Utabiri wa nyota leo jumatano 18/6/2025

Utabiri wa nyota leo jumatano 18/6/2025

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,144
Reaction score
3,459
UTABIRI WA NYOTA LEO JUMATANO 18/6/2025
1750240126588.jpg

Kumbuka kwamba nyota zina athari ya moja kwa moja katika maisha yetu na yeyote asiyefuata nyota yake hawezi kamwe kusonga mbele kwa maana anaishi nje ya asili yake♐

Ikiwa unavutiwa na utabiri huu basi jiunga nasi whatsapp kwa kubonyeza link ya group letu la whatsapp hapo chini♐

🌘🌘🌘🌘 BAKOLA YA UZIMA 🌱🌳
🌘🌘🌘🌘

Ikiwa unahitaji tiba za kiroho na asili ama dawa za mvuto, ndagu na k karibu whatsapp, namba ipo hapo chini♐

☀☀☀☀

🔯🛐🕉🕎🚺♈♊♋♌♍♎♏♐♑♒♓⛎

UTABIRI WA LEO
♐♐♐♐

♈NYOTA YA PUNDA
21st March to 20th April

Leo mambo yako yote yako vizuri utakuwa na furaha iliyopitiliza. kule kutokuelewana na mwenzio kumeisha penzi limerudi upya tegemea kupata habari za posa uchumba na ndoa.

Ile shughuli uliyoiomba utafanikiwa kuipata ikiwa utamshirikisha mwanamke.

Utatimiza ahadi na kuongeza maelewano. Uaminifu utadumishwa. Mambo ya kihisia yatasawazishwa.

♉NYOTA YA NG'OMBE
21st April to 21st May

Jiepushe na matumizi ya vyombo vya moto kwani vitakusababishia madhara. Baadhi ya mambo hayajakaa sawa ndani yako kama utakuwa umelegea utasumbuka sana. Leo huenda ukajikuta kwenye ugomvi mkubwa kazini au kwenye shughuli zako nyingine tumia nguvu.

Furaha na faraja itaongezeka katika maisha yako ya ndoa. Katika mahusiano kila kitu kipo sawa na utafurahia pia mahusiano yako ahadi za upendo zitakuwa nyingi sana siku ya leo.

♊NYOTA YA MAPACHA
22nd May to 21st June

Utapokea salamu au mgeni ambaye ni jamaa yako wa karibu kutoka mbali. Leo ni siku ambayo unahitajika kufanya mageuzi makubwa katika shughuli zako. Ile mipango yako haitatimia mpaka utakaporudi safari yako.

Watoto wako wana vita au uadui wafanyie maombi ya hapa na pale ili kuwaimarisha zaidi kimasomo na kiutafutaji kwakuwa wote wanauwezo mzuri ila uadui mchache unawayumbisha.

♋NYOTA YA KAA
22nd June to 22nd July

Unahitajika nyumbani na wazee ukakabidhiwe majukumu ya uongozi wa familia. Kutana na viongozi watakupa maelekezo. masuala ya kazi na biashara vitakuendea vema fanya kadri uwezavyo.

Maradhi yatasumbua nyumba yako kwa maana ya mmeo au mkeo au wanao, maradhi haya yanatokana na kitu kilicholetwa kutoka nje hivyo wape tahadhari ya kupokea vyakula vya nje kwa siku hizi mbili hadi tatu ili kujihadhari na jaribio hilo la maradhi.

♌NYOTA YA SIMBA
23rd July to 23rd August

Marafiki watakuwa misaada mkubwa kwako usikae mbali nao kuna jambo watakushirikisha. Kipindi hiki utajikuta umepata matumaini na kufanikiwa kuzidhibiti shughuli zako usikose kwenye mkutano utakao alikwa.

Katika mahusiano utakuwa imara na mawasiliano yatakuwa bora na mwenza wako. Utakuwa na hamu ya kufanya maendeleo makubwa.

