Utaanza kumsitiri nani?

teetotaller

JF-Expert Member
Dec 16, 2014
307
204
Habari wanaJF,

Umeoa na unaishi na mkeo mlie jaliwa naye watoto wawili ambaye mmoja yupo nje ya nchi anasoma,katika hali ambayo ni ya kawaida japo ngumu kuizoea unaambiwa mzazi wako wa kike amefariki (mama).

Wakati huo unapewa taarifa hiyo upo mbali na nyumbani kwako (kazini) ukaamua kupiga simu kwa mkeo,mwanao aliyeko nje ya nchi kimasomo, ndugu wengine,jamaa na marafiki, katika hali ya majaribu ya mwenyezi Mungu mwanao kapata ajali ya basi alipokua anakuja kuhudhuria maziko ya bibi yake.

Pia mkeo kapata shambulio la moyo(heart attack) na kumpelekea kupoteza maisha baada ya kupokea taarifa hizo, je kama wewe imekutokea hivi utaanza kumsitiri (kumzika) nani kati ya mama mzazi,mke na mtoto wako?
 
Habari wanaJF!
Umeoa na unaishi na mkeo mlie jaliwa naye watoto wawili ambaye mmoja yupo nje ya nchi anasoma,..katika hali ambayo ni ya kawaida japo ngumu kuizoea unaambiwa Mzazi wako wa kike amefariki(MAMA), wakati huo unapewa taarifa hiyo upo mbali na nyumbani kwako(kazini) ukaamua kupiga simu kwa mkeo,mwanao aliyeko nje ya nchi kimasomo, ndugu wengine,jamaa na marafiki, katika hali ya majaribu ya mwenyezi Mungu mwanao kapata ajali ya basi alipokua anakuja kuhudhuria maziko ya bibi yake,pia mkeo kapata shambulio la moyo(heart attack) na kumpelekea kupoteza maisha baada ya kupokea taarifa hizo......je kama ww imekutokea hivi utaanza kumsitiri (kumzika) nani kati ya Mama mzazi,mke na mtoto wako.????????
Tumsifu yesu kristu, familia au ukoo ndo hupanga mazishi, na Mara nyingi wataanza na yule aliefariki, milele Amina
 
kwakua nivigumu situation kama hii kutokea hili swali sitajibu but wewe wajua mama ni mama
 
Maudhui ya hili swali ni nini labda mkuu?
Au ndo maswali ya kufikrika

Mf.wa maswali haya:
Et ww mtoa posta Leo ukiokota barabarani Mil.200 utazifanyia nn?
 
Back
Top Bottom