Siri kubwa ya ushindi ni uvumilivu,kwa viongozi wa siasa uvumilivu huo huitwa stahmala,kwa maisha ya kawaida ni uvumilivu,utulivu na kutopapatika kujibu au kufanya kitu bila tafakiri kubwa.Angalia navyojibu hoja humu,kuna watu wananitukana,sijibu kwa matusi,kuna wanaokejeli,siwajibu kwa kejeli,kuna watu wanatoa kashfa mie najibu kwa staha.Basi tumeumbwa kusaidiana humu duniani hata mimi nilisaidiwa sana tu.Mimi niliwahi kwenda faroe islands na nikaugua ghafla nikiwa supermarket,nilianguka ghafla,pembeni yangu alikuwepo dada mmoja mwafrika akakimbia kunisaidia,kwenye koti nililovaa kulikuwa na pin ya rangi za bendera ya tanzania,akaniuliza hii umepata wapi? maana kwa wajihi wangu huwezi kuamini kuwa mie ni mtanzania maana nimetokea na rangi ya baba yangu.Nikamjibu mimi ni mtanzania.Akanisemesha kiswahili na tukaongea,yeye ndio alisimamia matibabu yangu yote,guess what? huyo dafa anaitwa paulina,mnyakyusa ila kaolewa faroe islands