Uso kwa uso na mke wa rafiki yangu gesti

Uso kwa uso na mke wa rafiki yangu gesti

Joined
Apr 21, 2015
Posts
11
Reaction score
21
Husika na heading hapo juu,

Wakuu weekend iliyopita nilimuaga mke wangu kuwa nina semina nje ya Dar kikazi maana hiyo ndo huwa mbinu yangu ya kwenda kwenye dhambi zangu kwa siku tatu nne.

Nilikua nime import mchepuko wangu kutoka arusha so nika check in kwenye hotel moja Bagamoyo tukajipumzisha hapo alhamisi,Ijumaa, Jumamosi, jumapili asubuhi tuka check out.

Wakati nafunga mlango wa room nashtuka kumuona mke wa rafiki yangu akitoka chumba mkabala na changu akiongozana na zee moja hivi nao wakifunga chumba chao, shemeji alitetemeka na kupata mshtuko mkubwa hadi yule mzee kumuuliza kuna nini?

Mchepuko wangu ulishatangulia kwenye gari nikamsalimia shemeji nikamwambia mimi ndio na check out nilikua semina ya siku tatu ndo imeisha, akaitikia kwa kichwa tu, nikapiga hatua za haraka kwenda kwenye Gari ili asiuone mchepuko wangu ambao ulishatangulia kwenye gari.

Jumatatu akanipigia simu mwenyewe akaniambia shemeji naomba unifichie siri sitarudia tena. Nikamwambia naomba tuongee baadae kwa sasa nipo busy.

Mchana wake akanitumia meseji inasomeka hivi "" Shem naomba kama vipi tafuta sehemu nije tumalizane kiutu uzima and you stay silence forever "" naomba unijibu i can't afford to loose this marriage

Wakuu nipo njia panda, ingawa mimi ni mzinzi na sina utakatifu lakini siwezi kutembea na mke wa rafiki yangu kipenzi tulieshibana miaka nenda miaka Rudi na nilishawahi kukaa kwake sana wakati sijapata kazi yeye alianza kuja Dar es salaam kabla yangu.

Kwa sasa huyu jamaa yupo mkoani kikazi alihamishiwa huko mke alishindwa kumfuata kwa yeye mwenyewe ana kazi hapa Dar.Jana kanitumia M-PESA laki tano ikisindikizwa na msg kuwa vipi shemeji lile suala letu umeamuaje ukimya wako unaniumiza sikujibu kitu.

Wakuu naomba muongozo wenu. Kweli nisimwambie rafiki yangu kuhusu uzinzi wa mkewe? Na mimi ndio nimepewa jukumu la kumuangalizia familia yake kwa mambo mbali mbali kwa kuwa yupo mbali.

Nawasikiliza wakuu
 
Mudishie pesa yake
mwambie huwezi kutembea nae
na mwambie unamuomba ajirekebishe ikitokea tena unaweza shindwa kukaa nayo moyoni....
but kwa kuwa wote ni watu wazima.....kila mtu atazame yake
 
kimkwanja poa. ila kimapenzi akuache hivhiv!
 
Mudishie pesa yake
mwambie huwezi kutembea nae
na mwambie unamuomba ajirekebishe ikitokea tena unaweza shindwa kukaa nayo moyoni....
but kwa kuwa wote ni watu wazima.....kila mtu atazame yake

umenena vyemaa kaka
 
Mudishie pesa yake
mwambie huwezi kutembea nae
na mwambie unamuomba ajirekebishe ikitokea tena unaweza shindwa kukaa nayo moyoni....
but kwa kuwa wote ni watu wazima.....kila mtu atazame yake

Anitumie mimi nimsaidie kumrudishia. Laki tano sio ndogo ujue.
 
Mudishie pesa yake
mwambie huwezi kutembea nae
na mwambie unamuomba ajirekebishe ikitokea tena unaweza shindwa kukaa nayo moyoni....
but kwa kuwa wote ni watu wazima.....kila mtu atazame yake

Huo ndiyo uungwana.
 
Kidogo tuu niamini ila hako ka'scene ka laki tano ndio kameharibu.
 
jifanye haujaona na wewe ujue hauna tofauti yoyote na yeye halafu unaziba kwa mwenzio kwako pako wazi.
mkeo nae alikua guest vilevile.
 
Kama ambavyo wewe unaona kinyaa na nafsi inakusuta kutembea na mke wa rafiki yako, ona kinyaa na nafsi ikusute hivyo hivyo kumuacha mkeo na kwenda kuzini na mchepuko. Njaa na tamaa za mwili kwa kuzini unadhani kipi cha maana umekipata baada ya kufanya uovu huo?
kwa nini ulioa wakati kumbe bado unataka kula ujana?

Sasa fanya hivi ili iwe dawa na wewe usichepuke tena. Mwambie huyo mke wa rafikio kuwa NA WEWE PALE ULIKUWA NA MCHEPUKE NA ASIMWAMBIE MKEO. Hiyo ndio dawa nzuri ili yeye aache kuchepuka kwa mumewe na wewe uache kuchepuka kwa mkeo. Kisha mrudishie pesa zake na muache umala.y.a wenu. Waoneeni huruma watoto na wake zenu mkifa kwa ukimwi mtawaacha na nani?mnataka wawe chokoraa?

Ukishaoa unatakiwa utulie. Funga zipu yako, wanawake wazuri hawaishi ukimuona mzuri wa makalio(ashakum si mmatusi) leo, kesho utamuona wa nywele, kesho kutwa utamuona mwenye MEWATA nzuri zaidi, mtondogoo utamuona mwenye guuu hasa...sema na moyo wako,sema na njaa zako za mwili.
 
Wewe unatakaje?????? wewe mwenyewe mzinzi alafu unamtishia mwenzio, MWAMBIE yameisha ajirekebishe na wewe jirekebishe, nyie ndio wanaume mnafia gesti mnatupa wakati mgumu wa kulilia maiti, maana mwanake anabaki kulia kwa aibu badala yakulia kwa uchungu. umenikera.
 
Na wewe acha uzinzi ka!unamuaga mke wako kumbe unamchepuko back to your friend's wife mwonye na asirudie tena fuata ushauri wa boss hapo juu
 
Back
Top Bottom