Usindikaji wa mvinyo au (WINE).

Nov 19, 2012
14
0
Habari zenu waheshimiwa,poleni sana na majukumu kidunia na kitaifa ndugu zangu mimi ni mjasiriamali mdogo hapa tanzania niko katika harakati za kujikwamua katika maisha hivyo nimeanzisha kamladi kangu kakutengeneza mvinyo wa zabibu au (RED WINE) hivyo naombeni msaada wa kimawazo na maelekezo jinsi gani ntapata vifaa vya kuwekea yani Chupa yani (empty bottle) pamoja na vifaa vyaku bania chupa sehemu ya mfuniko(vifuniko vya WINE) hivi vitu ningependa mtu anisaidie kwa hapa tanzania vinapatikana wapi pia kwa bei gani naweza kuvipata?naombeni msaada kwa hilo wana JF wenzangu ntashkuru sana.
 

Mshind

Member
Jul 10, 2012
55
70
Nenda kioo ltd chang'ombe industrial area, jam jar botles wanauza kwanzia carton50, chupa yako yoyote unayo taka kutengenezewa wanaanza na idadi ya chupa zisizo pungua million mbili malipo advance robotatu ya garama kisha badae unamalizia, mifuniko utapata SIDO nyerere road. kazi kwako!
 
Nov 19, 2012
14
0
MSHIND:mkuu mbona hawa KIOO LIMITED kwasasa naskia wao awatengenezi chupa za mtu yeyote zaidi ya TBL tu.yani TBL wamewachukua kwa kazi zao tu.labda naomba unifungue kwa hilo pia tofauti na KIOO LTD akuna sehemu nyingine?
 

bluetooth

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
4,279
2,000
I smell success here

ukijipanga unatoka .... nakushauri utumie muda muafaka kupata mashine za kupack .... China is the best

kila la heri
 

Mzee Mukaruka

JF-Expert Member
Jun 18, 2012
717
500
Pita SIDO Makao Makuu na pia nenda TBS hawa wapo kwa ajili yetu sisi walipa kodi. Watakuelekeza vizuri sana kwani wana deal na wajasiriamali kila siku. Nakushauri pia ujikite sana kwenye kufanya utafiti kwa macho, uone ili ujue unataka kutoka vipi! Sawa? Endelea na utatoka tu.
 

tz1

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
2,126
2,000
Sido utapata kila.kitu mpaka mashine ya kuingizia cork pamoja na karatasi la juu ya chupa.
 
Nov 19, 2012
14
0
Hichi ndio kinacho nifanya nijivunie kuwa mtanzania kwa ukarimu mlio nionesha na msaada wenu dhahili shahili kuwa ninyi ni watanzania harisi nashkuru sana nashkuru ndugu zangu kwa muongozo wenu ngoja niyafanyie kazi mawazo yenu na ushauli.
 

Evarm

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
1,680
2,000
Hichi ndio kinacho nifanya nijivunie kuwa mtanzania kwa ukarimu mlio nionesha na msaada wenu dhahili shahili kuwa ninyi ni watanzania harisi nashkuru sana nashkuru ndugu zangu kwa muongozo wenu ngoja niyafanyie kazi mawazo yenu na ushauli.
Asante kwa kushukuru
 
Top Bottom