Utafiti wangu: Maprofesa wengi walioteuliwa serikalini wameboronga

Simba mnyama

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
348
Reaction score
129
Kulingana na utafiti wangu nilioufanya kwa kuangalia samples za maprofesa mbalimbali waliopewa majukumu serikalini wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kitu kinachonifanya ni-conclude kuwa sio uprofesa unaoongoza bali kipaji, moyo wa uzalendo, na uadilifu wa mtu. Kwa muda mrefu na kwa vipindi tofauti tumeshuhudia maprofesa wakipewa dhamana ya kuongoza lakini ama wame-under perform au wamelitia kabisa taifa hili katika hasara, ufisadi na aibu. Utafiti wangu utaangalia maprofesa wafutao ambao wameishia katika sifa hizo hapo juu:

1. PROFESSOR PHILEMON MIKOL SARUNGI: Huyu ni mbunge na waziri mtaafu katika awamu ya pili na ya tatu ya serikali katika nchi hii. Professor Sarungi, Daktari Bingwa wa mifupa na upasuaji (Surgery and Injuries), alikuwa ni mbunge wa jimbo la Rorya lakini pia amewahi kuwa waziri wa afya, waziri wa mawasiliano na uchukuzi (Communication and Transport), Mkuu wa mikoa ya Pwani na Kilimanjaro, na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Muhimbili, ni waziri ambaye hakuacha historia yoyote nzuri katika nchi hii mbali na migomo ya madaktari na huduma hafifu za kiafya. Huyo ndiye Professor Philemon M. Sarungi.

2. PROFESSOR JUMA ATHUMANI KAPUYA: Huyu ni mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi aliyebobea kwenye mambo ya mimea (botany). Amekuwa mbunge wa jimbo hilo tangu 1995 hadi leo. Mbali na ubunge nyadhifa nyingine alizowahi kushika serikalini pasipo mafanikio yoyote ni pamoja na Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na kasha tena kurudishwa katika Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo. Huyu ndiye Profesa aliyeua michezo mashuleni na kwa kipindi kirefu timu ya taifa ilikuwa kichwa cha mwendawazimu. Hakuna fahari yoyote ya kujivunia kwa profesa huyu. Huyu ndiye profesa ambaye wananchi wake wa Urambo Magharibi wangali wanalilia maji, elimu bora, afya na barabara katika jimbo lake. Huyu ndiye Professor ambaye alikumbwa na skendo ya kumbaka na kumwambukiza Ukimwi mwanafunzi wa miaka 16.

3.
PROFESSOR ANNA KAJUMULO TIBAIJUKA: Huyu ni mbunge wa Jimbo la Muleba ya Kusini tangu mwaka 2010. Ni msomi aliyebobea kwenye masuala ya uchumi (Agro-Economics). Amewahi kufanya kazi katika vyombo vya kimataifa kama UN-HABITAT akiwa UN Under-Secretary-General and Executive Director; lakini pia amewahi kuwa Director-General, United Nations Office mjini Nairobi (UNON). Kwa sasa ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na Professor Jakaya M. Kikwete. Huyo ndiye Profesa aliyekubwa na kashifa ya kupata mgao haramu kutoka katika Akaunti ya Escrow. Ikumbukwe kuwa Bunge la Jamuhuri limemtaka Rais amuwajibishe Waziri huyu kwa kumvua nyadhifa zote aliyonazo serikalini. Huyu ndiye Professor ambaye amekuwa akilalamikiwa sana na wananchi wa Kigamboni kuhusiana na Ujenzi wa mji mpya Kigamboni.

4.
PROFESSOR SOSPETER M. MUHONGO: Huyu ni mbunge wa kuteuliwa na Rais. Huyu ni msomi mkubwa aliyebobea kwenye masuala ya miamba au madini (geology). Ni msomi na mtaalam anayetambulika na kuheshimika kimataifa kwenye masuala hayo. Miongoni mwa sifa nyingine alizonazo ni pamoja na kuwa Honorary Fellow of the Geological Society of America (HonGSA), an Honorary Fellow of the Geological Society of London (HonFGS), an Honorary Research Fellow of the Chinese Academy of Geological Sciences (HonFCAGS), a Fellow of the Academy of Sciences for the Developing World (FTWAS), a Fellow of the Geological Society of Africa (FGSAf), a Fellow of the African Academy of Sciences (FAAS) and a Fellow of the Tanzania Academy of Sciences (FTAAS). Professor Muhongo amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa State Mining Corporation (STAMICO) kati ya mwaka 1999 na 2005 lakini pia amewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Geolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1997-2000). Ni kutokana na sifa hizo pengine zilizomfanya Rais wa Jamuhuri kumteua kuwa Waziri wa Nishati na Madini lakini kama ilivyo kwa Professor Tibaijuka, Professor huyu amekuwa na kashfa kuwa kuhusishwa na Akaunti ya Escrow. Professor huyu anasubiri kuwajibishwa na Rais aliyemteua.

