"Ususi" wa Kikwete na kamati za Bunge?

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,017
7,220
Baada ya Rais Kikwete "kulisuka" upya baraza la mawaziri, hakuna shaka kuwa kamati za Bunge zitalazimika kujisuka au kusukwa upya. Hii inasababishwa na ukweli kwamba wenyeviti wa kamati kadhaa za Bunge wamekuwa sehemu ya ukili uliotumika kusuka baraza la mawaziri.

Kwa vile kamati ya Bunge inawajibika kudadavua makosa yanayojitokeza ndani ya serikali, ni dhahiri kuwa Waziri au naibu wake wanasongwa na mgongano wa maslahi wanapokuwa wanaongoza kamati za Bunge na wakati huohuo wakiwajibika kuitetea Serikali.

Usiondoke, movie bado inaendelea...
 
sioni kama amelisuka ila ameweka viraka tu!

Shangazi yangu ni msusi wa mikeka. Wakati mwingine akiona kuna kosa katika hatua fulani ya awali, huwa namuona akifumua kile kipande chenye makosa, ukili usiofaa anauweka pembeni na kusuka sehemu ile kwa ukili mwingine. Kusuka siyo lazima ufumue mkeka wote, unaweza kuanzia pale penye matatizo tu.

Hata hivyo, lengo kuu la thread ni kujadili hatma ya kamati za Bunge. Tumeshajadili sana juu ya Baraza jipya na lugha mbalimbali zinazotumika kulitambulisha, lakini tumesahau uhusiano wa Baraza jipya na Bunge.
 
Pamoja na kukarabatiwa kwa kamati za bunge, kiti cha bunge pia kitafanya mabadiliko madogo kwa kumchagua mwenyekiti mwingine kuziba pengo la Mheshimiwa George Simbachamwene alieteuliwa kuwa naibu katika wizara ya ulaji ya nishati na madini.

sisi wadanganyika tupo tayari kushirikiana kikamilifu kwa nguvu zetu zote kufa na kupona na mchwa wapya. ni matumaini yetu labda mnaweza kubadilika mkaacha wizi wa kitoto wa raslimali za nchi yetu.
kumbukeni hata mkilimbikiza kiasi gani mwisho wa siku hamuondoki na kitu na unarudi kuwa udongo wenye rutuba nzuri ambayo haitapatwa zao la maana.
jaribuni basi kuangalia umaskini wetu na sisi tujinyanyue
 
Baada ya Rais Kikwete "kulisuka" upya baraza la mawaziri, hakuna shaka kuwa kamati za Bunge zitalazimika kujisuka au kusukwa upya. Hii inasababishwa na ukweli kwamba wenyeviti wa kamati kadhaa za Bunge wamekuwa sehemu ya ukili uliotumika kusuka baraza la mawaziri.

Kwa vile kamati ya Bunge inawajibika kudadavua makosa yanayojitokeza ndani ya serikali, ni dhahiri kuwa Waziri au naibu wake wanasongwa na mgongano wa maslahi wanapokuwa wanaongoza kamati za Bunge na wakati huohuo wakiwajibika kuitetea Serikali.

Usiondoke, movie bado inaendelea...

Mbatia (kibaraka) atapewa kamati aliyokuwa anaishikilia Januari Makamba... maana wanajua hakuna tofauti kati yake na yeyote anayetoka CCM!!!
 
Back
Top Bottom