Usipoteze moyo mwema ulionao!

Red Scorpion

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,736
4,252
Bwana mmoja alimuona nyoka akiungua moto kiasi afe, akaamua aokoe maisha yake kwa kumtoa, alipofanya hivyo aling'atwa na yule nyoka na kumuachia maumivu makali yaliyosababisha amuachie na hatimaye yule nyoka kuangukia tena ktk moto.

HATA hivyo yule bwana aliamua kumuokoa tena yule nyoka.
Mtu mmoja shuhuda wa LILE tukio alimsogelea yule bwana na kumuuliza "ya NINI ujisumbue kuokoa maisha ya huyo nyoka aliyehatarisha maisha yako kwa kukung'ata?"
Yule bwana akajibu, *"Nyoka kung'ata ni asili yake, nami kusaidia ni asili yangu"*

wapo watu uliojitoa kwao ili kuwaepusha na hatari..lakini mwisho wa siku..wanakung`ata..na roho inakuuma sana Wapo ambao unahangaika kila siku kuwafanya wasonge mbele, lakini unachoambulia ni kejeli tu.. Hawana shukrani..

Imefika mahali na wewe unataka uwe kama wao vile...

NAKUKUMBUSHA...
Wapo ambao hiyo ndio sifa yao...
Wewe fanya moyo wako ulivyo Usilipe baya kwa baya, usipoteze moyo mwema ulionao badala yake jifunze kuchukua tahadhari.....

Nami nimeanza kuchukua tahadhari
 
Kwa hii dunia , mmmh ni kuiacha kama ilivyo, hata ukiwa na roho nzuri bado wanadamu watakutenda tuuu. Yamenipata mimi siku hizi nawapa wanadamu asilimia 20 tu ya upendo wangu pamoja na tahadhari sanaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom