Usitarajie Raha Katika Ndoa Bila Karaha

Usitarajie Raha Katika Ndoa Bila Karaha

As Salafiyyu91

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2014
Posts
2,537
Reaction score
2,544
1 Usitarajie Kila Kitu Kiwe Shwari Katika NDOA bila Misukosuko.

2 Usitarajie Kushiba,Kuvaa,Kuoga Bila ya Kukosa cha Kutia Kinywani Au Kuvaa Mwilini ni jambo la Kawaida Katika NDOA.

3 Usitarajie Aliyekuoa au Uliyemuoa Awe Mkamilifu Utakavyo Wewe! Bila Shaka Utie Akilini Kwamba Chochote Kizuri kina Ubaya Na Kinyume Chake.

4 Usitarajie Kubembelezwa katika Ndoa Bila maneno Makali Bila Manung'uniko katika Ndoa. Bila Shaka Kuna Kusutwa,Kupigwa,Kufukuzwa na Hata Kuchukiwa.

5 Usitarajie Vyote Katika NDOA Ni vyenye Kukufurahisha kuna Vile Vya Kuhuzunisha Kukutia Majonzi Kukupa Mihangaiko Mfadhaiko na Kukutupa Katika Lindi La Mawazo.

6 Usitarajie Kupata Mzuri Safi,Mwenye Hekima Na Busara Katika Ndoa. Kuna Wenye Hasira Bila Busara Wenye Midomo Mikali Mno Wenye Kupungukiwa Kwa Uwezo WaKutafakari.

7 Ndo Maana NDOA ni Chuo Ni Ibaada Na Kila Ibaada Inataka Uvumilivu Wa Hali Ya Juu Mno.

Sote Tuvumilie Katika NDOA zetu. Mwenyezi Mungu atupe Moyo Wenye Kusubiri.
images(6).jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tegemea maumivu..

#bila bila...Hamna kitu huko ndo maana sipo

you may not start conversation with the following recipient;Tairus
 
Back
Top Bottom