Utafiti: Tanzania inaongoza kwenye listi ya nchi zenye watu wasiokuwa waaminifu.

mjasiliaupeo

JF-Expert Member
Apr 21, 2013
2,162
3,086
Utafiti umefanywa na wanafunzi wa University of Nottingham Uingereza ukihusisha nchi 159, wanafunzi wa chuo kikuu cha Nottingham wamefanya utafiti wa kugundua ni nchi zipi zinaoongoza kwa uaminifu au ukweli duniani, utafiti umefanywa ukihusisha nchi 159 ikiwemo Tanzania.
Wanafunzi hao wamefanya tafiti huku wakichanganya na data za 2003 za ukwepaji kodi, rushwa na udanganyifu katika siasa lakini wamegundua kuwa nchi za Lithuania, Uholanzi, Uingereza, Sweden, Ujerumani na Italia zimetajwa katika list ya nchi zinazoongoza kwa uaminifu.
Wakati nchi za Tanzania, China, Uturuki, Poland na Morocco zimetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza watu wake kutokuwa waaminifu, utafiti huo unaeleza kuwa watu wanaoishi katika nchi zenye rushwa na siasa za udanganyifu wamekuwa sio waaminifu au wakweli, wakati watu wanaotokea katika nchi ambazo hazina rushwa na ukwepaji kodi ni waaminifu.
Tafiti zimefanyika katika chuo kikuu cha Nottingham Uingereza, lakini kimetajwa kufanya majaribio kwa kuhusisha vijana 2,586 wenye wastani wa umri wa miaka 22 kutoka nchi 23 zikiwemo Vietnam, Morocco, China , UK, Hispania, Sweden, Italy na Czech Republic. Utafiti huu umetolewa na dailyamail.co.uk March 11 2016.
IMEANDIKWA : dailymail.co.uk

www.dailymail.co.uk/sciencetech/article-3484297/The-British-Dutch-honest-world-people-Tanzania-s-corrupt-politicians-are.html
 
Mimi pia naona hali ya uaminifu inazidi kupungua miongoni mwa watanzania. Kwa mfano sasa hivi ukimtuma fundi Wa kujenga bila kumsimamia kwa karibu lazima atakuibia
 
Duh, kama tumeweza kuiovertake China basi sisi ni balaa.
f1bb431d398b761c9d6c7cd4ab9f3c25.jpg
 
hilo nalo linataka utafiti wakati wao kila mwaka wanaturudishia chenji ya mikataba mibovu inayofanyika huko huko na kulipwa huko...rushwa
 
Bahati mbaya sana, hili tatizo linaanzia ngazi ya familia. Ndio maana hata cases za infidelity zimekuwa nyingi kila siku. Watu ni waongo, hawana uaminifu hata kidogo.
 
Hili wala halina ubishi,Watanzania ni waongo sana.
Uongo kila sekta,mapenzi,biashara n.k
 
hasa watu wa dar, dar hawana uaminifu, tofauti na watu wa mikoani...huu utafiti ulilenga watu wa dar
 
Mimi naona hata dini zimeshindwa kazi. Kama dini zingefanya kazi vizuri matatizo kama ya wizi, rushwa na uongo yangepungua. Tatizo naona taasisi, majengo na shughuli za kidini zinaongezeka ila upande mwingine uaminifu unapungua.
 
Back
Top Bottom