Usiwe kimbilio Mioyo Yao inapokua Broken 💔

Usiwe kimbilio Mioyo Yao inapokua Broken 💔

Bei Rahisi Electronics

Senior Member
Joined
Apr 4, 2025
Posts
197
Reaction score
583
Usiwe kimbilio Mioyo Yao inapokua Broken, Baada ya kuumizwa kutoka kwa ampendaye anakuja kuuguza kidonda kwako ,Kikipona anarudi kwa amtakaye, Hakikisha unakua Mchoyo wa Mda wako Usipatikane kirahisi...
tengeneza Ngome Imara .... anayekushibokea mshobokee

Ishawahi kukutokea Kipindi Unamuhitaji Mtu alikukataa iwe mpenzi, Rafiki au ndugu, Baada ya mda Fulani akarudi? Muweke mbali na moyo wako ujue Hilo ni koti la kuazima litarudi tu kwa mwenyewe,Jiandae Maumivu.

Kosa Kubwa Katika Maisha Kumsamehe msaliti Tena ukamruhusu msaliti awe Katika Cycle Yako utajuta.....

Aina ya watu waliokuzunguka ni matokeo ya unavyojichukulia.

Watu wengi wamealibikiwa maisha kuruhusu watu wasio sahihi kuwa Kalibu ,Mtu Mwenye Mafanikio anawatu wachache waliomzunguka Ambao nipe nikupe na sio nipe nisipe...

Wewe Mfalme Jenga Ngome Yako kumruhusu unayemtaka kwa Manufaa maalumu, Anayekutaka Hakikisha anathamani gani Kwako maana Watu huja na kuondoka baada ya kupata Alichokihitaji.

Taarifa zako zikitoka basi umeziruhusu , Hakikisha Project umemaliza ndo unamwambia Mtu in Process stop telling anyone.

Kujishusha kwa Aliyekuzidi si Ujinga Bali ni Taurati(Mchakato wa mafanikio), Jifunze nawala Usimchukie ,Kumsema kwa Mapungufu yake sio Dalaja la kumshusha zaidi unampandisha.

Huruma si Malezi, Asilimia 60% ya matatizo tuliyonayo yanatoka na tabia Mbaya tulizokuwa nazo ,Hivyo saidia Mtu ndani ya uwezo wako , Mapito ni funzo lake la kumuimarisha ajutiye tabia Mbaya alizo nazo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom