Usiyofahamu kuhusu Fly Emirates

Hivi mkoa WA Rwanda na Mkoa wa Burundi wanamiliki boing sisi hatuña?,Mungu yupo tutamiliki tu ipo siku
 
Nasikia hilo Pangaboi limenunuliwa kwa bei ya kutupwa kama ilivyokuwa lile boti la Bagamoyo.
 
Wako vizuri lakini wananiudhi tu baadhi ya ndege zao ni kajamba nani yaani kativii kamoja kama kwenye basi mtoe macho mpaka shingo ziume
 
Kumbe Tz tulikuwa na midege mikubwa hapo kabla, nani aliziuza ndege zetu ili tumtegeshe shingo yake kwenye pangaboi zetu mpya zimkate kichwa!!? Inauma sana! Nawachukia sana waliotuhujumu.
 
makao makuu ya hili shirikA yapO wapI?
 
Ila inauma sana.....nchi hii imekuwa shamba la bibi. Tunachagua watu wa kutuongoza ambao ni mufilisi kimawazo. Ngoja tumuache JPM japo afanye mabadiliko. Tulisha miliki ndege sasa ilibaki kuwa kichekesho.
 
Inauma kwakweli kwa hili tumerudi kwenye sifuri. Kuna watu wametusaliti katika hili. Tulisha miliki ndege za maana. Wahuni waliuza wakanywea bia. Tumpe muda JPM angalau naona ana nia nzuri na nchi hii. Ila wajinga wajinga wote wapishe wanaoweza kufanya kazi.
 
Matapanda hiyo hiyo mkitaka ziuzeni .. sijui sasa mtawauzia nani wakati mnaziponda.. ha ha ha
 
Emirates, Qatar, KLM, hutajutia kwa masafa marefu. They're absolutely nice.
 
Ya kwetu



Wenzetu!
Tumechelewa sanaa,tumeharibu mashirika yetu ya uma na kufika tulipofika kwa ufisadi uliolelewa na chama tawala, na leo tumeshindwa kesi na kutakiwa kulipa mabilioni mengi kwa SCBank. Sasa si vibaya kuanzia na tulipoanzia, hata mbuyu ulianza kama mchicha. CAG aongezewe fungu la kutosha ili afanye kazi yake kwa ufanisi hasa kwenye mashirika haya ya uma.Mkuu wa kaya atumbue majipu halisi na si vijipu uchungu, soon tutawapita hata wenzetu.
 
Team mpya. Team TUSIONAJEMA.
 
Ndege sioo biashara ya Mpesa kaka inaitaji kuwa NA reg kuchekiwa NA tcaa NA mengineyoo msihizi mlivyojaza Mpesa kila sehemu sawa NA biashsra ya ndege

Walitangulia Canada kwa shughuli hiyo ndiyo maana in registration tayari. ukaguzi ulifanywa na TCAA na wamesema wazi wazi kuwa iko vizuri sana na tayari kwa shughuli.
Hivi wakianza ukaguzi saa hii wa hiyo panga boy na wakakuta ina hitilafu watairudisha huko walikoinunua? Everything is done just waiting official inauguration to fly!!!!
 
Wako vizuri lakini wananiudhi tu baadhi ya ndege zao ni kajamba nani yaani kativii kamoja kama kwenye basi mtoe macho mpaka shingo ziume

ckipato watu wanatofautiana mkuu hizo kitivii kimoja sawa na pangaboi letu inawezekana ndo ndege yao ya thamani ya chini
 
Ni kawaida masikini kulalamika,haishi kulalamika wala kuridhika..... Ukimpa mia kama una sh elfu moja ataona ni kama umemuonea na una roho mbaya..
Huyo ndo maskini, hana shukraniiii!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…