♍NYOTA YA MASHUKE
24th August to 22nd September

Utajikuta unapingwa na kila mtu ni siku ambayo utapambana na vikwàzo vingi. Lile wimbi la kukosa bahati bado linakuandama omba msaàda utapewa lakini hautakidhi shida zako.

Utapokea ujumbe mzuri leo kila mtu atakuwa na furaha akiwa karibu yako ikiwa utamtembelea mapema mganga wako.

♎NYOTA YA MIZANI
23rd September to 23rd October

Anzisha mahusiano na mtu mwingine achana na huyo uliyenae kwani hutapata mabadiliko yoyote. Siku ya leo unatakiwa kujali mipango yako ya maisha tafuta njia mpya za kujiongezea kipato.

Unashauriwa kufanya shughuli yoyote ile kwank siku ya leo itakwenda vizuri na kukuletea mafanikio.

♏NYOTA YA NG'E
24th October to 22nd November

Huitaji kutumia nguvu nyingi siku ya leo kila kitu kiko tambarare, kuhusu kazi utafanikiwa kuipata, masuala ya pesa yasikuumize kichwa utafanikiwa kupata bila usumbufu, wakumbushe unaowadai na fuatilia stahiki zako.

Utaonyesha ukarimu katika mahusiano yako. Katika mahusiano yako utakuwa na mshikamano na mpenzi wako huku hisia za kimapenzi zitaongezeka. Leo unaweza kwenda safari na mpendwa wako.

♐NYOTA YA MSHALE
23rd November to 22nd December

Kaa mbali na jamaa zako jitahidi kutofanya mawasiliano nao. Ile shughuli unayotaka kuanzisha usimuhusishe jamaa yako yoyote atakuchelewesha. Punguza kuwatembelea mara kwa mara rafiki zako. Badilisha mpango wako wa awali kuhusiana na safari.

Katika siku ya leo utamu utaongezeka kila mahala na kuifanya siku yako kuwa imara zaidi.

♑NYOTA YA MBUZI
23rd December to 20th January

Kila unachofanya hakitakwenda sawa, kama utakutana na viongozi wako kuna nafasi kubwa ya kupata mafanikio kama utazingatia ushauri wao jishushe kidogo nazi haishindani na jiwe kuwa mtulivu.

Utakuwa na ukaribu na wanafamilia wako. Utakuwa mtu muhimu leo kwa mpenzi wako hususani katika shida zake. Marafiki watakuwa kando yako leo.

♒NYOTA YA NDOO
21st January to 19th February

Uko kwenye nafasi nzuri ya kupata msaada na mkopo ikiwa utashirikiana na rafiki yako mwenye umri mdogo. Utapokea mualiko wa sherehe nenda lakini usiende peke yako. kile unachotaka kununua kinunue tu kitakusaidia hapo baadaye kwenye masuala ya mtoto.

Utabakia kuwa mvumilivu katika mahusiano. Epuka kutenda kwa hisia. Usipuuze hisia za wapendwa wako.

♓NYOTA YA SAMAKI
20th February to 20th March

Utatuhumiwa jambo kuhusiana na ugonjwa hata hivyo unashauriwa kukaa kimya maana kutazuka ubishi na kutoelewana. Chunga vitu vyako kuna wizi utatokea.

Taarifa muhimu zinaweza kupokelewa. Familia yako itakusaidia katika maswala yako. Fanya kazi kwa kushauriana na watu wako wa karibu.

Maalim dogoli kinyamkela 💀☠️ mtabiri wa nyota Yako na mambo mbali mbali yanayo husiana na nyota zenu.
 
Mimi ya kwangu mbona naona haihusiani kabisa na mimi au kuna utaalamu wa kuzisoma na kuzielewa hizo nyota
 
Kwenye Elimu hii nadhani hujabobea we jikite kwenye kutibia utafika mbali ila haya mambo ya Nyota unabahatisha.
 
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom