Utabiri: Kilichotokea kwa Uhuru Kenyatta kitatokea kwa Edward Lowassa

Hivi Watanzania mmelogwa na mchawi gani? Yaan EL ni mtu wa kufikiria kuongoza Tanzania wakati kila siku mnalia umeme umeme, maisha magumu maisha magumu, nani katufikisha hapa kama si EL? Bila umeme maendeleo yatakujaje, bila viwanda kuzalisha kwa kutumia uchumi utakuaje, ajira itakujaje kwa vijana? EL Richmond ndio wametufikisha hapa, ok ana hisa za kwenye Vodacom, vodacom hawalipi kile wanavuna kuchangia pato la taifa je akiwa Rais si aiatkuwa na hisa kila kampuni?
EL ni mwizi, mroho wa mali, anakula bila kunawa, yuko radhi kuuza nchi mradi itampa pesa. Ni mtu haridhiki, amekuwa Waziri wa Ardhi akakomba ardhi yote amejenga majumba kila mji, akawa waziri ofisi ya Rais inayoshughulikia maafa akala misaada yote, watu wa kusini wanajua ilo, amakuwa waziri mkuu Richmond, Vodacom, nani hasiyemjua wakati akiwa mkurugezi mkuu wa AICC alivyokuwa hana kitu anatembelea kibito (Vokswagen) leo EL mnamonaje, kapata wapi pesa. Leo anamwaga mapesa makanisani na misikitini anapata wapi nguvu hiyo kama hajawaibia Watanzania.
Swali lingine Watanzania mmelogwa na nani kufikiria bado CCM inaweza kukutawala tena. Miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru tunatambaa bado? Yote nani hasiyejua kwamba CCM imetufikisha hapo? Amka jamani Watanzania tuache ukondoo wa mawazo, tutoke kwenye ulevi wa kufikiri CCM na bila CCM hatufiki. Tufike wakati tuseme basiii. CDM imekuja na ipo na mnaona inafanya nini lakini bado watu wanota kasumba ya CCM. angalia wabunge wenu wa CCM ni rudo lakini wanafanya nini? Angalia wabunge wa CDM ni wangapi lakini wanafanya nini? Ni wakati wa kuamka jamani nawasii hata kama kurongwa kwenu hakuna mganga lakini basi jitambue wenyewe. nani hasiyependa maendeleo ya jumla kwa watoto wetu wa baadae, kwa dada, shangazi, bini babu zetu uko vijijini.
AMKENI USINGIZI
 
Nahisi Ngoma itakuwa ngumu kama 2015 atasimama Lowasa VS Dr. Salaa.

Maoni yangu ni kwamba tunahitaji Rais mwenye maamuzi kututoa hapa tulipo
 
Chadema haina mpinzani kama kweli Lowassa ndio aliyebaki CCM ni uchochoro kwa chadema maana Lowassa alishachafuka na wala hasafishiki.
 
KAMWE KAMWE KAMWE nasema tena KAMWE HUWEZI KUMSAFISHA EL KWA KEYBOARD.......nakushangaa unamlinganisha El na uhuru a u serious??????
Unamlinganisha lengwanani na Mh rais wa kenya?????
Unamlinganisha fisadi na mtu aliyepata utajiri wake kihalali(uhuru)????yani baba awe rais mtoto awe maskini unadhani huyu ni makongoro?????
Ridhiwani ni mtoto wa raisi na ni tajiri mkubwa.....uhuru ni mtoto wa raisi kwanini yeye asiwe tajiri??????

Kwa maoni kama haya mkuu,nahisi mimi ni mwendawazimu!kwani sijakuelewa kabisa!kama si hivyo basi basi kinyume chake ni sahihi!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Chadema haina mpinzani kama kweli Lowassa ndio aliyebaki CCM ni uchochoro kwa chadema maana Lowassa alishachafuka na wala hasafishiki.

Kama silaa alishindwa kuendelea na utumishi wa mungu kwaajili ya tamaa ya raha za dunia je akiingia ikulusi ndio itakuwa balaa kabisa. vilevile akashindwa kukaa na mke wake wa ndoa akamwacha kwasababu ya hawara atakuwa na usafi gani huo mnaousema ? Na uzee wote huo badala ya kutulia na mke wake pamoja anakaa kukimbizana na hawara . anausafi gani huo mtu ameshindwa kuendesha na kusimamia familia yake mwenyewe ndio ataweza kusimamia nchi ?
 
