Usiudhuru uumbaji kwakuwa hujui umebeba hatima ya wangapi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,067
Reaction score
871,225
Bila Shaka utakuwa umegundua hii ni mizoga ya makinda ya ndege fulani!

Kwa mtazamo wa kawaida utaungana nami kuwa kifo chao kilitokana na kutokuwepo kwa Mama yao!

Yamkini mama alienda kutafuta chakula na hakurudi tena!

Hata hivyo, maisha yao, makuzi yao, kula na kunywa kwao, hatima yao ilimtegemea Mama yao Sana.!

Yawezakuwa ni Tamaa, ubinafsi, njaa ya mtu au mnyama mwingine iliyo sababisha mama wa makinda haya afe na kuleta kifo cha makinda yake pia!

Sikia nikuambie mpendwa Tamaa yako, jeuri yako, ubinafsi wako, njaa yako isiwe sababu ya kuleta shida kwa wengine.!

KUMBUKA
Huyo umuonaye wa kawaida machoni pako na unaamua kumuwekea kila aina ya vizingiti asifanikiwe labda kwa haraka ni tegemeo na msaada kwa wengine.

Wako wengi nyuma yake ambao maisha yao yanamtegemea huyo.!

Jifunze kutokuamua kwa tamaa, hasira wala jeuri au kwa ubinafsi, fikiria maisha ya wengine na utakuwa heri.

Kuna mtu leo hii ukimungalia unaona kabisa ameangamiza wengi waliokuwa nyuma yake,! dumisha upendo, nia njema na amani, kuchukuliana nawe utaitwa heri na kukumbukwa kwa mema na si mabaya

Tunatanguliza tamaa zetu katika mambo madogo, kuchukia na hata kuwaumiza wengine na kuua bila kujua kuwa wamebeba hatima ya watu wengi![emoji419][emoji375]

Jr[emoji769] future pastor[emoji173]
FB_IMG_1686708224306.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli alipowafukuza kazi watumishi kisa vyeti feki haya ndio yaliyowapata maelfu ya wategemezi wa wafanyakazi wale kumbe busara ingetumika makinda yasingeathirika.
 
Ogopa mtu anaitwa HR hao jamaa labda uwe na Godfathers ndani ya kampuni ndio wanaufyata maana wakifanya tu figusu zao za kijinga za kutaka kukutemesha ndoano Godfathers lazima waje juu kumuuliza kulikoni ?
Kuna kima moja aliitwa Bruno alikuwa HRM WA tanesco mkoa wa Arusha jitu jinga sana lile kumbe ajabu hakuwa na vyeti ancle magu alivyo kuja akamzambaratisha kwa mbali.
 
Kuna kima moja aliitwa Bruno alikuwa HRM WA tanesco mkoa wa Arusha jitu jinga sana lile kumbe ajabu hakuwa na vyeti ancle magu alivyo kuja akamzambaratisha kwa mbali
Ilikua halali yake kufukuzwa na maHRM wengi wenye pigo za ajabu hua mwisho na wao wanafukuzwa pia
 
Bila Shaka utakuwa umegundua hii ni mizoga ya makinda ya ndege fulani!

Kwa mtazamo wa kawaida utaungana nami kuwa kifo chao kilitokana na kutokuwepo kwa Mama yao!

Yamkini mama alienda kutafuta chakula na hakurudi tena!

Hata hivyo, maisha yao, makuzi yao, kula na kunywa kwao, hatima yao ilimtegemea Mama yao Sana.!

Yawezakuwa ni Tamaa, ubinafsi, njaa ya mtu au mnyama mwingine iliyo sababisha mama wa makinda haya afe na kuleta kifo cha makinda yake pia!

Sikia nikuambie mpendwa Tamaa yako, jeuri yako, ubinafsi wako, njaa yako isiwe sababu ya kuleta shida kwa wengine.!

KUMBUKA
Huyo umuonaye wa kawaida machoni pako na unaamua kumuwekea kila aina ya vizingiti asifanikiwe labda kwa haraka ni tegemeo na msaada kwa wengine.

Wako wengi nyuma yake ambao maisha yao yanamtegemea huyo.!

Jifunze kutokuamua kwa tamaa, hasira wala jeuri au kwa ubinafsi, fikiria maisha ya wengine na utakuwa heri.

Kuna mtu leo hii ukimungalia unaona kabisa ameangamiza wengi waliokuwa nyuma yake,! dumisha upendo, nia njema na amani, kuchukuliana nawe utaitwa heri na kukumbukwa kwa mema na si mabaya

Tunatanguliza tamaa zetu katika mambo madogo, kuchukia na hata kuwaumiza wengine na kuua bila kujua kuwa wamebeba hatima ya watu wengi![emoji419][emoji375]

Jr[emoji769] future pastor[emoji173]View attachment 2656642

Sent using Jamii Forums mobile app
Fact bro kuna watu wana disappoint sana kwenye maisha haya

Kuna watu wanatuchukulia simple sanaaa

Kuna watu wanaangalia leo yetu ,nakuitumia kutukandamiza

But ,prayers, hard working ,patience and focus vita waprove wrong

Wanaotudharau siku moja watatuheshimu " tupambane kwa bidiii"
 
Back
Top Bottom