Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Utafiti mpya wa kimataifa uliofanywa na Ipsos Global Trustworthiness Index 2024 unaonesha kuwa madaktari ndio taaluma inayoaminika zaidi na watu duniani kote. Zaidi ya asilimia 58 ya washiriki walisema wanawaamini Madaktari, ikifuatiwa na Wanasayansi (56%) na Walimu (54%).
Utafiti huo ulihusisha watu 23,530 walioko chini ya umri wa miaka 75 kutoka nchi 32, na ulilenga kupima kiwango cha uaminifu kwa taaluma mbalimbali.
Baada ya madaktari, wanasayansi na walimu, taaluma nyingine zilizoonyesha viwango vya juu vya kuaminika ni: Wahudumu wa migahawa (44%), Jeshi (43%), Polisi (38%), Raia wa kawaida na majaji (38%).
Hata hivyo Wanasiasa wameendelea kutoaminika zaidi, wakiwa na asilimia 15 pekee ya uaminifu, 'Influencers' wa mitandao ya kijamii (15%), Mawaziri wa serikali (20%)
Vipi mdau, wewe nani zaidi?