Ustaadh alawiti Watano Msikitini!

Ustaadh alawiti Watano Msikitini!

Status
Not open for further replies.

MaxShimba

Platinum Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
36,008
Reaction score
4,093
Na Asha Bani

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemfutia dhamana mwalimu wa madrasa, Mohamed Matimu, anayetuhumiwa kuwalawiti watoto watano.

Mbele ya Hakimu Mkazi Hadija Msongo, Mwendesha Mashitaka Nasoro Siwaya, aliiomba mahakama hiyo kumfutia dhamana mshitakiwa kwa kuwa hayupo tayari kusikiliza ushahidi wa upande wa jamhuri kwa madai ya ugonjwa kila mara.

“Mimi sipo tayari kuendelea kusikiliza ushahidi kwa kuwa naumwa sana,” alidai mtuhumiwa huyo na hata mwendesha mashitaka alipotaka kuona cheti cha daktari, alieleza kuwa anatumia miti shamba.

Aidha, mwendesha mashitaka huyo, alimwomba hakimu awatizame walalamikaji ambao ni watoto walivyoathirika, huku mtuhumiwa akikwepa kusikiliza ushahidi wa makosa yake kwa hofu ya kukutwa na hatia.

Mabishano kati ya mtuhumiwa na mwendesha mashitaka yalichukua dakika 10 kabla ya hakimu kupitia upya masharti ya dhamana na kuifunga kwa maelezo kuwa zipo dalili za mtuhumiwa huyo kuruka dhamana. Ilidaiwa na mwendesha mashitaka kuwa kati ya Aprili 7 na Juni 10, mwaka jana mtuhumiwa huyo aliwalawiti watoto watano wenye miaka kati ya 8 na 16 na kwamba upande wa mashitaka umekamilisha upelelezi.
 
Kaazi kweli kweli. Jamaa anafanya majaribio hapa, kabla ya kwenda ahera. lol
 
Mwacheni ustaadh wa watu afwaidi matunda ya uhuru. Watu hamna dogo.
 
Mwacheni ustaadh wa watu afwaidi matunda ya uhuru. Watu hamna dogo.

ARE YOU SERIOUS? Au ndiyo yale yale ya mwizi kumtetea mwizi mwenzie? God forgive you & everyone else who thinks like you.
 
Siku hizi watu wanao takiwa kuwa watumishi wa Mungu ndiyo wanaongoza kwa dhambi. Anyway Mungu atusaidie.
 
Wewe Doe, acha mchezo, hili si jambo la mzaha. lol

Naona itabidi madrasa zifungwe kufuri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom