Mlenge ni tabu sana kuwa na pesa za ziada ilhali umezungukwa na masikini wa kutupa. Ninakumbuka miaka mingi kidogo mjomba wangu alistaafu na kuamua kurudi kijijini
Mtu mmoja alipata kutuambia duniani hakuna mtu maskini. Kama ukiangalia mipango na matamanio ya watu, wote wangependa kuwa katika maisha bora yasiyo ya umaskini. Shida ni kwamba mipango na matamanio yao hayatimii. Kwa hiyo, tajiri ni mtu ambaye mipango na matamanio yake yametimia.
Kama Mwenyezi Mungu amemkubalia mtu akapata utajiri (kwa maoni ya wanaomzunguka), ina maana Mungu amekubali mipango na matamanio ya mtu huyo yatimie. Lengo kuu la Mungu kumkubalia mtu huyo afanikiwe, ni kumuwezesha awasaidie watu fulani kwa wakati fulani, kwa namna aliyokusudia Mungu. Yaani mtu huyo anageuka kuwa kipitishio ( conduit ) ya kuwa msaada kwa watu wengi.
Baba yangu alipata kutuambia kwamba Mungu alikasimu madaraka ya vitu vyote kwa wanadamu na malaika, lakini jambo moja tu alibaki nalo Yeye Mwenyewe, ni kugawa riziki. Kwa hiyo, kwa mfano wa huyo mjomba aliye kijijini, Mungu anamtumia ili kazi yake Mungu ya kugawa rizki iwe fanisi kuwafikia wale aliowalenga.
Siku ambayo ataacha kuwatumikia wananchi, hata hilo Land Rover 110 litaanza kupata majanga yanayoyapata Malendrova mengine. Kwa sasa hilo Landrover linalindwa na Mungu kwa vile ndiye analitumia kwenye kazi zake za kugawa rizk, na linalindwa pia na wananchi ambao humkumbusha Mungu kupitia sala zao na shukran zao kwa mjomba wanapomuombea kheri kwa msaada anaowapatia.
Ni hivyo pia kwa cheo, madaraka, mamlaka, elimu, uwakilishi na namna zote zinazomuinua mtu mmoja ukilinganisha na wenziwe.