Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Utafiti uliofanywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu Cha Muhimbili kwenye machinjio ya kuku ya Shekilango na Manzese umegundua uwepo wa kiwango kikubwa cha dawa za kuua bakteria ambazo wafugaji huzitumia katika kuwatunza.
Watafiti hawa wamebaini uwepo wa kiasi kikubwa cha dawa ya tetracycline kinachozidi uhitaji wa dozi ya kawaida ya binadamu kwa siku. Aidha, dawa za sulphonamide zimethibitika kuwepo pia kwenye kuku hawa.
Utafiti huu unaibua sintofahamu kubwa kwenye nyakati hizi ambazo dunia inapambana na usugu wa vimelea unaosababishwa na matumizi mabaya ya dawa za antibiotics.
Madhara ya muda mrefu ya kula kuku wenye kiwango kikubwa cha dawa hizi ni kutengeneza jamii yenye watu walio na usugu wa vimelea. Jambo hili huongeza mzigo wa kiuchumi kwa watu, vifo pamoja na kuongezeka kwa ugumu katika kutibu magonjwa ya kawaida yanayosababishwa na bakteria mfano UTI, nimonia, kisonono, Kifua Kikuu pamoja na Kaswende.
Jambo hili linapaswa kuangaliwa kwa tahadhari kubwa kabla halijatela madhara makubwa zaidi kwa kuwa matumizi holela ya dawa za antibiotics kwa wanyama wakiwemo kuku huchangia uwepo wa kiasi kikubwa cha dawa hizi kwenye nyama na mazao yao mengine yakiwemo mayai.
REJEA
Chapisho: MDPI
Tarehe 8 Septemba, 2022