Utabiri wa hali ya umeme kwa sikuya leo

danione

Member
Oct 26, 2011
58
5
Pepo za umeme zitavuma taratibu kutoka upande wa kusini mwa Dar es Salaam kuelekea upande wa Kaskazini. Hivyo kutakuwa na umeme mchache maeneo yote ya Jiji na ngurumo nyingi za Jenereta pande za Kariakoo, Mwenge, Posta na maeneo yote ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Na kwa wakati wa usiku watu wa Mbagala, Kigamboni, Kimara, Mtoni na maeneo yote ya jirani wilaya ya Temeke na Kinondoni kutakuwa na Kiza kisichojulikana mwisho wake.
Maeneo ya Sinza, Mbezi na Tegetakutakuwa na miunguromo ya jenereta hapa na pale nyakati za usiku. Hii ni kutokana na familia chache zinazotumia jenereta nyakati za usiku
Utabiri huu umeletwa kwenu na Mamlaka ya Utabiri wa Nguvu za umeme waTanesco, Ubungo ghorofa ya Pili.
Nawatakia siku njema. Ahsanteni.
 
baada ya kupata utabiri wa hali ya umeme. Tumalizie kwa muktasar wa khabar, rais wa tz asema kutokana na gesi iliyogundulika mgao wa umeme utapungua asilimia mia hasa maeneo ya ikulu .........,... msomaji wako alikuwa realness ukweli. Usikose kipind kijacho cha rushwa ni rafiki wa haki
 
Pia tupate mazungumzo baada ya habari!
Mhariri: Mh. waziri unawaambia nn wananchi kuhusu mgao unaondelea?
Ngeleja: Asante sana ndugu mhariri kwanza ningependa kuwashukuru wananchi wa jimbo langu kwa kunichagua, pia kumshukuru Mh. raisi kuniteua kuwa waziri mwenye mamlaka makubwa ya kugawa haki ya umeme na nafikiri utakuwa shahidi jinsi watu walivyo wabishi kwa kuwasha majenereta huku wakijua Tanesco ndio mwenye haki miliki ya mgao pasipo ubishi, vilevile nawaasa wasipende kukanyaga nyaya zilizodondoka maana mgao utapokuwa unamia sehemu nyingine wanaweza rushwa ikawa shida maana madaktari nao wameanza mgao pia .......
Mhariri: nashukuru mh. waziri naona muda umetutupa mkono nakutakia ukomae na hali halisi maana nguvu ya umma ni soo!
 
Back
Top Bottom