Baba Vladmir
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 413
- 726
Tuendelee kukumbushana kila wakati juu ya ulaji sahihi kwa ajili ya kutunza miili yetu, japo kuna watu husema tutakufa tu hata tufanye nini lakini ni muhimu kuwa na tahadhari juu ya maisha yako ya kila siku, maana huwezi kujua pengine Mungu anataka uende mpaka miaka 80 na zaidi.
Kuna watu wanafikri na kudhani kuwa wanakula vizuri mno kumbe wanakula vibaya sana na fedha zao ndizo zinawafanya wapate madhara ya baadaye katika afya zao.
Magonjwa kama saratani, shinikizo la damu na mengine yafananayo yanachangiwa pakubwa na matumizi yetu ya kila siku katika kuendenda, kula na kunywa.
Ni vema kutumia chakula kama tiba kwa sasa kuliko baadaye ulishapata shida ukawa unabugia madawa kila saa. Ukitumia chakula, vinywaji na mienendo mizuri ya maisha dawa unaweza kuzisikia tu.
Sisi watu wa tiba mbadala tunashauri kila siku watu wajiepushe na miendendo mibaya kwa kuzingatia ulaji, unywaji na tabia njema kwenye jamii.
Hayo ndiyo mambo yanayoepusha kuzorota kwa afya.Shida kubwa walimwengu wamejaa ubishi na ujuaji mkubwa badala ya kusikiliza na kujifunza.
Baadaye wakiwa na shida ya afya tukiwaambia gharama za kujitibu wanalalama,lakini tukiwafundisha kujikinga napo hawataki....!
Muhimu zaidi tujifunze kumcha Mungu.