SoC04 Usiulize Taifa limekufanyia nini, uliza umelifanyia Taifa nini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Ghettominds

New Member
May 2, 2024
4
0
Naandika kutokea Ghetto hii ni story ya Ghettominds. Anaesoma hii namuomba samahani kwa kumkumbusha machungu aliyopitia, katika ngazi ya elimu ya juu yani chuo. Hii ngazi wengi humu tumepitia na hakuna asiyejua maisha ya chuo jinsi yalivyo. Hivyo basi kupitia sera ya Tanzania niitakayo nawapa wanajamii DUKA LETU, ni duka litakalo saidia kutatua shida ya njaa kwa wanafunzi wa vyuo. Walengwa wakubwa wa DUKA LETU ni wanafunzi wa elimu ya ngazi ya juu( chuo). Kupitia The Tanzania Commission for University (TCU) wanaeleza kwa mwaka wa masomo 2022/2023 zaidi ya wanafunzi 300,000 walijuunga na elimu ya ngazi ya juu kwa vyuo vikuu ambavyo vipo sio pungufu ya 30 na kukifanya chuo kimoja kuwa na wanafunzi wasiopungua 10,000. Hii ni namba kubwa na nzuri itakayoweza kufanya kuanza kwa safari yetu kuipata Tanzania tunayoitaka kwani ni mtaji tosha kuendesha shughuli zote za DUKA LETU.

Njaa nayoizungumzia hapa ni kushindwa kula milo zaidi ya mmoja kwa siku au kushindwa kupata chakula chenye virutubisha kamili. Aminini vyuoni wapo wanafunzi wanalala na njaa kwa kukosa pesa tuu ya kufanya manunuzi yao ya kila siku kwasababu hudumu za maisha katika jamii zimekuwa kubwa.

DUKA LETU litasimama kama mkono utakao walisha wanafunzi wote wa vyuoni kuanzia litakavyoanzishwa kwenda miaka zaidi ya 25.

CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA VIJANA WA VYUONI KIPINDI WAKIKABIRIANA NA NJAA

Kushindwa kuhudhuria vipindi darasani. Wanafunzi wengi hushindwa kuhudhuria masomo sababu unakuta mtu amekula mara moja ambayo ni mchana wa jana hivyo asubuhi inamuwia ngumu kuamka na kwenda vipindi vya asubuhi sababu ya mwili kukosa nguvu itakayo muwezesha mwanafunzi huyu kwenda na kukaa darasani masaa zaid ya 3.
  • Kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsi. Kwa wanafunzi wa vyuoni wahanga wakubwa kwenye suala hili ni wanawake maana maisha yanavyozidi kuwa magumu hukimbilia kwa wanaume huko hukutana na manyanyaso ya aina mbalimbali na hukubali kuvumilia sasababu uwezo wao wa kiuchumi ni mdogo kukidhi mahitaji yao ya msingi hususani chakula.​
  • Mimba za kutokukusudia. Hii hutokea pale mwanamke hukosa kauli mbele ya mwanaume wake maana yeye ndio mnunuzi wa chakula hivyo akisema leo ni ngono bila kinga inabidi iwe hivyo maana isopokuwa hivyo ndio mwisho wa mahusiano.​
  • Matatizo ya afya ya akili. Nilisoma pahala walitoa hoja kuwa njaa imaweza pelekea matatizo ya afya ya akili. Hii ni pale mtu hutumia mda wake mwingi kuwaza anapata wapi chakula cha kumfanya aione kesho au kuvuta masaa mbele hivyo kuwa na msongo mkubwa wa mawazo kupelekea matatizo ya afya ya akili.​
  • Kudhohorofisha ufaulu kwa mwanafunzi. Lishe bora na kupata chakula kwa mda hufanya akili kuwa nyepesi kwenye kufikiria hivyo basi mtu akikosa chakula chenye lishe bora (mlo timilifu) au kutokula kwa wakati huifanya akili kushindwa kufikiria kwa ufanisi na kumpelekea mwanafunzi kushuka kitaaluma.​
  • Kushindwa kuendelea na masomo. Wanafunzi wengi hushindwa kuendelea na elimu yao ya ngazi za juu kwani wengi hujikita kwenye shughuli zitakazo wafanya wapate pesa ya kujikimu na kuweza kutatua shida zao, njaa ikiwemo. Waathirika wakubwa wa hili jambo ni wavulana maana wao kupata chakula ni kwanjia ya jasho tuu.​
JINSI YA KUPAMBANA NA HIZI CHANGAMOTO

DUKA LETU
litakuwa ni duka litakalokuwa linatoa huduma ya bidhaa za chakula kwa wanafunzi wa vyuoni. Kupitia DUKA LETU wanafunzi wa vyuoni watatumia duka hili kununua bidhaa za kupikia(nafaka) au zilizokuwa tayari kwa matumizi kama vile soda, juice, biscuits, mchele, unga, sukari, mafuta, n.k

