Utajili zaidi wa haraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajili zaidi wa haraka

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Mbaga Michael, May 10, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,913
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Habari wanajamii!

  Nawatafuta watu wenye mitaji ya kuanzia kama milioni 3 hivi tufanye nao biashara.

  Biashara yenyewe iko namna hii ni kuzalisha umeme kwa kutumia machine ya kusaga itakayobadilishwa na kuwa ya kufua umeme kwa kufungiwa moter, nipo eneo moja Mkoani mwanza pembezoni mwa mji ni sehemu iliyo na watu wengi sana kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiwa wamekuja kutafuta eneo hili, kwa bahati mbaya eneo hili hakuna umeme usambazwao na shirika letu la umeme la Tanesco bado haujafika, ingawa kuna mtu mmoja yupo sehemu hii ikijaribu kutoa huduma hii maeneo haya kwa kutumia machine ya kusaga yenye piston moja ambayo imeelemewa mzigo kwa mahitaji ya wateja kuwa makubwa hivyo kufanya watu kuendelea kukaa gizani


  hizi ndizo gharama anazozitoza huyu bwana kwa wateja wake kwa siku

  1. Ukihitaji umeme nyumbani kwako balbu moja tsh. 500/=@siku

  2. Kwa mwenye salon maeneo haya kama anahitaji hudumu yake anatozwa 3000/=@siku

  3. Kwa wenye kumbi labda za kuonyesha video tsh.5000/=@siku

  3. Kwa wenye maduka tsh.5000/=@siku kama ana charge na simu

  4. Kwa wenye mabaa tsh. 4000/=@siku huruhusiwa kutumia friji kuepusha mashine kuzimika kwa ukubwa wa mzigo

  kwa kifupi mahitaji bado ni mengi mno na hudumu iliyopo sasa inalegalega sana kama utalizika na maono yangu ya kufanya nawe mfanyabiasha biashara hii katika eneo ili tafadhari tuwasiliane kwa kuniPM
   
 2. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,680
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  kwa kuangalia nature ya hiyo biashara, utajua kuwa hailipi hiyo milioni 3 ni bora ua kaifanyie biashara ya kununua mpunga na kuuleta pale mabatini mwanza. nenda kabuni biashara nyingine
   
 3. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,680
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  hizi ndizo gharama anazozitoza huyu bwana kwa wateja wake kwa siku

  1. Ukihitaji umeme nyumbani kwako balbu moja tsh. 500/=@siku
  (kwa wakazi wa pembezoni na mji wa mwanza hawawezi kumudu bei hii, isitoshe wanaohitaji ni wachache kama wapo hawazidi 50, 50x500= 25000)

  2. Kwa mwenye salon maeneo haya kama anahitaji hudumu yake anatozwa 3000/=@siku
  (wenye saloon hawana pato la kutosha kumudu hii gharama kama wapo hazidi 1, 1x3000=3000)
  3. Kwa wenye kumbi labda za kuonyesha video tsh.5000/=@siku
  (hakuna ukumbi wa video unaoweza kumudu gharama hii labda useme @Tsh. 2000/day, kama yupo ni mmoja, 1x2000=2000)
  3. Kwa wenye maduka tsh.5000/=@siku kama ana charge na simu
  (hakuna mwenye duka wa kumudu hii gharama isitoshe kwa vijini huwa wana wahi kufunga)
  4. Kwa wenye mabaa tsh. 4000/=@siku huruhusiwa kutumia friji kuepusha mashine kuzimika kwa ukubwa wa mzigo
  (kwa wenye baa labda kidogo nao hawawezi kuzidi 3, 3x4000=12000)

  jumla ya mapato kwa siku itakuwa 25000+3000+2000+12000=42000 x30days =1,260,000 hapo bado hujatoa gharama za uendeshaji na matumizi ya ya kifamilia ambayo unaweza kuyakadiria kufikia 30,000/day, kwa mwezi kuwa 900,000, na kubakiwa na faidi ya 360,000 kwa mwezi,
  hapa ni bora ukauze ng'ombe ufungue kwa mtaji wako binafsi na wala si wa kushirikisha mtu mtatafutana ubaya
   
 4. l

  london JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Sep 12, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ningependa kujadiliana nawe zaidi hebu niandikie email: etambala@yahoo.co.uk itakuwa vizuri kama una skype address ukaniandikia ili tuongee kwa mapana.
   
 5. u

  ulanzi mtamu Senior Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  million 3 c bora nianzishe kibanda cha m pesa..
   
 6. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #6
  May 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,913
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  We ni kilema au ni mchaga ndo maana, pole sana
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  tanesco wakileta umeme itakueje? au ndio value of risk?
   
Loading...