Mimi natoa tahadhari kwa Watanzania wenzangu wenye mapenzi mema, hawa majambazi hawana masihara na hawatanii na wanamaanisha, kwanza Lowasa haamini katika Bahati bali mikakati.

Hii ni picha iliyopigwa leo akitapanya mapesa kwa Masheikh maana makanisa wameshazitafuna mpaka zimewakifu, huyu akiendelea kuchekewa na kukenuliwa meno tu hakuna sanduku la kura la kumwangusha huyu mtu, si kwa sababu anakubali bali huyu ni zaidi ya Shetani hawa ndio waliotuletea JK.

7.jpg
 
Ndugu zangu wanaJamvi,

Nianze kwa kuwaomba radhi wapinzani wa Edward Lowassa bila kumsahau Mwandishi maarufu wa makala zinazofikirisha Bw. Mbwambo wa gazeti la Raia Mwema. Najua watakuwa wamefungua uzi huu wakiwa wamefura kwa hasira na kujiandaa kuchangia kwa jazba na maneno ya kashfa dhidi yangu. Lakini naomba mnivumiliea kuchangia mawazo yangu kwenye jamvi hili ambamo “WE DARE TO TALK OPENLY”.Kwa kipindi kifupi nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Kenya na hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliokamilika hivi karibuni, ambapo akina Bwana Wadogo Uhuru Kenyatta na mwenzie William Rutto wameibuka washindi. Jana waliapishwa kushika madaraka hayo makubwa ya taifa la Kenya. Kabla ya kufika hapo, safari yao ilikuwa ni ndefu, yenye mabonde na milima mikubwa yenye miiba na kila aina ya karaha.

Ikumbukwe kuwa vijana hao, ni washtakiwa wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC na kesi bado inarindima kwenye Mji wa The Hegue nchini Uholanzi. Wakati wa kampeni, Uhuru Kenyetta alikuwa na vigingi viwili vikubwa ambavyo bila kujipanga kisawasawa, vingemwangusha na kukosa nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa nchi. Kigingi cha kwanza kilikuwa ni kesi inayoendeshwa na ICC, ambapo wapinzani wake na hasa Mzee Odinga walikuwa wakitumia kama turufu ya kampeni. Kwamba kitendo cha kushtakiwa tu na ICC whether kwa makosa ambayo ni kweli alifanya au hakufanya, hilo lilikuwa ni doa ambalo haifai mgombea wa nafasi hiyo muhimu kuwa nayo. Hata mbele ya macho ya mataifa makubwa doa hilo lilikuwa linaoneka kuwa ni kubwa na kumpunguzia uwezekano wa kushinda uchaguzi. Kigingi cha pili kilikuwa ni utajiri. Ni jambo lililo bayana kwamba Uhuru ni miongoni mwa matajiri wakubwa nchini Kenya. Mbali ya mashamba makubwa, inasemekana Uhuru anamiliki biashara kubwa mbalimbali zinazomwingizia mabilioni ya shilingi za Kenya. Hiyo nayo ilikuwa ni turufu kwa wapinzani wake wakati wa kampeni.

