Uswahilini Vituko Haviishii

Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,980
3,577
Naandika hili tukio nikiwa nina furaha kwani naskia wimbo wa Raymond - Huku kwetu ukiwa unajirudia rudia ndani ya akili yanguu. " Huku kwetu ukifua viwalo kumbuka kuvilinda ....sijui nini na nini....Nyumba na Gari badooo baadoo....

Nirudi kwenye madaa kulikua kuna shughuli ya ujenzi katika nyumba ya mzee mmoja aliweza kuwapa hiyo kazi vijana 5 pamoja na Fundi mmoja.
Huyu mzee kidogo umri umesogea na hutumia miwani ya macho katika mambo yake. Miwani yake ina frame nzuri sana na ni ya bei ghalii pia, ina mfuko mzuri sana wenye rangi ya gold. Ilipofika jion mzee alikwenda kuwakagua vijana wake, Basi kufika ndani ya nyumba aliweza kuivua miwani aliokua amevaa na kuitia ndani ya kava yake na kisha akaiweka katika dirisha.

Utu uzima una mambo mengi baada ya kumaliza kukagua mafundi aliweza kuondoka bila kukumbuka miwani yake. Usiku ndipo alipokumbuka na kurudi katika ile nyumba lakini hakuikuta alipoiweka.

Jasili haachi asili, na Mwizi ata akistaafu bado ni mwizi tu. Kulipokucha kama kawaida mafundi walikuja kazini na mzee alipo wauliza kama kuna aliechukua mawani yake wote walijibu hapana.

Utu uzima dawa bana. Basi mzee akawambia haina tatizo na akawapiga mkwara kuwa ameshaaongea na shehe ili aweze kumsomea duwa kwa yeyote aliechukua miwani yake hivo amewauliza tu ili yatakayompata aliyechukua miwani yake asijekulaumiwa baada ya hapo mzee akawatakia kazi njema kisha akaondoka zake.

Kusomewa dua sio mchezo ndugu ni hatari! Kumbe kati ya wale mafundi mmoja wao ndio aliiba kufika jion akawaza nitakufaje mie. Basi akatafuta mtoto asiyemtambua yeye na akampa ile miwani ampelekee yule mzee lakini akajitaja kwa jina la mwenzake kua ndio amempa huyo mtoto iyo miwani arudishe.

Narudia tena Utu uzima ni dawa!! Siku iliyofuata mafundi walipokuja mzee akajiuliza haiwezekani huyu alieniibia miwani yangu airudishe alafu amwambie yule mtoto aniambie kuwa nimepewa na fulani nikuletee??? Haiwezekani haiwezekani??

Mzee alimuita yule mtoto na kumuuliza nani kati ya hawa alikupa miwani Jana uniletee?? Chaajabu mtoto alimuonyesha mtu tofauti kabisa ndipo mzee akajizihirishia kumbe huyu alikua anataka kumchafulia jina mwenzake???¿

Jamani utu uzima ni dawa mzee aliamua kumsamehe kisha akawatakia kazi njema kama kawaida kisha akaondoka zake.

Mzee wa watu hakusema chochote kwani angewagombanisha wale mafundi kwa kumpakazia mwenzake ndio alirudisha miwani kumbe sio kweli!!

Nawaza tu ingekuwa ni mtu mwingine nini kingetokea?
Natumai huyu mzee kwa busara zake tutajifunza kitu.
 
Hahahaaaa mkuu kusomewa dua unaweza kupigwa suratul misukosuko au kitanda cha sokwe usiombe kukutwa
 
Back
Top Bottom