Utajiri ni Muda, Specialization & Turnover kubwa

Apollo one spaceship

JF-Expert Member
Jan 28, 2021
242
431
MUDA& SPECIALIZATION
Nimejifunza kutoka kwa tajiri mmoja ambaye aliwekeza juhudi&maarifa yake kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu, matokeo yake nimeyaona baada ya miaka kama 20.Leo hii anakula matunda ya kazi yake.Huenda watu wakawa maskini kwa kutaka matokeo ndani ya muda mfupi.Pia huenda umaskini ni kwa sababu watu hufanya Jambo hili kisha wanarukia jingine(Kuwa na mishemishe nyingi__no specialization)

TURNOVER KUBWA
Huu ni uharaka wa kuuza bidhaa na huduma.Mfano, huduma ya mpira ya Messi pale PSG inamwingizia TZS.6000 kila sekunde,bidhaa za MO Dewji zinauzika kila saa masaa 24,Amazon&Alibaba kuna transaction za kila sekunde,huduma za mabenki ni kila muda.Hapa tutegemee ukwasi wa kutosha tu.Turnover ya Mlimani city ipo juu,pia maduka yenye marketing nzuri ya turnover kubwa sana.Maskini tunajulikana tu!! Machungwa hamsini yatachukua siku tatu kuuzika yote,nguo utauza mbili kwa siku moja tena kwa kuwabembeleza au kuwalilia wanunuaji

HAYO YOTE YAKIWEZEKANA,sambamba na money management kama saving utajiri utakugongea hodi bila nguvu nyingi.
 
Talk is always easy, but all in all make sure your savings work for your total income. Sio kuwekeza hela kwenye kibubu ikae tu. Tuendelee kupambana.
 
Back
Top Bottom