Utabiri wa Shehe Yahaya bado unaishi

Utabiri wa Shehe Yahaya bado unaishi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,810
Reaction score
831,023
Sheikh Yahya Hussein, aliyekuwa mmoja wa wapiga ramli maarufu sana nchini Tanzania, Ingawa kauli zake hazikuwa sehemu ya tafiti rasmi za kisayansi wala siyo maandiko ya kiroho yaliyo katika vitabu vitakatifu, ziliwahi kuvutia hisia za watu wengi hasa alipokuwa akizungumzia masuala ya kisiasa kwa mtazamo wa kiunajimu (astrology).

Kauli hiyo inayodaiwa kutolewa na Sheikh Yahya inasemekana ilitabiri kwamba:

1. Baada ya vipindi viwili vya Rais Jakaya Kikwete (2005–2015),

2. Angetokea Rais mweusi, mchapa kazi, na mcheshi sana – sifa ambazo wengi wameziunganisha na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli.

3. Rais huyo angebaki madarakani kwa kipindi kifupi tu, jambo ambalo lilitokea kwani Magufuli alifariki dunia akiwa bado katika muhula wake wa pili mwaka 2021.

4. Baada yake, Tanzania ingempata Rais mwanamke – na kweli, Samia Suluhu Hassan alichukua nafasi hiyo na kuwa Rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania.

5. Hatimaye, upinzani kuchukua nchi ..✌🏿💪🏿
Huu utabiri bado unaishi kwakuwa Sheikh Yahaya hakuweka kikomo cha muda kwamba itakuwa wakati wa uchaguzi mkuu 2025
Hivyo wanaondelea kubeza wanajifariji ama hawajui kuupa muda wakati
1763299728363.jpg
 
Hivi ni kweli alitabiri hivi?

Mbona kama JamiiCheck ya hapa JF waliwahi kukanusha?

Kama ni kweli, basi huyu bwana hakuwa mtu wa kawaida
 
Nilimsikia
Hivi ni kweli alitabiri hivi?

Mbona kama JamiiCheck ya hapa JF waliwahi kukanusha?

Kama ni kweli, basi huyu bwana hakuwa mtu wa kawaida
Kwa sikio langu nilimsikia 'bingwa wa utabiri afrika mashariki na kati' marahemu sheikh yahya akisema hivi...

kwenye mkutano na waandishi Kama sikosei...

I think ilikuwa mwaka 2006 kama sikosei nikiwa A' level.
Kipindi kile ilichukuliwa kawaida huu utabiri... haikuchukuliwa kwa uzito huu utabiri...

ANGALIZO!!! Lakini Hayo maneno ya mwisho "Upinzani kuchukua nchi" sheikh HAKUYASEMA!... Yameongezwa!!!
 
images.jpeg
 
Ukisoma between the line huyo mwanamke aliyetajwa ndiye sababu ya anguko la ccm na nachoona soon kuna chama kipya kinaenda kutokea kikihusisha wazalendo walikuwa ccm na wale wazalendo wa vyama vingine na hapo ndipo watakapo chukua Dola.
 
Bado unapumua huo...japo timu ilishapigwa 2
 
Zwazwa analeta utabiri kwenye karne ya sayansi na teknologia.Danganya wajinga wenzako.Sikushangai kwani hata mada zako zime base kwenye ushirikina uchawi na nguvu za giza.Alifikiriaye mjinga ndio humtokea.
 
Back
Top Bottom