USINGIZI UNAWEZA KUUA NGUVU ZA KIUME

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Ni habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Nipashe Jumapili, Oktoba 23, 2016.

Pamoja na faida kadhaa za usingizi kiafya, tabia ya kulala muda mfupi (kujinyima usingizi) au kulala kupita kiasi, ni hatari kwa afya ya uzazi kwa wanaume kwa sababu inaweza kuwasababishia matatizo ya kushindwa kuwapa ujauzito wenzi wao.

Mtafiti wa hii hali, Prof Wise, L. wa Chuo Kikuu cha Boston Marekani, aligundua kwamba katika jozi 790 za wapendanao, kulala chini ya saa 6 au zaidi ya saa 9 (kiwango cha kati kikiwa saa 8) 42% ya hizo jozi uwezo wao kupeana mimba ulipungua. Jozi hizo zilithibitisha kwamba jitihada za kupeana mimba ziligonga mwamba.

Ushauri wangu kwa vijana wa enzi hizi za "digital" mpunguze muda wa kukaa kwenye mitandao ya kijamii ili mpate usingizi wa kutosha (saa 7 au 8) usiku. Wengi wenu wana ma'group' zaidi ya 5 kwenye "whatsapp" mbali na mitandao mingine ya kijamii. Na wengi hulala usingizi alfajiri.

KUPANGA NI KUCHAGUA WAKATI NDIO HUU
 
Back
Top Bottom