Usiombe yakukute jamani, daah!!!

Pole sana rafiki, hapo sasa ndo panaitwa Golgota ya Tanga!!
 
Mtu ana watoto wawili analazimisha awe mkeo? Huyu anaujasiri namna hii ni hatari kwa afya yako na familia yako kwa njia yoyote ile hata ndumba.
 
Huu ushauri,una mantiki sana nimeukubali Brother Great CHUKUA HUU USHAURI
 
Umeongea ukweli mtupu!!!
 
Hiyo picha imenikata stimu halafu na wewe mtoa mada ni mtu wa ovyo sana ungekuwa ndugu yangu ningesikitika sana ila ingawa sikujui bado nasikitika sana akili yako ni ya kijinga mnoo kwa Maisha unayoishi na ujinga unaofanyiwa na hao wanawake wote wawili.
 
Mkuu naomba utupe angalau mbinu usisahau
Tujinasue maana wengine tumecheza hattrik zote lakin wapi
 
Daaa pole sana mkuu
 
The greatman ktk ubora wako, kwanza una miaka mingapi? Kifua huna pia wanawake wanakuzidi akili
Mkuu yakikufika utaelewa,lakini kwa sasa ni rahisi sana kuniona dhaifu,japo awali nilikuwa naamini haiwezi kufikia hatua kama hii,kwani niliamini huyu wa ofisini lazima atakuwa na woga wa kibinadamu kwa kujua kwamba mimi na yeye tynaiba tu,lakini kumbe sivyo hata kidogo!!!
 
Mkuu mpaka kufika hatua ya kuleta Uzi hapa,ni kwamba yamenifika shingoni,kwa uzembe au ujinga wangu,inanigharimu sasa,ninachokitafuta zaidi ni namna ya kutoka hapa nilipo kurejea maisha yangu ya kawaida!

Najua nilipotoka kumdhania huyu co-worker kuwa atakuwa na hofu na kuficha mahusiano yetu,kumbe sivyo kabisa!!!
 
Bro
Brother binafsi nimejifunza kitu kutoka kwako ni bora ukawa na mtu mmoja tu tena ambaye una malengo nae hata ikitokea mimba basi najua nitakwenda kumuoa
Kabisaaa,ni hatari sana kuingia kwenye mahusiano na mtu (hasa mfanyakazi mwenzako) huku ukiwa na mahusiano mengine,itakutesa sanaaa!!!
 
Hapo hauna ujanja maana umeshachanganya nao damu inabidi upambane na matokeo yatakayotokea mbele yako. Umefanya kosa sana kumzalisha huyo demu wa kwanza watoto wawili bila kumuoa na huyo wa pili umeenda pekupeku tena bila kumchunguza kama alishazaa watoto huko alikotoka.

Ndio maana nashindwa kukuelewa wewe ni mtu wa aina gani mpk umefanya yote hayo bila kujua kuwa unaharibu Maisha yako. Hapo kwa lolote unalolifanya hiyo misala itasafiri na ww
 
Kabisaaa,ni hatari sana kuingia kwenye mahusiano na mtu (hasa mfanyakazi mwenzako) huku ukiwa na mahusiano mengine,itakutesa sanaaa!!!
Kweli pole,Kaka Omba Msamaa kwa Mungu na Fanya jitihada za kumtuliza huyo wa Tanga atulie,baadae Fanya njia za kuama kama inawezekana Mrudie yule wa Singida japo haumkubali na Fanya jitihada za kumshirikisha Mungu kwa Wakati huu Mgumu,mpe Mungu nafasi ataufanya Mzigo huu kuwa Mwepesi kwako,Fanya hivyo Brother hamna jambo linalomshinda Mungu na usijione Mkosaji sana Mbele za Mungu,Bali Wanadamu tuna Mapungufu sana wala mtu asikuhukumu kwa haya kuwa na Amani Moyoni na Mkabidhi Mungu hili jambo Mungu atafanya njia pasipokuwa na njia tafanya maji mahali palipo na Mwamba na kuwa mtulivu kwa sasa
 
Ahsante sana!!!
 
Siku utajikuta amekuua na kukuzika kimya kimya.
Ndo malipo yake lakini..
Mkeo ni mpole kwa Hiyo ukachukulia upole wake kumuumiza.
na bado kidogo tu utaumbuka
 
Siku utajikuta amekuua na kukuzika kimya kimya.
Ndo malipo yake lakini..
Mkeo ni mpole kwa Hiyo ukachukulia upole wake kumuumiza.
na bado kidogo tu utaumbuka
Wengi mnanituhumu kwa sababu nimekuwa mkweli,lakini si ajabu hata wewe umeshateleza mara nyingi tu,ila hayajakukuta,linapokuja swala la mapenzi watu tunafanya mambo ya ajabu sana,lakini kwa kuwa ni siri basi tunaziacha mioyoni mwetu,wachache tunaojitokeza na kusema yanayotusibu tunashambuliwa sana kana kwamba washambuliaji wote ni innocent kumbe na wao wana ya kwao ila hawayasemi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…