Utafiti: Wanaume wanakufa kwa Saratani kimyakimya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,462
Imebainika asilimia mbili tu ya Wanaume ndiyo wana uelewa kuhusu Saratani Mkoani Mwanza, hivyo kuwafanya baadhi yao kupoteza maisha kwa ugonjwa huo bila kujitambua.

Utafiti uliokusanya taarifa katika vituo vya Afya 50 mkoani hapo kuhusisha watu 1,120 ni Wanaume 11 pekee kati ya 560 waliohojiwa na kuelewa kwa undani kuhusu Ugonjwa wa Saratani ikiwemo saratani ya tezi Dume.

Utafiti huo uliyofadhiliwa na Taasisi ya Afya ya Aga Khan Tanzania umefanywa na Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili (Muhas), Profesa Twalib Ngoma kuanzia Septemba 2021 hadi Februari, 2022

Profesa Ngoma anasema "Katika utafiti nimebaini uelewa wa saratani kwa wanaume uko chini sana kiasi kwamba wanaume wengi wanaelewa kwamba saratani ni ugonjwa wa kifo ambao hauna tiba.

“Wengi wao wakishaonekana kuwa dalili zake huisia kukaa kimya kwa hofu matokeo yake wanakufa na tai shingoni yaani kimya kimya.”

Profesa Ngoma amesema katika utafiti huo pia amebaini jamii hasa vijijini inaamini saratani ni ugonjwa wa laana na unasababishwa na imani za kishirikina, hivyo mtu anayegundulika kuugua huishia kutengwa na jamii kisha kupoteza maisha bila kupatiwa msaada.

Amesema utafiti huo pia umebaini kuwa elimu duni inachagia zaidi ya 80% ya wagonjwa wapya wanaokutwa na saratani ikiwa katika hatua ya tatu na nne ambazo ni ngumu kutibika.

Aidha, Profesa Ngoma amesema uelewa wa saratani kwa Wanawake uko juu kutokana na uwepo wa programu za kuhamasisha wanawake kupima saratani kwenye mitandao na vyombo vya habari huku wanaume wakionekana kuwekwa kando jambo aliloshauri kuwa kuna haja serikali ikaanzisha programu za kuhamasisha wanaume kupima ugonjwa huo.

"Serikali inatakiwa kuwekeza nguvu kubwa katika utoaji wa elimu kwa Umma kujenga uelewa wa saratani hii itasaidia watu kujenga utaratibu wa kupima afya mara kwa mara ili kuanza matibabu wakibainika kuwa na dalili za saratani," amesema

Pia, amependekeza huduma ya vipimo vya serikali itolewe bila malipo kwa wananchi ili kutoa fursa na kuongeza mwamko kwa jamii kupima saratani na kuanza matibabu ikiwa katika hatua ya kwanza na pili ambayo kitaalam inatibika.

Katika kuongeza uelewa na mwamko wa jamii hasa wanaume kupima saratani, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RMO), Dk Thomas Rutachunzibwa amesema serikali kwa kushirikiana na Aga Khan imetoa mafunzo ya utambuzi wa dalili za saratani kwa watoa huduma ngazi ya jamii 200 mkoani humo.

"Changamoto iliyopo ni kwamba hawa watoa huduma ni wachache ikilinganishwa na mahitaji ya jamii kwa sababu elimu hii inatakiwa itolewe kwa kina hasa maeneo ya vijijini ambako mwamko wa upimaji afya kwa hiari uko chini," amesema Dk Rutachunzibwa

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tiba Aga Khan ambaye ni Meneja Mradi wa TCCP, Dk Harrison Chuwa amesema kupitia mradi huo wenye thamani ya Euro milioni 13.5 (Tsh. Bilioni 32.46) wamefadhiri tafiti, kujenga uelewa na kuboresha miundombinu itakayoleta ufumbuzi wa tatizo la saratani nchini.

"Ndiyo maana mbali na kutoa elimu ya kujenga uelewa wa saratani kwa jamii, tumenunua vifaa ikiwemo mashine ya Mamografia yenye uwezo wa kubaini saratani ya matiti. Tunaomba watu watumie fursa hii kupima afya zao," amesema Dk Chuwa.

Katika hafla hiyo matokeo ya tafiti tatu yamewasilishwa ambapo tafiti nyingine ni Utafiti wenye lengo la kupima uelewa wa saratani katika vituo vya afya na utafiti wa kuangalia jinsi gani jinsia inaathiri matibabu ya saratani.

Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo unaofanyika chini ya Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania (TCCP) katika wilaya za Mkoa wa Mwanza, Profesa Ngoma amesema zaidi ya 98% ya wanaume hawana uelewa kabisa kuhusu visababishi vya ugonjwa wa saratani.

Chanzo: Mwananchi
 
Imebainika asilimia mbili tu ya Wanaume ndiyo wana uelewa kuhusu Saratani Mkoani Mwanza, hivyo kuwafanya baadhi yao kupoteza maisha kwa ugonjwa huo bila kujitambua...
Matumizi ya seli shina kwa wagonjwa au waginjwa watarajiwa wa sukari ni lazma

Piga kwa naelezo zaidi
Dr Ben
0699254400
 
Back
Top Bottom