Umasikini wa Nini? Wa sperm, wa upendo, wa uvumilivu, wa nguvu za kiume, wa kipato au wa Nini?
Umasikini wa kipato Ni rahisi Sana kuushinda hasa mkiwa mwapendana kwa dhati.
Vichwa viwili vitafanya Mambo makubwa.
Lakini mumeo akiwa ni tajiri wa mali na ni masikini wa upendo, utajuta kuzaliwa. Utanyanyaswa wewe, utadharaulika wewe, utatukanwa wewe na wazazi wako, Tena atakwambia kabisa hapa umefuata mali tu wewe.
Ushauri wangu ni huu. Kama unataka kuoa, muombe Mungu akupatie mwenzi wa kufanana naye, mwenye upendo na atakayeweza kukuvumilia katika yote.
Mkweli asiye mnafiki, mzandiki Wala mtu wa shirki