Usitukane Wakunga Wakati Uzazi Ungalipo.

dfreym

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
342
87
Ukipata fedha usidharau watu ukajiona wewe ni bora kuliko wasiokuwa nazo,
Ukipata nafasi ya kusoma na usiwaone wale wasiosoma sio kitu, hata kama ni Wazazi wako,
huwezi kujifanya wewe ndo wewe ukawaambia Wazazi wako hawajaenda shule,
kumbuka walinyima wewe uende shule, unapata Mshahara Unakula wote, kisa mshahara hautoshi,
kwa taarifa yako hata wao ulikuwa haitoshi lakini walijipinda usome unaona Kero ukipewa matatizo ya home itakula kwako, we tukana wakunga kimoyo moyo kuwa "wamezidi".
Ukipata Mchumba au hata Boyfriend ama Girl Friend basi usijione wewe ndo Beautiful kuliko Cleopatra, unawaona wenzio wasiopata watu ni "Magume gume".
Ukiolewa wenzio wakikosa bahati usianze nyodo "Siongei na Wasio na Ndoa",
Ukipata kazi sehemu nyingi bora kuliko hapo ulipo, usiondoke na mbwembwe za matarumbeta, hii dunia bwana huwezi jua.
Dharau haziwezi kutupeleka mahali popote, unayemdharau leo hujui kesho yake itakuaje, hapa ni duniani na malipo ni hapa hapa unachopanda ndicho utakachovuana, mbwembwe na majigambo ni utoto wa hali ya Juu ukikua utaacha, Sasa kwanini kufanya dharau sababu ya mafanikio yasiyodumu??
hukuwahi sikia ama kuona watu waliokuwa na nyodo na mbwembwe wazazi wao wakiwa hai ghafla wazazi wakafaraki??
hukuwahi sikia watu waliokuwa wanafanya mbwembwe na kufuru sababu ya wapenzi wao ghafla kikaumana??
hujawahi sikia mtu aliondoka kwenye ofisi moja kwa mbwembwe huko alikokwenda kikanuka??
yangu mimi ni macho, ninarudia kusema Usitukane Wakunga Wakati Uzazi Ungalipo.

 
Si tu ukiwa na hela, Hata kuwazushia CHADEMA uongo huku wewe maisha yako unategemea siasa ni kutukana wakunga wakati CHADEMA ndo DOLA TARAJIWA 2015
 
Binaadamu huhitaji maeneo ya kujidai na unapopata mafanikio basi ni vizuri usherehekee nayo. Siyo kila anaejifarisha kwa mafanikio kuwa anafanya jambo baya!
 
maneno kuntu...tatizo umeyaleta jukwaa lisiloendana na busara hizo...taomba lianzishwe jukwaa la busara na hekima...big up
 
"Dharau haziwezi kutupeleka mahali popote, unayemdharau leo hujui kesho yake itakuaje, hapa ni duniani na malipo ni hapa hapa unachopanda ndicho utakachovuana, mbwembwe na majigambo ni utoto wa hali ya Juu ukikua utaacha, Sasa kwanini kufanya dharau sababu ya mafanikio yasiyodumu??
hukuwahi sikia ama kuona watu waliokuwa na nyodo na mbwembwe wazazi wao wakiwa hai ghafla wazazi wakafaraki??
hukuwahi sikia watu waliokuwa wanafanya mbwembwe na kufuru sababu ya wapenzi wao ghafla kikaumana??
hujawahi sikia mtu aliondoka kwenye ofisi moja kwa mbwembwe huko alikokwenda kikanuka??
yangu mimi ni macho, ninarudia kusema Usitukane Wakunga Wakati Uzazi Ungalipo"

Maneno kuntu haya jama
 
MankaM ur making me happy,dahhh maneno ya maana sana haya
zamani watu walikuwa wanaandika point sanaa,tunazingua sie wa ckuiz
 
Last edited by a moderator:
Kweli kabisaaaaaaa!!!hilo halina ubishi malipo ni hapa hapa duniani akhera kuhesabiwa tu.
 
MankaM ur making me happy,dahhh maneno ya maana sana haya
zamani watu walikuwa wanaandika point sanaa,tunazingua sie wa ckuiz

nimeona ni peruzi vya miaka ya nyuma jaman kumbe kulikuwa na madini duuuu sijui nilikuwa wapi muda wote huo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom