Usiwe king'ang'anizi...soma alama za nyakati!!

So does not matter how much it pains (time heals) ni bora uondoke mapema na kujijenga mwenyewe.., because you should never depend on someone else for your happiness you must be a King/Queen to your own castle so its true "If he cant learn to love you, you should leave him" sababu life is too short and the time you spend na huzuni with someone can be spent better with someone else who know your value.., and they are a lot people out there who will value you more hata kama hakuna ni bora kukaa peke yako kuliko na mzigo wa matatizo........BY J!!
its a viscous cycle and you may end up recycling your love life because there is no perfect man!

Love is a gamble, only 0.1% WIN IT
 
Kuna wakati unaweza kumkuta mtu yupo kwenye mahusiano yenye kila aina ya karaha na unyanyasaji lakini bado yupo tu na wala hafikirii kuondoka.Unakuta mtu anatukanwa...anapigwa...anadharauliwa...yani kwa ujumla anaonyeshwa kila dalili za kuchokwa ama kutotakwa tena lakini anaamua kufa kibudi.Uvumilivu ni muhimu kwenye mahusiano...ila pia inabidi tujifunze kusoma alama za nyakati.Kuna vitu ambavyo mwenzi wako akianza kuvifanya tena kwa kuvirudia rudia unatakiwa ujue kwamba hapa sitakikani tena na utafute jinsi ya kujitoa.Ndio maana wahenga walisema ''akufukuzae hakwambii ondoka.'' Mara nyingi mtu atakufanyia visa akijua kwamba ukivichoka utaondoka mwenyewe...kumbe kuna wale wenzangu na mie wanaoamini na kujipa moyo wa mabadiliko hata pasipo na moyo...unavumilia manyanyaso ukijua kesho itakua bora ya jana alafu matokeo yake jana inageuka bora ya leo pale unapovunjwa moyo kabisa.

Na hii ni zaidi kwa sisi kina dada!!Jamani embu tujifunze kusema inatosha na tuache kua ving'ang'anizi.Jiamini kwamba ulivyompata huyo ndivyo ambavyo utampata mwingine.Usiishi kwa mateso kwa wasiwasi wa kutokupendwa tena kwasababu hujui kuna kizuri gani kinakusubiria huko nje ila hakiwezi kujitokeza bila wewe kuweka hiyo nafasi wazi!Hamna mtu anaestahili kulala akilia kila siku au kutokua na furaha kwasababu ya binadamu mwenzake.Ukiona mtu hakufai achana nae...usimpe mtu mwingine nafasi ya kucontroll maisha yako ....hiyo ni kazi yako.Ukitaka furaha itafute....ukikereka na kuchoka huzuni ikimbie!!!

Usisubiri kuvunjwa moyo uokote vipande....ondoka na moyo wako mzima ukatafute atakaeupa furaha na amani!!

So does not matter how much it pains (time heals) ni bora uondoke mapema na kujijenga mwenyewe.., because you should never depend on someone else for your happiness you must be a King/Queen to your own castle so its true "If he cant learn to love you, you should leave him" sababu life is too short and the time you spend na huzuni with someone can be spent better with someone else who know your value.., and they are a lot people out there who will value you more hata kama hakuna ni bora kukaa peke yako kuliko na mzigo wa matatizo........BY J!!

nashukuru lizzy imenigusa
 
:smash::smash:
:mad2::mad2:
:rant::rant::rant::rant::rant::rant::rant:

Hubby embu soma katikati ya mistari bwana!!!Ina maana hata washkaji siruhusiwi kuwamiss???WE NDO KILA KITU BANA.....:hug:
 
its a viscous cycle and you may end up recycling your love life because there is no perfect man!

Love is a gamble, only 0.1% WIN IT

Well...perfect man or no perfect man, no one deserves to be treated like SH!T!!
 
Yani kwa jinsi navyosoma wana jf wanavyochangia nahc maumivu ya kuachwa/kuacha moyo jaman moyo unauma sana liz we acha 2.
 
inahitaji ushujaa mkubwa kujitoa kwenye abusive relationship, unyanyasaji unaweza usiwe unausisha kipigo moja kwa moja lakini maneno ya kuumiza na yenye kuondoa confidence na kujisikia huko trapped kwenye relationship, kwa kweli ni suala la kupongeza ukiona mtu amejitoa kwenye uhusiano wa namna hii.
 
Na hiyo psychological abuse ndo haswaa inayowaondolea watu kujiamini!
 
Hebu jamani nielezeni, kama mwanamke anamnyanyasa mwanaume inakuwaje hapo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom