USIPITE HEBU soma HAPA

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
12,716
19,849
Jana 14 june Tukiwa katika mizunguko yetu ya life mi na rafiki yangu ghafla alipokea simu yake iliyokua ikiita na baada kukatika nikaona kama jamaa ghafla katokwa na mood {kapotea kimawazo} nakaanza kumdodosa kwa nini amechange ghafla kidogo agome kunieleza ila baada kushow care akanieleza yafuatayo:
MPENZI WAKE ALIPATWA NA TATIZO LA KIFAMILIA MWAKA JANA na HILO TATIZO LILIPELEKEA MPENZI WAKE KUOKOKA tangu safari yake ya wokovu imeanza kwa huyo mpenzi wake imemsababishia kukonda,anacomplicates life kitu kidogo tu YESU HAPENDI hata kiss imekuwa tabu kupata na mengine kibao hadi kupelekea jamaa yangu akae pembeni kucheki trend ya huyo mpenzi wake.Sasa ile simu aliyotoka kupigiwa ilikuwa ni taarifa kutoka kwa rafiki yake na jamaa yangu huyu ambaye anasoma na huyo msichana chuo kimoja hapa nchini ikimueleza kuwa mpenzi wake hasomi na anafail mitihani sana kutokana na kuwa MUDA wote anautumia kusali na free time yake anaitumia kuhubili Injili chumba hadi chumba kwenye hosteli za pale chuoni anaposoma na anazidi kupungua kwa kukonda kwa ajili ya kuzidisha kufunga(fasting) mara kwa mara.SASA JAMAA YANGU AMEINGIWA NA HURUMA ANAHISI MPENZI WAKE ANACHANGANYIKIWA NA KILA AKIMFUATA KUMUELEZA NDO KABISA JAMAA YANGU ANAONWA KAMA SHETANI ANAMTUMIA JAMAA ILI AMTOE MIKONONI MWA YESU.jamaa yangu hajui pa kuanzia mi nimeshindwa kumshauri nimemsihi ajipe muda aombe ushauri kwa watu mbali mbali ila nimeona bado nina nafasi ya kumshauri jamani mnalionje hili swala?
 
wewe umemshauri nini huyo rafiki yako? awaone wachungaji wake wamshauri pia maana yeye hatamwelewa,pia ikiwezekana naye aokoke halafu ndio aanze kutoa ushauri,vinginevyo itakuwa ngumu Mwambie jamaa ajisogeze madhabahuni mwa Bwana
 
Ndani ya Yesu kuna raha unapotimiza na kufuata sheria na wajibu lakini inapopitiliza inakuwa kero ndio maana maandiko yanasema kila kitu kiwe kwa kiasi,sasa ameokoka huku anafeli masomo huo wokovu gani wakati tuliookoka tunafanywa kuwa vichwa wala sio mkia au yeye anatumia Biblia ipi hiyo?
 
wewe umemshauri nini huyo rafiki yako? awaone wachungaji wake wamshauri pia maana yeye hatamwelewa,pia ikiwezekana naye aokoke halafu ndio aanze kutoa ushauri,vinginevyo itakuwa ngumu Mwambie jamaa ajisogeze madhabahuni mwa Bwana

Nitalifikisha hili
 
maisha bila Yesu si kitu lakini pia maisha bila elimu ni sawa na chai isiyokuwa na sukari. mwambie ajitahidi kumweleza na ikibidi aokoke pia ili waende sawa.
 
cwaamini sana walokole wa stail hii huenda ni mental illness.mwambie jamaa ampeleke kwa psychiatrist kabla mambo hayajaharibika zaid
 
Back
Top Bottom