Usumbufu na ubabe Chuo Kikuu Mzumbe

Usumbufu na ubabe Chuo Kikuu Mzumbe

hahahah kumbe umejiunga jana usiku
Kujiunga na comment yangu, wapi na wapi! Una matatizo dogo, tumia muda wako kufanya kilichokupeleka. For your information first degree ni muhimu sana katika maisha yako ya baadaye kama ilivyo form four. Ukikalia ati sijui muso nini, hutaweza pata GPA ya 3.8 angalau ujiweke Sawa na yajayo. Fuata maelekezo ya chuo, unavyokurupuka hata hujaona mwaka 2019
 
Kama ufafanuzi uliotolewa wa kulipa angalau 1000 ni kweli hii ni picha halisi ya jinsi tulivyo na watu wazembe, kulalamika kwa ujinga wao uliopitiliza.
Halafu eti serikali ya wanafunzi ipoteze mda kutetea ujinga huu? Hawa warudie tu tutalea ujinga hadi lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila watanzania ni wazembe sana na walalamishi yaani unapewa nafasi zaidi ya mara 3 unakumbushwa kulipa ada hata buku tu ili wakutambue bado hufanyi ivyo ila unapata ujasiri wa kulalamika.
 
B
Habari zenu wakuu,

Naomba nisiwe na maneno mengi sana, mimi ni mwanafunzi hapa Chuo Kikuu Mzumbe mwaka wa pili. Hapa chuoni kuna usumbufu na kero kubwa zinazo endelea dhidi ya wanafunzi, uongozi wa chuo naona umechoka na wanafanya kazi kwa mazoea na ubabe mkubwa. Kwa mfano, sasa hivi wamegoma kufanyia watu usajili na kuwaambia waahirishe mwaka mpaka mwaka ujao kwa madai ya kwamba wamechelewa kufanya usajili.

Wanaelewa kwamba kuna watu wanalipiwa ada na bodi ya mkopo na kuna wanafunzi wanajilipia ada kupitia boom wanazopewa na bodi lakini bado wameshindwa kuelewa na kufungua usajili kwa ambao hawakua wamefanya usajili hapo mwanzo. Sababu za kuahirisha mwaka au mitihani ziko wazi na zinaeleweka vizuri kwamba, mtu ataahirisha mwaka kama atakua na matatizo ya kiafya au ana matatizo ya kifedha.

Ofisi zote wanatoa jibu moja tu rahisi la 'nakushauri ahirisha mwaka', sasa naahirisa vipi mwaka na ada ninayo? pay in slips ninazo mkononi na mtu anakushauri uahirishe mwaka? huu ni utaratibu wa vyuo vyote Tanzania? Waziri wa elimu, na watu watu wenye mamlaka ya kusaidia wanafunzi waendelee na masomo yao naomba mfike hapa chuoni mlitazame hilo. Wanafunzi ambao hwajasajiliwa ni wengi na muda wa kufanya mtihani umekaribia. Rais Magufuli naomba umulike na hapa chuoni .
Bloody bureaucrats who never think outside the box.
 
Back
Top Bottom