WATAKAO NUFAIKA NA DUKA LETU
  • Wanafunzi.​
  • Hawa watakuwa ni wanafaika wa moja kwa moja kwani watatumia DUKA LETU kupata huduma ya bidhaa hizo kwa bei nafuu kulinganisha na maduka mengine.​
  • Pia wanafunzi watatumia DUKA LETU kama fursa ya kuweza kujipatia kipato kwani DUKA LETU litahitaji bidhaa mbalimbali za kuuza.​
  • Serikali.​
  • Kila serikali inajukumu la kuhudumia jamii zake na hivyo ndivyo huonekana kama serikali inajali watu wake, basi kupitia DUKA LETU serikali itakuwa imepata huduma nyingine itakayoweza kusaidi raia wake hususani wanafunzi na hawa ndio kesho ya taifa.​
  • Pia itajipatia mapato maana itakuwa inakusanya ile asilimia ya mapato yatakayo patikana na mauzo ya bidhaa hizo dukani.​
  • Makampuni binafsi na watu binafsi.
  • Kwa upande wa makampuni hawa watanufaika na DUKA LETU kwani watakuwa kama wadau wa maendeleo katika jamii na itawaleta karibu na wanafunzi hawa kwani pia ndio wateja wao wakubwa kwenye bidhaa na shughuli zao.​
MCHANGO WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI
  • Kupitia wizara husika zitumike kutoa elimu na semiza za matumizi ya fedha kwa wanafunzi kwani wengi hawana bajeti inayoeleweka kwenye manunuzi ya bidhaa za chakula.​
  • Serikali kupitia wizara husika, makampuni na watu binafsi kwa kushirikiana watoe msaada kwa DUKA LETU kwa kuwaudhia bidhaa hizi kwa bei nafuu na kwapunguzo la kodi kwani bidhaa hizi zitauzwa dukani humu kwa bei ya kuchangia huduma nasio faida.​
  • Kuwapatia maeneo uongozi utakao simamia DUKA LETU eneo sahihi ya kuanzisha duka hilo karibu na mazingira ya chuo.​
  • Kufuatilia mwenendo mzima wa DUKA LETU na huduma zake kwa wanafunzi hao.​
  • Serikali itengeneze mazingira mazuri na mashirika na makampuni binafsi yatakayojitokeza kutoa msaada kwa wanafunzi hawa kwa kuwatoza kodi ndogo kwenye bidhaa hizo zitazowekwa dukani.​
  • Serikali iwashirikishe wanafunzi kwenye uendeshaji wa DUKA LETU kwani itawapa chachu nawao kuja kuwa watu wa kujitoloea kwani itakuwa ni sehemu ya wao kujifunza elimu jamii na kuweza kuja kuendesha shughuli nyingine za kijamii.​
  • Wahitimu wapatiwe maeneo na serikali waweze kuendelea kuzalisha mazao ya chakula ili kupunguza gharama za manunuzi kwani wao kupitia vikundi vyao watatumika kuuzia DUKA LETU bidhaa hizo.​
USHAURI WANGU KWA JAMII NZIMA

Watanzania ni watu wakarimu sana, na ukarimu wetu ndio hufanya mataifa jarina na yale ya mbali kututolea macho na kutupa sifa hii kwani tunapenda kusaidiana. Kama mtaungana na mimi tunawezapata Tanzania niitakayo kwa zaidi ya miaka 25.

Ni Tanzania ambayo kila mwezi wa 10 unapofika wewe mzazi au mlezi utakuwa na uwakika kuwa mwanao akienda chuo bajeti ya pesa utakayompatia kwaajili ya matumizi ya chukula inakidhi kwa muda wote yupo chuoni. Tukifanya hivi tukakuwa tumejijibu swali letu la nini tumelifanyia taifa na sio kulalamika taifa limetufanyia nini.
 
Unamaanisha kama kila chuo kiwe na MLIMANI CITY MALL YAKE kwa ajili ya wanachuo. Au kama ilivyo kila kambi ya jeshi ina duka/supermarket yake eeeh.

Labda kupunguza usimamizi wa hayo mambo mengi ya DUKA basi vyuo viwe na utaratibu kama wa boarding schools.

Kinakuwepo chakula kwa ajili ya yeyote asiyeweza kumudu chakula.

Tofauti na hivyo basi ni kuhakikisha kila mwanafunzi anapata mikopo ya kujikimu ili ajinunulie chakula popote anapoona panamfaa.
 
Naam huko na mim sawa kiongozi, ila kwny upande wa pale kila mwanafunzi apate mkopo na akijinunulie chakula anapoona panamfaa hii itazidi kuchochea hali hiyohiyo kwani wafanyabiashara watatumia tena hili suala kama fursa na kuongeza gharama ya bidhaa kwani wenyewe wanazana ya kuwa wanafunzi wa chuo wanayo pesa nyingi maana hupokea kutoka bodi na kwa wazazi wao na ndio maana kujipangia bidhaa kwa bei watakayoipanga wao(soko huru). Mfano kuna vyuo havipo mijini au vipo njee ya mji nikichukulia SAUT kama mfano wa moja kwa moja kwani jamii ya wafanyabiashara maeneo hayo ya chuo wanafunzi hawa ndio soko lao kuu hivyo ukisema kila mwanafunzi apate mkopo ilimradi tuu akajinunulie chakula anapoona panamfaa ni kama tumeongezea mafuta maana sio madukani tuu bali hata kwenye migahawa ya chukula nayo bei hupanda. Ndio maana nmeona njia sahihi ni kuwa na hii kitu karibu na chuo kuwasaidia hawa wanafunzi
 
Labda kupunguza usimamizi wa hayo mambo mengi ya DUKA basi vyuo viwe na utaratibu kama wa boarding schools.

Kinakuwepo chakula kwa ajili ya yeyote asiyeweza kumudu chakula.
Hili nalo ni wazo zuri, ila kwa upande wangu naona kama hii itakuwa ni changamoto kwani tumeona serikali ilijaribu na imejaribu kufanya hili kwa ngazi za msingi na sekondari. Shida inayojitokeza ni kuwa jamii ya kitanzania hawaamini sana kwenye misaada ya bure. Mfano tumeona msaada uliotolewa na USAID watanzania walivyopinga vikali na kudai wao wanaweza zalisha hicho chakula nasio kutegemea msaada kutoka nje, pia tuliona mashuleni suala hilohilo lilitokea na ndio maana hadi leo huduma ya chakula cha bure mashuleni inakuwa ngumu
 
Back
Top Bottom