Usione mwanaume katulia kwenye ndoa ukajua kaendewa kwa mganga,uganga tunao wenyewe wanawake....

Candy kisses

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
296
210
Jana tulikua na kamjadala karefu kidogo kuhusu hawa wandugu kitu gani wanataka ili watulie ndoani. Nami nimeyachuja, nikaongeza na tu chumvi kidogo ili kunogesha. haya si maneno yangu. Ni yakwao wenyewe. Mwenye macho na asome na mwenye kusikia asikilize sauti yake mwenyewe ikisoma....... Usione mwanaume katulia na mkewe ukaanza kuuliza mke kamwendea kwa mganga yupi,uganga tunao wenyewe wanawake shutu kuwajibika;

1. Kumjali mumeo kadri uwezavyo. Usipo mjali wengine wataja saidia kumjali. Mfano …..kuna watu hapa hata hawajui leo mume wake kava nini!! Wengine hata soksi za waume zao haawajui ziko ngapi. Mume anaenda kazini hata hukumbuki kava shati rangi gani. Akipita na kimada mbele yako unaanza kujiuliza, sijui ndo Yule……. Mbona shati ka lake??? Hivi leo alivaa shati ile eh……! Jipange mwanamke

2. Jifunze kuhusu mapenzi na mbinu mpya…. Hii nadhani wanasema ubunifi uwe mara dufu hasa chumbani. Sio mbaya hata mkizungumza na wanawake wenzenu mkapata maujuzi mapya. Style zile apendazo mumeo ndo mwake. Basi hata japo uliza mume wangu vipi hii… nah ii je!! Na Msijisahau, yale masham sham ya uchumba yaendelee mpaka kwenye ndoa.

3. Tuwaelewe waume zetu kutokana na hali zao. Mfano kachoka, anamatatizo. Usiwe wakati wa sisi kuanza lawama. Mume kapata msiba, wewe ndo unapeleka shida zako. Atakuona hovyooo kabisa.

4. Usafi wa nyumba, mwili mzima bila kusahau kinywani. Na uvae vizuri uvutie. Hapa hasa ni usafi na kujipenda. Usione uvivu kujipamba ukiwa kwako na mumeo. Shurti bi mdachi unukie vizuri. Chmba chako sio kinanuka mikojo ya mtoto. Na wanao pia wawe wasafi jamani.Mume anazidi kupata hamasa ya kuwa karibu na familia. Mjitunze vizuri kipindi cha uzazi…. Sio mnanuka maziwaaaa. Yani mazingira yooote yawe ya kushawishi. Nyumbanyingine ukikanyaga tu sakafu, mchaka kama upon je.

5. Jikoni pia uwe mbunifu. Na upate nafasi ya kumpikia mumeo chakula wewe mwenyewe sio kila siku dada wa kazi ndo mpishi. Mume asipate hamu ya kula baa. Kama ni mpenzi wa pombe basi aishie kunywa tu, msosi ataupata kwa mkewe.

6. Kelele majumbani. Hapa wanawake tuache midomo. Kitu kidogo maneno kibao. Kila saa wewe tu ndo unaekerwa. Huishi lawama. Mara nyingine tuchague kukaa kimya, au hata kama tunasema basi kwa sauti ya chini. Si vizuri kumpandishia mumeo sauti hata kama kakosea sema nae tara tara. Na tone zetu ziwe zile za mahaba. Sio umekaza sauti ka unaamrisha gwaride mweh!!!

7. Mnapokosa mkubali makosa na muombe msamaha. Wanaume wanapendaga kuonekana wao ndo kichwa na wanaheshika. Sio unarekebishwa tabia na mumeo, unaishia kununa siku tatu ndani hapaeleweki. Umenunaaaaa hatari.

8. Msijibweteke. Maisha ya sasa ni kusaidiana. So jishughulishe mtoto wa kike. Ukiwa na kakitega uchumi kako si mbaya. Hata mume anakuheshim.

9. Mnapokuwa na watoto mjitahidi kugawa muda kwa ajili ya mtoto na kwa ajili ya mumeo pia. Na msiwe wavivu kutoa unyumba kisa una watoto

kama kunanililo sahau ongezea.......
 
Ni kweli japo la kujiuliza ni

Mmmmmmh! Hayo yote uliyotaja ni ALLERGY kwa small house, na bado wanaenda!!!!!!!!! na ndo ushangae wewe wampikia na katu hawahi kurudi nyumba ndogo amtajia oroza ya bar mpya za kutembelewa ila saa kumi kesharipoti!

SOME TIMES BEING A WIFE IS NOT ENOUGH TO KEEP A MAN!

Ujue mke kujitia kucover nafasi ya MAMUSHKA a.k.a Maza Mzazi na kusahau HAVING SOME FUN part ndo mwanzo wa matatizo mengi! Mumeo kufika tu wamdaka na topic ya ada za watoto, au site. Akija kwangu mie small house na mwambia unajenga nini, hizi nyumba za mjini akae nani? Raha jipe mwenyewe!

FACT IS MAISHA YA NYUMBA NDOGO NI NIGHT MARE KWA WANAUME WENGI! But they keep going n going! Maybe when life is too good at one side of the world, life ceases to be fun and war becomes entertaining! I always ask them why? (honestly not because i care abt the wife but just out of curiousty) They are always like WE DONT KNOW WHY!!!!!!!!!! Psheeeeeeeeeeeeew!