5. PROFESSOR JUMANNE ABDALLAH MAGHEMBE: Huyu ni mbunge wa jimbo la Mwanga tangu mwaka 2000. Ni msomi aliyebobea kwenye masuala ya misitu. Licha ya kuwa mbunge amekuwa ni waziri ambaye amekuwa akihamishwa kutoka wizara moja kwenda nyingine kwa vipindi tofauti. Amewahi kuwa waziri wa elimu, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika na hivi sasa ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji. Huyu ndiye waziri ambaye sehemu kubwa ya nchi hii haina maji. Ni waziri mwenye majigambo kuliko utendaji. Huyo ni profesa wa misitu.

6.
PROFESSOR JAKAYA M. MRISHO: ???

Nihitimishe kwa kusema kuwa, ni kutokana na utafiti wangu huu nashindwa kabisa kujiaminisha kwa asilimia mia kuwa CAG Mteule, PROFESA MUSSA JUMA ASSAD ataweza kutuletea mafanikio yaliyoletwa na Bwana Ludovick Utouh ambaye hakuwahi kuwa professor, wala kuwa na degree ya uzamivu au uzamili lakini ameacha historia kubwa ili njema katika nchi hii. Tumeambiwa kuwa Professor Mussa Juma Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991. Mimi sitaki kusikia sifa za elimu, nataka kuona atafanya nini kwa kutumia elimu yake.

Nawasilisha.
 
Unaweza sema lolote kuhusu Prof. Machunda - Waziri wa Kilimo, RC Kigoma...? Huyu alikuwa Waziri enzi za Mwl. Nyerere.
 
Prof. Maji Marefu & Dr. Rwakatare Mbona anafanya vizuri tu.
 
Bado hujamaliza orodha. Kuna wengine walioboronga na wakavuliwa nyadhifa kama vile Profesa Peter Msola, Profesa David Mwakyusa na wengine kadhaa.
 
Mkuu shukrani ingawaje listi yako ya maprofesa iko selective.
Kuna ambao wameweza kuingia siasa na kuogelea nayo kama inavyotakikana.

Mamlaka za uteuzi wa maprofesa katika ulingo wa kisiasa lazima utambue haya
  1. Maprofesa siyo proffessionals wengi wao ni academicians wasio nahata chembe ya proffessional skills katika fani zao, ingawaje fani hizo wanazijua fika
  2. Kwa kuwa maprofesa ni academicians, uzoefu wao wa kujichanganya na kuona mambo kutoka chini uko very limited
  3. Wakiingia siasa kichwa kichwa maprofesa wengi hawana zile cloak-and-dagger corridor warfare experience
  4. Kwa kuwa wengi wa maprofesa walikuwa vyuoni au tasisi za utafiti ambazo hazina mapato mengi, naturally wakiingia siasa wanafanya kosa lile lile la wanasiasa , yaani grabbing as much as you can, in the limited time.
  5. Kutokana na kujiona wamesoma sana kuliko wengine, maprofesa katika siasa wanauponda ushauri ambao uneweza kuwaokoa kirahisi kutoka kwa walinzi, madereva, makatibu muhtasi, wafagizi etc
Ni hayo tu kwa sasa, lakini yako megi zaidi
 
Kumbe, madereva, walinzi... Uwa wanatoa ushauri wa kisiasa kwa Ma Prof! Nilikuwa sijuhi hili.
 
Profesa Mbilinyi .aliishia kufukuzwa kwa kashfa ya sukari
 
hilo ulilolisema la maprofessor kuboronga ni kweli kabisa na sababu zake ni hizi.

kwa msomi yeyote anatambua kuwa ipo tofauti kati ya mambo yanayofundishwa chuoni na mambo yaliyoko mitaani kwa maana kuna tofauti kubwa kati ya theory na experience.

maprofesa wanajua theory lakini hawana practical experience, they know what to do but they do not understand how to do.

katika ngazi ya kimataifa hawa wanaweza kufanya kazi kwa mafanikio kutokana na mtu kuzungukwa na wataalam mbalimbali. kwa theory zake wataalamu wakizungumza anawaelewa na wakikwama anaweza kuwashauri.

kwa tanzania nothing can be expected from proffesorial or doctorial

kwa tanzania viongozi wanafanya kazi bila competent people arround them kutokana na sababu tunazozijua. unapewa kundi la wataalamu humo kuna watoto wa marafiki zako ndizo sifa zao kuwa katika kundi la kitaalamu, kuna mahawara wa vigogo wengine, na kwa kifupi unakuwa na collection ya non experienced people without tacticts but they are there to earn.