Kama nilivyotarajia, Bw. Uhuru alijipanga kisawasawa kukabiliana na vigingi hivyo viwili. Kwa wale waliopata fursa ya kushuhudia mdahalo uliorushwa moja kwa moja (live) kupitia luninga, watakubaliana nami kuhusu hiki ninachosema. Pamoja na kubanwa na maswali mazito na wapinzani wake hususani Mzee Odinga na Mama Martha Karuwa, kijana Uhuru alipangua hoja zao zote kwa ustadi mkubwa na kwa kujiamini sana.
Hoja yake kubwa ilikuwa kwamba wakenya wanayajua yote hayo na waachwe waamue. Kila ninapotafakari ushindi wa Uhuru Kenyatta, maneno hayo, yamekuwa yakijirudia kichwani mwangu mara kwa mara na nimebaini kuwa yana ujumbe mzito katika medani za kisiasa na hasa siasa zinazoendeshwa kidemokrasia. Katika tafakuri yangu hii, nimemkumbuka mwanasiasa maarufu hapa nchini Mhe. Edward Lowassa maarufu humu jamvini kama EL. Huyu jamaa tangu alipojiuzulu uwaziri mkuu kwa kashfa ya Richmond, amekuwa akisakamwa sana na wapinzani wake kupitia vyombo vya habari vya magazeti, luninga na redio kwamba ni fisadi mkubwa. Imefika wakati mtu hawezi kutaja ufisadi bila kumtaja Edward Lowassa. Wengine wanasema ni tajiri mkubwa na utajiri wake ulitiliwa shaka hata na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Nyerere. Mimi binafsi siwezi kumtetea kwani mengi yanayosemwa juu yake hayajawekwa hadharani kwa kiwango cha kuwaaminisha akina Thomaso. Wakati kampeni ya kumchafua ikiendelea, yeye ameendelea na harakati zake za kiasiasa. Kamwe hajakata tamaa na anatumia mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa anarejea kwa kishindo. Mbaya zaidi (kwa wapinzani wake) utendaji wa serikali iliyopo madarakani hivi sasa unaweza kwa namna moja au nyingine kuwa kichocheo cha umaarufu wake kuongozeka kwani wapo baadhi ya wananchi wanaoamini kuwa kuondoka kwake ni moja ya sababu ya kupwaya kwa serikali.

Kwa kipindi kifupi nimeshuhudia maongezi mitaani yakiashiria kupanda “chati” kwa EL na hivi karibuni wakati wa mohojiano kwenye kipindi cha Medani za Siasa kupitia Startv, Bw. Hussein Bashe alieleza bayana na kwa kujiamini kabisa kwamba mtu anayeamini anaweza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo ni Edward Lowassa. Bashe alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa chama chake kwamba kihakikishe kinazingatia matakwa ya demokrasia wakati wa kumpata mgombea wake wa nafasi ya urais ili apatikane mtu ambaye itakuwa rahisi kwa chama kumnadi mbele ya wananchi. Kwa “wanaosoma katikati ya mistari”, watakubaliana nami kwamba Bashe anaamini kuwa demokrasia ikishika mkondo wake ndani ya chama, basi Edward Lowassa hana mpinzani wa kumzuia kuibuka kidedea. Kwa kawaida, demokrasia inasisitizwa na kuhimizwa na upande wenye imani na wapiga kura wake. Mtu asiyejiamini hawezi kuhimiza demokrasia katika kupata nafasi ya uongozi. Mbinu pekee anayoweza kutumia ni udikteta. Kwa hiyo, nataka nihitimishe mawazo yangu kwamba mazingira yanayomkuta EL yana mfanano wa aina fulani na mazingira aliyopitia Uhuru Kenyatta ingawa siasa za Kenya na sheria zake vinatofautiana kwa kiasi kikubwa na hapa kwetu nchini. Lakini kwa hali iliyotokea Kenya, kamwe tusimbeze EL. Kwa kura za wananchi na haswa katika mazingira tuliyopo hivi sasa, tunaweza kushtukia EL ametua Magogoni kwenye jengo jeupe.

Ndimi Ndashene Mbandu

Penye point ni hapo penye RED... BYE BYE
 
My dear, umesema Uhuru Kenyatta alijitetea mwenyewe basi vivyo hivyo mwache Lowasa ajitetee mwenyewe! Mbona wamtetea au umeahidiwa 'pande'?
 
Kama silaa alishindwa kuendelea na utumishi wa mungu kwaajili ya tamaa ya raha za dunia je akiingia ikulusi ndio itakuwa balaa kabisa. vilevile akashindwa kukaa na mke wake wa ndoa akamwacha kwasababu ya hawara atakuwa na usafi gani huo mnaousema ? Na uzee wote huo badala ya kutulia na mke wake pamoja anakaa kukimbizana na hawara . anausafi gani huo mtu ameshindwa kuendesha na kusimamia familia yake mwenyewe ndio ataweza kusimamia nchi ?
Wewe tukikufuatilia binafsi ni mchafu kuliko nzi wa chooni acha kuingilia maisha binafsi. Je ukiambiwa yote ya Jakaya utayapenda kama kuwa na mahawara 70 wote wakilishwa kodi za watanzania! Je unajua vyeo vya wanawake kwa JK vinapatikana kwa "pillow interview"? Yako mengi acha upuuzi tukimwaga hapa mtahangaika na Rama Ighondu kututafuta bila mafanikio.
 
.... UTABIRI.....

.... a fool will explain things after seeing results ....

... a clever man will explain things b4 they happen.....
 
Siku mheshimiwa Lowassa Alipotangaza kujiuzulu alisema yafuatayo,nitanukuu tu sehemu ya hotuba yake
......."katika kila hoja walizojenga wamesema waziri mkuu ilikuwa hivi. Kulukuwa na shida gani kuja kuniuliza waziri mkuu wanasema ulitoa dekezo hili,ni sawasawa ni kweli. Kulikuwa na shida gani kwa mfano mheshimiwa spika, kufuata utaratibu wa westminster, Kuthibitisha hapa unaposema mwenye Richmond ni flani ukalay on the table records kwamba una ushahidi ni flani.................................nilichofanyiwa mheshimiwa spika napenda kuweka kumbukumbu sahihi sawa,kwamba naona si sahihi, NIMEFADHAIKA SANA, NIMEDHALILISHWA SANA, NIMEONEWA SANA KATIKA HILI. Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijaulizwa. Kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa, tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama...............................................lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni, tunahutubia nchi nzima na kusema waziri mkuu amefanya hiki amefanya hiki amefanya hiki bila kumsikiliza"

Kwa kipindi kifupi nimeshuhudia maongezi mitaani yakiashiria kupanda “chati” kwa EL na hivi karibuni wakati wa mohojiano kwenye kipindi cha Medani za Siasa kupitia Startv, Bw. Hussein Bashe alieleza bayana na kwa kujiamini kabisa kwamba mtu anayeamini anaweza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo ni Edward Lowassa. Bashe alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa chama chake kwamba kihakikishe kinazingatia matakwa ya demokrasia wakati wa kumpata mgombea wake wa nafasi ya urais ili apatikane mtu ambaye itakuwa rahisi kwa chama kumnadi mbele ya wananchi. Kwa “wanaosoma katikati ya mistari”, watakubaliana nami kwamba Bashe anaamini kuwa demokrasia ikishika mkondo wake ndani ya chama, basi Edward Lowassa hana mpinzani wa kumzuia kuibuka kidedea. Kwa kawaida, demokrasia inasisitizwa na kuhimizwa na upande wenye imani na wapiga kura wake. Mtu asiyejiamini hawezi kuhimiza demokrasia katika kupata nafasi ya uongozi. Mbinu pekee anayoweza kutumia ni udikteta. Kwa hiyo, nataka nihitimishe mawazo yangu kwamba mazingira yanayomkuta EL yana mfanano wa aina fulani na mazingira aliyopitia Uhuru Kenyatta ingawa siasa za Kenya na sheria zake vinatofautiana kwa kiasi kikubwa na hapa kwetu nchini. Lakini kwa hali iliyotokea Kenya, kamwe tusimbeze EL. Kwa kura za wananchi na haswa katika mazingira tuliyopo hivi sasa, tunaweza kushtukia EL ametua Magogoni kwenye jengo jeupe.

Unazungumzia fanana za Uhuru na EL bila ya kuziainisha. Uhuru alipoona Kanu ni kikwazo aliikimbia Kanu na kuanzisha chama chake cha TNA. Swali la kujiuliza EL lini ataikimbia CCM baada ya kuona mwelekeo ni Pemba-2015?
 
7.jpg

Mimi Ningelikuwa EL ningekazania afya yangu kuitunza. Matatizo ya Parkinson hayataki purukshani kama hizi za siasa anatakiwa aondoe msongo wa mawazo na kuondoa tamaa za kidunia ambazo zinapita tu tena mithili ya kasi ya mwewe
 
lowasa ni mzur kiutawala achen uzushi, huwez kuwa CCM ukawa nje ya ufisadi ingawaje kwangu mimi ningependa CCM wa mweke Mwakiembe au Magufuli.
 
Unazungumzia fanana za Uhuru na EL bila ya kuziainisha. Uhuru alipoona Kanu ni kikwazo aliikimbia Kanu na kuanzisha chama chake cha TNA. Swali la kujiuliza EL lini ataikimbia CCM baada ya kuona mwelekeo ni Pemba-2015?[/QUOTE EL hawezi kamwe kuhama CCM na kuunda chama ingine anaogopa kivuli chake mwenyewe huo ujasiri atautoa wapi,anatamani sana Kufanya hivyo nahisi ila hicho kivuli chake ......
 
Hivi Watanzania mmelogwa na mchawi gani? Yaan EL ni mtu wa kufikiria kuongoza Tanzania wakati kila siku mnalia umeme umeme, maisha magumu maisha magumu, nani katufikisha hapa kama si EL? Bila umeme maendeleo yatakujaje, bila viwanda kuzalisha kwa kutumia uchumi utakuaje, ajira itakujaje kwa vijana? EL Richmond ndio wametufikisha hapa, ok ana hisa za kwenye Vodacom, vodacom hawalipi kile wanavuna kuchangia pato la taifa je akiwa Rais si aiatkuwa na hisa kila kampuni?
EL ni mwizi, mroho wa mali, anakula bila kunawa, yuko radhi kuuza nchi mradi itampa pesa. Ni mtu haridhiki, amekuwa Waziri wa Ardhi akakomba ardhi yote amejenga majumba kila mji, akawa waziri ofisi ya Rais inayoshughulikia maafa akala misaada yote, watu wa kusini wanajua ilo, amakuwa waziri mkuu Richmond, Vodacom, nani hasiyemjua wakati akiwa mkurugezi mkuu wa AICC alivyokuwa hana kitu anatembelea kibito (Vokswagen) leo EL mnamonaje, kapata wapi pesa. Leo anamwaga mapesa makanisani na misikitini anapata wapi nguvu hiyo kama hajawaibia Watanzania.
Swali lingine Watanzania mmelogwa na nani kufikiria bado CCM inaweza kukutawala tena. Miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru tunatambaa bado? Yote nani hasiyejua kwamba CCM imetufikisha hapo? Amka jamani Watanzania tuache ukondoo wa mawazo, tutoke kwenye ulevi wa kufikiri CCM na bila CCM hatufiki. Tufike wakati tuseme basiii. CDM imekuja na ipo na mnaona inafanya nini lakini bado watu wanota kasumba ya CCM. angalia wabunge wenu wa CCM ni rudo lakini wanafanya nini? Angalia wabunge wa CDM ni wangapi lakini wanafanya nini? Ni wakati wa kuamka jamani nawasii hata kama kurongwa kwenu hakuna mganga lakini basi jitambue wenyewe. nani hasiyependa maendeleo ya jumla kwa watoto wetu wa baadae, kwa dada, shangazi, bini babu zetu uko vijijini.
AMKENI USINGIZI

Hatuamki Ng'o!
Fisadi Bw.Lowasa, Raisi wa Tz 2015
 
Kwa ufupi unataka kusema mazingira yalliyompa ushindi Uhuru Kenyata yanasadifiana na ya EL. Mfano EL. anatumhuma wakati Uhuru pia alikuwa na tuhuma. EL. ana utajiri mkubwa wakati Uhuru pia ana utajiri mkubwa pia. Lakini unashindwa kuainisha tofauti zao. Ili kumweleza vizuri mtu ni vizuri kumwelewa kwa undani wake. Compare and contrast. Kuelezea tu jinsi wanavyofanana na jinsi wanavyotofautiana pia. Mazingira yanayofanyia shughuli zao pia ni muhimu
Hapa nitajaribu kuelezea jinsi wanavyofanana, wanavyotofautiana katika mazingira tofauti. Ni kweli wote wanatuhuma. Wakati Kinyata anatuhumiwa na ICC kulipiza kisasi kwa watu waliokuwa wanalishambulia kabila lake kupinga ushindi wa Mwai Kibaki, EL anatuhumiwa na WATANZANIA WENZAKE kuwaibia wananchi kupitia Kampuni ya kifisadi Richmond.Utajiri wa Uhuru Kenyata unatokana na urithi wa kifamilia uliotokana na siasa za ubepari wa Kenya tangu Uhuru wa Kenya, utajiri wa EL unatokana matumizi mabaya ya nafasi za uongozi katika nafasi alizopata kushika katika nchi yenye itikadi ya siasa za kijamaa. Umaarufu wa Uhuru Kenyata unatokana na kutetea hoja zake kwa kujiamini wakati EL umaarufu wake unatokana na kuwanunua watu (supporters) kwanjia ya rushwa ukiwemo wewe mtoa uzi huu. Wakati Uhuru hajapata kujiuzulu nafasi ya uongozi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi, EL alijiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu kutokana na kashifa ya Richmoond. Wakati EL. ni bingwa wa kuwazushia tuhuma wapinzani wake na roho yake haishiwi fitina Uhuru yuko radhi kushirikiana na wapinzani ili kujenga Taifa na uchumi imara wa Nchi yake. Wakati EL hutenda kwa kurupuka, sifa ambayo inamfanya aoneke kuwa na uthubutu wa kufanya maamuzi mazito Uhuru utenda na kujibu kwa umakini mkubwa ( rejea majibu yake kwa maswali magumu kwenye mdahalo wa kumtafuta mgombea uraisi wa Kenya 2013.
Ndugu zangu wanaJamvi,

Nianze kwa kuwaomba radhi wapinzani wa Edward Lowassa bila kumsahau Mwandishi maarufu wa makala zinazofikirisha Bw. Mbwambo wa gazeti la Raia Mwema. Najua watakuwa wamefungua uzi huu wakiwa wamefura kwa hasira na kujiandaa kuchangia kwa jazba na maneno ya kashfa dhidi yangu. Lakini naomba mnivumiliea kuchangia mawazo yangu kwenye jamvi hili ambamo “WE DARE TO TALK OPENLY”.Kwa kipindi kifupi nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Kenya na hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliokamilika hivi karibuni, ambapo akina Bwana Wadogo Uhuru Kenyatta na mwenzie William Rutto wameibuka washindi. Jana waliapishwa kushika madaraka hayo makubwa ya taifa la Kenya. Kabla ya kufika hapo, safari yao ilikuwa ni ndefu, yenye mabonde na milima mikubwa yenye miiba na kila aina ya karaha.

Ikumbukwe kuwa vijana hao, ni washtakiwa wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC na kesi bado inarindima kwenye Mji wa The Hegue nchini Uholanzi. Wakati wa kampeni, Uhuru Kenyetta alikuwa na vigingi viwili vikubwa ambavyo bila kujipanga kisawasawa, vingemwangusha na kukosa nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa nchi. Kigingi cha kwanza kilikuwa ni kesi inayoendeshwa na ICC, ambapo wapinzani wake na hasa Mzee Odinga walikuwa wakitumia kama turufu ya kampeni. Kwamba kitendo cha kushtakiwa tu na ICC whether kwa makosa ambayo ni kweli alifanya au hakufanya, hilo lilikuwa ni doa ambalo haifai mgombea wa nafasi hiyo muhimu kuwa nayo. Hata mbele ya macho ya mataifa makubwa doa hilo lilikuwa linaoneka kuwa ni kubwa na kumpunguzia uwezekano wa kushinda uchaguzi. Kigingi cha pili kilikuwa ni utajiri. Ni jambo lililo bayana kwamba Uhuru ni miongoni mwa matajiri wakubwa nchini Kenya. Mbali ya mashamba makubwa, inasemekana Uhuru anamiliki biashara kubwa mbalimbali zinazomwingizia mabilioni ya shilingi za Kenya. Hiyo nayo ilikuwa ni turufu kwa wapinzani wake wakati wa kampeni.

Kama nilivyotarajia, Bw. Uhuru alijipanga kisawasawa kukabiliana na vigingi hivyo viwili. Kwa wale waliopata fursa ya kushuhudia mdahalo uliorushwa moja kwa moja (live) kupitia luninga, watakubaliana nami kuhusu hiki ninachosema. Pamoja na kubanwa na maswali mazito na wapinzani wake hususani Mzee Odinga na Mama Martha Karuwa, kijana Uhuru alipangua hoja zao zote kwa ustadi mkubwa na kwa kujiamini sana. Hoja yake kubwa ilikuwa kwamba wakenya wanayajua yote hayo na waachwe waamue. Kila ninapotafakari ushindi wa Uhuru Kenyatta, maneno hayo, yamekuwa yakijirudia kichwani mwangu mara kwa mara na nimebaini kuwa yana ujumbe mzito katika medani za kisiasa na hasa siasa zinazoendeshwa kidemokrasia. Katika tafakuri yangu hii, nimemkumbuka mwanasiasa maarufu hapa nchini Mhe. Edward Lowassa maarufu humu jamvini kama EL. Huyu jamaa tangu alipojiuzulu uwaziri mkuu kwa kashfa ya Richmond, amekuwa akisakamwa sana na wapinzani wake kupitia vyombo vya habari vya magazeti, luninga na redio kwamba ni fisadi mkubwa. Imefika wakati mtu hawezi kutaja ufisadi bila kumtaja Edward Lowassa. Wengine wanasema ni tajiri mkubwa na utajiri wake ulitiliwa shaka hata na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Nyerere. Mimi binafsi siwezi kumtetea kwani mengi yanayosemwa juu yake hayajawekwa hadharani kwa kiwango cha kuwaaminisha akina Thomaso. Wakati kampeni ya kumchafua ikiendelea, yeye ameendelea na harakati zake za kiasiasa. Kamwe hajakata tamaa na anatumia mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa anarejea kwa kishindo. Mbaya zaidi (kwa wapinzani wake) utendaji wa serikali iliyopo madarakani hivi sasa unaweza kwa namna moja au nyingine kuwa kichocheo cha umaarufu wake kuongozeka kwani wapo baadhi ya wananchi wanaoamini kuwa kuondoka kwake ni moja ya sababu ya kupwaya kwa serikali.

Kwa kipindi kifupi nimeshuhudia maongezi mitaani yakiashiria kupanda “chati” kwa EL na hivi karibuni wakati wa mohojiano kwenye kipindi cha Medani za Siasa kupitia Startv, Bw. Hussein Bashe alieleza bayana na kwa kujiamini kabisa kwamba mtu anayeamini anaweza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo ni Edward Lowassa. Bashe alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa chama chake kwamba kihakikishe kinazingatia matakwa ya demokrasia wakati wa kumpata mgombea wake wa nafasi ya urais ili apatikane mtu ambaye itakuwa rahisi kwa chama kumnadi mbele ya wananchi. Kwa “wanaosoma katikati ya mistari”, watakubaliana nami kwamba Bashe anaamini kuwa demokrasia ikishika mkondo wake ndani ya chama, basi Edward Lowassa hana mpinzani wa kumzuia kuibuka kidedea. Kwa kawaida, demokrasia inasisitizwa na kuhimizwa na upande wenye imani na wapiga kura wake. Mtu asiyejiamini hawezi kuhimiza demokrasia katika kupata nafasi ya uongozi. Mbinu pekee anayoweza kutumia ni udikteta. Kwa hiyo, nataka nihitimishe mawazo yangu kwamba mazingira yanayomkuta EL yana mfanano wa aina fulani na mazingira aliyopitia Uhuru Kenyatta ingawa siasa za Kenya na sheria zake vinatofautiana kwa kiasi kikubwa na hapa kwetu nchini. Lakini kwa hali iliyotokea Kenya, kamwe tusimbeze EL. Kwa kura za wananchi na haswa katika mazingira tuliyopo hivi sasa, tunaweza kushtukia EL ametua Magogoni kwenye jengo jeupe.

Ndimi Ndashene Mbandu

Huyu jamaa lanchi za wanyama alifanya mali zake! Mroho aliekubuhu!! Naamini hata wafuasi wake ni waroho waliokubuhu!!
 
Siku mheshimiwa Lowassa Alipotangaza kujiuzulu alisema yafuatayo,nitanukuu tu sehemu ya hotuba yake
......."katika kila hoja walizojenga wamesema waziri mkuu ilikuwa hivi. Kulukuwa na shida gani kuja kuniuliza waziri mkuu wanasema ulitoa dekezo hili,ni sawasawa ni kweli. Kulikuwa na shida gani kwa mfano mheshimiwa spika, kufuata utaratibu wa westminster, Kuthibitisha hapa unaposema mwenye Richmond ni flani ukalay on the table records kwamba una ushahidi ni flani.................................nilichofanyiwa mheshimiwa spika napenda kuweka kumbukumbu sahihi sawa,kwamba naona si sahihi, NIMEFADHAIKA SANA, NIMEDHALILISHWA SANA, NIMEONEWA SANA KATIKA HILI. Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijaulizwa. Kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa, tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama...............................................lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni, tunahutubia nchi nzima na kusema waziri mkuu amefanya hiki amefanya hiki amefanya hiki bila kumsikiliza"

Mroho huyu wa mali na madaraka!! hakutoa hitimisho kwa kile alichojua juu ya Richmond!! Siyo Mzalendo na hatakuwa mzalendo kwa sekunde!! Hafai!! na hatufa!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom