Utabiri 2020

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,436
Reaction score
872,033
Ni magoli ya mbali lakini mchoro umeshaanza kuonekana mapema...

Maisha yatakuwa murua sana
Pesa nyingi itaingizwa kwenye mzunguko
Vinywaji vitashushwa bei na kuuzwa kuanzia alfajiri
Kodi nyingi zitapunguzwa na nyingine kufutwa kabisa
Machinga na wafanyabiashara mdogomdogo hawatabughudhiwa kabisa
Vikundi vinavyoanzishwa sasa vya akina mama na vijana vitapata mikopo kwa masharti nafuu na rahisi sana na utakuwa mikopo isiyo na riba
Wasanii watapewa nafuu nyingi kwenye kazi zao.. Hakuna kufungiafungia nyimbo zao au sinema zao
Kumbi za starehe utakuwa mpaka majogoo
Wafungwa wengi wa kisiasa ama wataachiliwa huru, kesi kufutwa na kupata msahama
Miradi mingi mikubwa itazinduliwa na kuorodheshewa mlolongo wa mafanikio.... Kisha tutaenda kupiga kura kwa hiari, kwa ushawishi, kwa nguvu ama vinginevyo......
 
hakika umenena, tutasahau shida kwa muda ili tusaidie kupiga kula (kura). alafu maisha yataendelea kukaza baada ya tukio la kula
 
 
Walimu watalipwa malimbikizo yao
 
Lazima uwe kada au mkereketwa na utakuwa unafuatiliwa bila kujua
Aisee hapo kwenye ukanda wa kijani, siwezi mkuu maana nikijaribu kuwa kada wa lichama hilo naweza kuugua kutokana na roho yao mbaya pamoja na unafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…