sasa elimu ya professor inakuwa haijakamilika na kosa wanalolifanya ni kutojitambua udhaifu wao wa experience na kutumia nyadhifa zao kuongeza nguvu katika team kwa kuweka experienced huku ukiwaacha hawa waliokuja kutafuta maisha maana ukiwagusa hao kibarua kinaota nyasi.

hapa huwa wanadhani wanajua kila kitu sababu wanaitwa professor wanajikuta wanalizimika kushauri hata kwenye how to do eneo ambalo hawalijui na mwisho wa siku ni kuboronga kupitia eneo hilo na kuonekana ni wapuudhi kabisa.

kwa mtizamo wangu ili kuokoa nchi yetu mashirika na taasisis si kuwapa ma accademicians au watu wenye miaka mingi maofisini lakini hawana experience bali

ATC tafuta mtu kutoka mashirika ya ndege yanayofanya vizuri lakini aliye katika position ya kupanga na kutekeleza.
Reli, bandari, na mashirika mengi tuache kuteua watu ambao wanakaa maofisini hawana mbinu mpya wanaenda kusoma huku wakilipwa mshahara akirudi ni doctor lakini amewahi kufanya nini hakuna bali cv inaonyesha kuongoza mashirika yanayokufa.
 
Kumbe, madereva, walinzi... Uwa wanatoa ushauri wa kisiasa kwa Ma Prof! Nilikuwa sijuhi hili.

Hao watu ni muhimu sana mkuu.
Ndio watu wanajua mapema kabisa bosi wake au mwingine alikuwa wapi jana usiku, kwa mkuu mwingine au kwa Kalimanzira!
Ndo wanajua kwenye faili linalozunguka kwa kasi kuna nini.
Ndo wanajua leo bosi wizarani anaangusha kisago kwa watu fulani.

Na hao hao ndo wanaweza kutumika kukuhujumu au kukuwekea sumu, uliza kama waziri fulani aliyeponea chupuchupu baada ya kuwekewa sumu na mfagizi wake.
 
Mkuu shukrani ingawaje listi yako ya maprofesa iko selective.
Kuna ambao wameweza kuingia siasa na kuogelea nayo kama inavyotakikana.

Mamlaka za uteuzi wa maprofesa katika ulingo wa kisiasa lazima utambue haya
  1. Maprofesa siyo proffessionals wengi wao ni academicians wasio nahata chembe ya proffessional skills katika fani zao, ingawaje fani hizo wanazijua fika
  2. Kwa kuwa maprofesa ni academicians, uzoefu wao wa kujichanganya na kuona mambo kutoka chini uko very limited
  3. Wakiingia siasa kichwa kichwa maprofesa wengi hawana zile cloak-and-dagger corridor warfare experience
  4. Kwa kuwa wengi wa maprofesa walikuwa vyuoni au tasisi za utafiti ambazo hazina mapato mengi, naturally wakiingia siasa wanafanya kosa lile lile la wanasiasa , yaani grabbing as much as you can, in the limited time.
  5. Kutokana na kujiona wamesoma sana kuliko wengine, maprofesa katika siasa wanauponda ushauri ambao uneweza kuwaokoa kirahisi kutoka kwa walinzi, madereva, makatibu muhtasi, wafagizi etc
Ni hayo tu kwa sasa, lakini yako megi zaidi
Mchango mzuri sana mkuu. Ndiyo maan nchi zilizoendelea vyuo vikuu hushirikiana na makampuni ilikujifunza vitu vipya. Hapa kwetu mtu akiwa professor nadhani huwa wanajilinganisha kama Mungu. Sababu wanajichukulia wanajua kila kitu, wanashindwa kujua kuwa technolojia na mambo mapya yanatokea kila siku. Hawataki kujifunza. Ndo maana wakipewa nafasi tofauti na kufundisha na utafiti wanaboronga haswaaa.
 
Unaweza sema lolote kuhusu Prof. Machunda - Waziri wa Kilimo, RC Kigoma...? Huyu alikuwa Waziri enzi za Mwl. Nyerere.
Huyu Prof alikumbana na Moringe pamoja na Mwl Nyerere baada ya kutoa cooked data.
 
Tuanze sasa uhakiki wa madokta na maprofesa
 
Na je prof bashite yupo WAP??

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Hawa waheshimiwa walipaswa kubaki VYUONI washie CHAKI zao
 
Hapo hakuna wafalme bali kuna watawala ndo shida iluko

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Shida hapa ni mfumo na wateuliwa ,wanaopewa kazi hawafuati Misingi na utaratibu wa kazi zao ila wanafuata matakwa ya alie wachagua.Wateuliwa nao hawana ujasiri wa kusema Ukweli kwa kukataa yasio endana na kazi zao ,siku wanapo kuja kufutwa kazi basi Utashi na Akili ndio huwarudia kwa baadhi yao..
 
Back
Top Bottom