Utafanyaje?

Mkeshahoi

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
2,469
281
Fikiria kidume na mbavu zako ulikuwa na mpenzi wako siku za nyuma..mkazinguana mkaaachana kwa ngumi na matusi...kila mtu akaendelea na maisha.

Leo una maisha yako lakini bahati mbaya umepata maradhi na unahitaji tiba. unapelekwa hospitali na baada ya vipimo unaambiwa unaihitaji uapasuaji wa maeneo yako nyeti.... na unapangiwa siku.

Siku ya siku unasainishwa kitabu(pamoja na familia yako) kukubali matokeo ya upasuaji. Unaingizwa chemba tayari kwa shughuli. TAHAMAKI unagundua kuwa daktari mkuu atakaekufanyia upasuaji ndo yuleeeee XXXX wako na tayari anankudunga sindano awe nusu kaputi ....
UTAFANYAJE Mwanamume?:msela:
 
Naomba prior break nikutane na ndugu zangu kwanza, halafu nawaambia ukweli kuwa mmoja wa wahudumu ni ex wangu ambae tuliachana kwa ugomvi mkubwa.

Mchawi mpe mwanao amlee.
 
Ndio maana tunatakiwa tusamehe na kujiosha kwa wale tunaowakosea, Ni muhimu sana kupunguza jazba na kiburi kwenye mambo haya ya mahusiano. Sawa tumegombana tumetukanana lakini walau baada ya muda fulani tafuteni namna ya kuwekana sawa, kwamba bwana yale yalitokea tusameheane ni ubinadamu na pengine Mungu hakupanga tuwe pamoja kivile. Hata kama mtu atakataa msamaha lakini moyoni atakuwa anajua jamaa kaniomba msamaha, na litakuwa linamsumbua hilo kila akijaribu kukutengenezea ubaya.

Sio hospital tu, duniani hapa tutakutana popote na mbya zaidi ni huko kwene kufa au kupona huko.
 
hapo umenena mkuu ni vema kusawazisha mambo kabla baya zaidi halijatokea.
 
Ndio maana tunatakiwa tusamehe na kujiosha kwa wale tunaowakosea, Ni muhimu sana kupunguza jazba na kiburi kwenye mambo haya ya mahusiano. Sawa tumegombana tumetukanana lakini walau baada ya muda fulani tafuteni namna ya kuwekana sawa, kwamba bwana yale yalitokea tusameheane ni ubinadamu na pengine Mungu hakupanga tuwe pamoja kivile. Hata kama mtu atakataa msamaha lakini moyoni atakuwa anajua jamaa kaniomba msamaha, na litakuwa linamsumbua hilo kila akijaribu kukutengenezea ubaya.

Sio hospital tu, duniani hapa tutakutana popote na mbya zaidi ni huko kwene kufa au kupona huko.

Kweli Bible study ni kiboko . . . :roll::roll:
 
utahisi umepona na utakomaa utoke humo..fikiria baada ya operesheni unajigundua si rijali tena... Mtuhumiwa wa kwanza lazma takuwa X wako...
 
duh hapo huna ujanja maana nusu kaputi ishaanza kuingia ile unataka kuongea tu domo linakuwa zito unalala. Basi hapo kila kitu kinabaki kwa yule aliye juu
 
Daktari aliyekula kiapo atamhudumia mgonjwa bila kujali past history ya mgonjwa. Pia ni vigumu kufanya ubaya wowote sababu kwenye chumba cha operation hawi peke yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom