Usipochukuwa risiti ya EFD kuadhibiwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kuanza kutumia sheria katika kutoa adhabu kwa wale wote watakaokaidi kutoa au kudai risiti kwa kuwa wamekuwa wakichangia upotevu wa mapato ya Serikali hali inayodidimiza uchumi na kukosa maendeleo ya nchi.

Kamishina Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata ametoa taarifa hiyo, katika mkutano TRA na walipakodi jijini Arusha wakiwemo wafanyabiashara pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali.

"Kuanzia sasa tutatumia sheria zetu kutoa adhabu kali kwa wale wasiotoa risiti ni vizuri tuwe na utamaduni wa kudai risiti kwani endapo utabainika itachukuliwa hatua kali,"amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela akizugumza katika mkutano huo, amewataka wakazi wa Mkoa wa Arusha kushirikiana katika kufichua biashara ya bidhaa bandia ambazo zimekuwa zikichangia kudidimiza uchumi .

"Bado mkoa wetu unatumika kama daraja la bidhaa za kughushi kwa hiyo sisi kama Mkoa wa Arusha tunatakiwa kushirikiana na kuendelea kuhamasisha kuepuka kufanya biashara za bidhaa za kughushi,"amesema.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo Kelvin Remen amesema mkutano huo ni jukwaa muhimu litakalowasaidia wafabishara kulipa kodi kwa njia rafiki bila kuwa na matatizo yeyote kwa wafanyabiashara.

"Hii ni fursa kwa walipakodi kupata nafasi ya kukaa na uongozi wa juu wa TRA ilinkuwaeleza changamoto zetu ili kuweza kufikia malengo yetu na Taifa pasipo kumwumiza mfanyabiashara yeyote,"alisema.

Mwananchi
 
Tanzania ni bidhaa chache sana huwezi pata kwa wamachinga..Sasa sijui watakabilianaje kuhusu hilo
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kuanza kutumia sheria katika kutoa adhabu kwa wale wote watakaokaidi kutoa au kudai risiti kwa kuwa wamekuwa wakichangia upotevu wa mapato ya Serikali hali inayodidimiza uchumi na kukosa maendeleo ya nchi.

.....


Vile vile ni vyema kuwajulisha mnakonunua kua wanaweza wanaweza pia kutumia kompyuta, POS, SIMU na mashine yoyote kutoa risiti halali.

Setup nayopendekeza kama tayari kuna smartphone ni hii... Inaghalimu laki tatu tu na unaweza lipa baada ya kupewa huduma uzurimteja anapata risiti kama aliyozoea na inayotambulika na TRA







SOMA ZAIDI: Simu Janja kama Mashine ya EFD - Nafuu kubwa kwa wajasiliamali na wafanya biashara.
 
Back
Top Bottom