carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 331
- 838
Pretoria, Afrika Kusini. USM Alger ya Algeria imeandika historia nyingine katika soka la Afrika baada ya kuichapa Mamelodi Sundowns mabao 3-1 na kutwaa ubingwa wa taji la CAF Super Cup kwa mara ya pili.
Katika mchezo huo uliopigwa leo Jumapili, Novemba 8, 2026, kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld, Pretoria, Afrika Kusini, USM Alger ilitumia vyema nafasi ilizopata na kuizima Mamelodi Sundowns.
Mabao ya USM Alger yamefungwa na Zakaria Draoui katika dakika ya nne, Saadi Radouani katika dakika ya 37 na Ahmed Khaldi katika dakika ya 55, huku bao pekee la Sundowns likifungwa na Iqraam Rayners kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 25.
Ushindi huo umeiwezesha USM Alger kuongeza taji lingine katika historia yake, baada ya awali kutwaa ubingwa huo mwaka 2023. Pia imejinyakulia kitita cha dola 500,000 (Sh1.3 bilioni).