Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,535
1. Amezaliwa Tarehe 7 Oktoba Pamoja na viongozi mashuhuri Vladmir putin wa Urusi, na Askofu Desmond Tutu.
2. Ni Kiongozi wa Sita mwenye ushawishi zaidi africa, mpaka april 4 2013 alikua na wafuasi 57,626 katika mtandao wa Twitter.
3. Ndiye Kiongozi Aliyechangia Kiasi Kikubwa kupatikana kwa aman katika nchi za Burundi na DRC akiwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania.
4. Kama ilivyo kwa Rais Obama wa Marekani, Raisi Kikwete ni Mchezaji mzuri wa Mpira wa Kikapu. alichezea timu ya shule katika mashindano mbalimbali.
5. Ukiacha mwalimu Nyerere, Raisi Kikwete ndiye kiongozi mwenye Tuzo nyingi zaidi za Heshima. Ameshapata tuzo zaidi Ya Tano za heshima toka aanze muhula wake wa kwanza mwaka 2005.
6.Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga. Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mjamzito naye, Babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.
7.aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.
8.Ni Mmoja Kati Ya Mawaziri wadogo zaidi wa Fedha Kuwahi Kutokea Nchini Tanzania alichaguliwa kuwa waziri wa fedha akiwa na umri wa miaka 44 tu. mwaka 1994
9.Licha ya Kuwa Mkwere, Hawezi kuogelea!
10.Aliwahi kusema “ Roads are the blood vessels of the economy. ” akiwa na maana ya kwamba barabara ndio mishipa ya damu ya uchumi!.. anaamini ukiwa na barabara bora na uchumi wako utakua kwa haraka zaidi!
Cc : Nifah