You should not listen to me, because i have come to terms that I may never marry anyone! No man is good enoughf for me! Labda hio ndio fate yangu kusleep arround thats why i see things from my own perspective.
 
kwenye point namba mbili, unamaanisha kwamba mmoja kati ya wanandoa awe mtazamaji mzuri wa picha za ngono ama vipi? huo uzoefu ama ubunifu atautolea wapi?.. dont you see that this is encouraging small houses?
 
Umeongea vema sana lakini yoote hayo yanakuwa hayana maana kama mwanamke hutosimama na Mungu katika ndoa yako!! Wanawake wengi sana wamejikuta katika wakati mgumu kwenye ndoa zao, wamefanya kila kitu kum-please mume lakini waapi, kila siku wanalia. Kuweni wacha Mungu nae atazipigania ndoa zenu
 
Hapo kwenye chakula ni tatizo kubwa. Madam anapaswa kujua hasa kama chakula kimepikwa vizuri ama, hamna kitu nakichukia kama kurudia home jioni nimechoka halafu nikute chakula cha hovyo au hakijaiva vizuri. I really hate that
 
kila siku mijadala ya kijinga kama hii ya kazi gani?

nyumba ndogo ina umuhimu wake na kidumu kina umuhimu wake pia kwenye kujenga amani ndani ya ndoa.

hii mjidala ya kudekeza wanaume imepitwa na wakati, namuonea huruma mwanake yeyote atakayefuta hayo yaliyotajwa hapo juu. Itakula kwake.
 
Hapo kwenye chakula ni tatizo kubwa. Madam anapaswa kujua hasa kama chakula kimepikwa vizuri ama, hamna kitu nakichukia kama kurudia home jioni nimechoka halafu nikute chakula cha hovyo au hakijaiva vizuri. I really hate that

si ukale kwa mama ntilie, kwani umelazimishwa?
 
Ni kweli japo la kujiuliza ni

Mmmmmmh! Hayo yote uliyotaja ni ALLERGY kwa small house, na bado wanaenda!!!!!!!!! na ndo ushangae wewe wampikia na katu hawahi kurudi nyumba ndogo amtajia oroza ya bar mpya za kutembelewa ila saa kumi kesharipoti!

SOME TIMES BEING A WIFE IS NOT ENOUGH TO KEEP A MAN!

Ujue mke kujitia kucover nafasi ya MAMUSHKA a.k.a Maza Mzazi na kusahau HAVING SOME FUN part ndo mwanzo wa matatizo mengi! Mumeo kufika tu wamdaka na topic ya ada za watoto, au site. Akija kwangu mie small house na mwambia unajenga nini, hizi nyumba za mjini akae nani? Raha jipe mwenyewe!

FACT IS MAISHA YA NYUMBA NDOGO NI NIGHT MARE KWA WANAUME WENGI! But they keep going n going! Maybe when life is too good at one side of the world, life ceases to be fun and war becomes entertaining! I always ask them why? (honestly not because i care abt the wife but just out of curiousty) They are always like WE DONT KNOW WHY!!!!!!!!!! Psheeeeeeeeeeeeew!

You should not listen to me, because i have come to terms that I may never marry anyone! No man is good enoughf for me! Labda hio ndio fate yangu kusleep arround thats why i see things from my own perspective.

Hivi nini maana ya to KEEP A MAN?

Hili neno hwa silielewagi kabisa, halafu huwa nalisikia sana.

eti to keep a man, how?
 
mama candy uko wapi mama! mbona una akiri nyingi namna hii. mm nimeo hakika natamani nifute mke mwingine,huyu niliye naye ana sifa zote negative.
 
Hii ni hoja ya nguvu,..wenye macho wameona_wenye masikio wamesikia....mimi naendelea kutekeleza yanipasayo hapa home.
 
Umeongea vema sana lakini yoote hayo yanakuwa hayana maana kama mwanamke hutosimama na Mungu katika ndoa yako!! Wanawake wengi sana wamejikuta katika wakati mgumu kwenye ndoa zao, wamefanya kila kitu kum-please mume lakini waapi, kila siku wanalia. Kuweni wacha Mungu nae atazipigania ndoa zenu

Hakika.
 
Jamani mbona hamniiti?

Heheheeee.....
Mwanamke kila Siku kiguu na njia hata cream haikai mwilini atakubeba nani!!!
Hebu ninyamaze mie.
Hainihusu.
 
Umeongea vema sana lakini yoote hayo yanakuwa hayana maana kama mwanamke hutosimama na Mungu katika ndoa yako!! Wanawake wengi sana wamejikuta katika wakati mgumu kwenye ndoa zao, wamefanya kila kitu kum-please mume lakini waapi, kila siku wanalia. Kuweni wacha Mungu nae atazipigania ndoa zenu

kweli kabisa mana bwana asipoulinda mji wakeshao wanafanya kazi bure...
 
Umenena vema Candy kisses! pamoja na hayo tusisahau tumeumbwa kila mmoja kwa jinsi yake, tabia zake kutokana na mazingira/malezi. Jitahidi sana kupata mtu wa jinsi yako (ubavu wako wa kufanana naye) yaani mtakayeendana na kuvumiliana tabia na hali zenu. Lakini ukabeba jitu tu kwa tamaa zako ambalo huendani nalo hata uwe na msaafu wa mambo yanayopasa kumfanyia mwanamume haitasaidia kitu kwako itakuwa ni mzigo, malalamiko na machungu tu milele na milele!
 
Last edited by a moderator:
No.1 nimeipesha shost......
Ndio maana mwafulani habanduki kwangu....kwa mkewe kapaona kama mji wa utalii....aenda kwa msimu.
 
Back
Top Bottom