanyika kwa malengo ya mwaka mmoja au miwili kukusanya mtaji

Mradi utakaoanzishwa ukawa na mgao kwa wanakundi kila mwaka

MTAFIKAJE HAPO

▶️Kwanza kundi liwe na watu wenye malengo ya pamoja wakweli waliodhamiria kusaidiana kuondoka kwenye lindi la umasikini

▶️Pili lazima muwe watu wa eneo moja mnaloweza kukutana kwa urahisi

▶️Tatu lazima mfanye mkutano wa pamoja wa maaamuzi ya kuliendea lengo hilo kwa kuchagua viongozi wakweli wenye dira na hilo jambo

▶️Nne lazima ujirasimishe kwa mamlaka husika na kujisajili na muwe na Uongozi na mfungue akaunti ya benki wanakundi wote wawe wanachama wa hiyo taasisi ili waweze kuhoji na kushiriki katika uendeshwaji wa jambo kihalali

Hapa nitakuwa nimewafumbua macho wenye akili

Watu wamo kwenye makundi mengi tu ila hayanafaida zaidi ya kupiga soga kuchekeshana na kutumiana maujingaujinga 🤔

Tuzinduke

Unakuta mtu simu yake ina kundi la:

Shule ya msingi,
Secondary,
A level,
Chuo kikuu,
Bado makundi ya kazini,
Bado makundi ya familia,
Bado makundi ya mitaaani, nk.

Katika makundi haya yote ni liability ya kuomuongezea gharama ya data tu na kusogoa hana kundi hata moja lenye uwezo kumnyanyua kipato chake huku ni kupoteza muda sana🤔🤔

Mwisho wa siku ni umasikini tu uliokithiri🤔

Amkeni, tumelala
 
Kimaandishi ni rahisi ila utekelezaji ni zero nilishawahi kuwahamasisha sana ila Hola
 
Ulichowaza ndio kuzidishiana umasikini zaidi labda hiyo pesa awe anakusanya baba paroko/imamu japo nao ni binadamu
 
Pdf, Huwa Ndiyo Mawazo Yao Kila Kitu Rahisi
 
Watu 200, mtafanya kitu gani kiwanufaishe wote, hivI unafikiria sawa sawa🤔
 
Watu 100 mchange buku kwa siku ili mwisho wa siku mfanye nini?
Eti uchangishe classmates, sasa wengine wameolewa wengine wameachika. Hawa wako Mtwara hawa Sengerema. Unaumwa wewe
 
Uo utajiri watu wa forex ndo wanaupata kwa kuuza signo kiingilio 30usd kwa mwezi u akuta mtu ana pipo 500
 
Ukiona kuna kitu hakifanyiki ujue hakiwezi kufanyika
 
Kwanini usichange peke yako kwa mwaka upate hizo lakio kadhaa; kuna maisha zaidi ya kazi na pesa watu wanaingia kwenye hizo group for socializing ukishabadilisha na kuwa group la kuchangishana usishangae ukabaki peke yako and everyone has left au wale marafiki zako mkageuka kuwa maadui
 
Back
Top Bottom