Utafanya nini endapo mpenzi wako kaku-block?

Utafanya nini endapo mpenzi wako kaku-block?

Salaam wakuu,

Heri ya Christmas in advance. Naombeni ushauri wenu.

Yapata miezi mitatu namiss na kutamani kuyarejesha mahusiano yangu ingawaje imeniwia vigumu kabisa kutokana na kublokiwa katika njia zote za mawasiliano ya kijamii.

Sababu ni kuhisiwa nime-CHEAT lakini katika ukweli halisi sijafanya hivyo wala sijawaza kufanya; natamani mpenzi wangu anipe walau nafasi niweze kuzungumzia hili labda atanielewa lakini amekuwa akinikwepa na kutotaka kuniona kabisa. Mbaya zaidi kani-block kila sehemu za mawasiliano.

Kwa wataalamu wa mahusiano, nini naweza kufanya kuyaokoa mahusiano yangu maana bado nampenda na kuwa na tofauti naye kumeniathiri sana katika harakari zangu.

Nimetumia marafiki zake lakini bado hakuna dalili njema ya marudiano sababu kila contact nitakayo mtafuta, akijuwa ni mimi tu, nachezea kufuli.

Kiukweli inaniuma hasa mwaka mnaenda kwisha bila mapatano, na ukizingatia mazingira ya yeye kuhisi nimem-CHEAT yana asilimia ndogo sana.

Na kuhusu mimi binafsi, nampenda sana na sijawahi waza kuchepuka since naanza naye relationship.

Imebidi kuomba basi kama imefika kikomo aseme huenda moyo ukawa na amani lakini hayupo tayari kuwa wazi kama bado ananipenda au la.

Wataalamu wa mahusiano tusaidiane katika hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unampenda yeye hakupendi na kapata bwana mwingine kafikiria njia ya kukuacha ndo kapata huo upenyo wa kukuangushia jumba bovu ndo maana hakupi nafasi ya kujieleza anajua utamshinda tu kwa sababu huja cheat!!.. Kiufupi ushaachwa endelea na mambo mengine!
 
Unampenda yeye hakupendi na kapata bwana mwingine kafikiria njia ya kukuacha ndo kapata huo upenyo wa kukuangushia jumba bovu ndo maana hakupi nafasi ya kujieleza anajua utamshinda tu kwa sababu huja cheat!!.. Kiufupi ushaachwa endelea na mambo mengine!
Fact, Jamaa ajiongeze tuu ukiona mpenzi wako umemkosea au kahisi umemkosea na kaendelea kusimamia msimamo hataki usuluhishi anataka shali tuu, ujue huyo sio riziki!! Bwaga manyanga acha kulia tumia madhaifu yake kumsahau kabisa, usikumbuke mazuri yake jitahidi kukumbuka mabaya yake, Utamsahau tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Dada mmoja nilikuwa nampenda ila Mauza uza haya ndo yalinifanya Kukata tamaa, Mara aku Block mara akudanganye
 
Back
Top Bottom