Usimwamini sana mwanamke

zegamba180

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
818
536
Haya nayotaka kuwashirikisha wadau humu ndani, yamemkuta rafiki yangu wa karibu kabisa. Wanajua wapo watakaokwazika ila ukweli lazima usemwe tu, hakuna njia nyingine.

Rafiki yangu alitokea kumpenda sana msichana mmoja waliishi jiran. Binti alikuwa anaishi kwa mjomba wake. Binti akazidi kumchota jamaa, kwa penzi fake. Binti akamuomba jamaa pesa amtumie mama ake kijijini ya kulimia. Jamaa kwa sifa akatuma mpaka ya kupalilia. Binti akachonga na mama ake kuwa amshukuru jamaa.

Baada ya miezi 2 binti akamuomba jamaa aende kijijini kwao akamsalimie mama ake mzazi na kuangalia maendeleo ya kilimo. Huku Dar anaishi kwa mjomba ake. Jamaa akamuandalia zawadi nying zake na za mama ake(mkwe).

Siku anayoondoka binti analia machozi kisa atammiss jamaa kwani kamzoea na anampenda sana. Binti alipofika kijijin kwao simu kabadili number jamaa hana, hakuna mawasiliano.

Jamaa kapeleleza kaambiwa binti amechumbiwa tayari. Jamaa kwenda alichoambulia ni shukrani toka kwa mama kwa ufadhili.
 
Dah kama mshikaji wako alikula mzigo haina kwere kwani wamemalizana tayari. Lakini kama alikuwa anaremba imekula kwake
 
Sasa hapo ushauri wako unahusikaje kuhusu kutowaamini wanawake? Lazima nimpende na kumwamini mke wangu, huo ni wajibu wangu.
 
Ama kweli wanawake we runs yo world, mkiamka mna sisi mkilala mnasisi.
Kiufupi ni kwambaaaaa anayeaminika ni Mungu tu, kila binadamu kimeo tu.
 
Last edited:
mmmmh ujinga wake tu na utoto mwingi kwani mwanamke ni yy pekee hapa duniani??? hata nyie hua mnakosea sana tusiwaamini pia?? mweeeeh kila mtu aish na mwenzie kwa akili yake si ya kushikiwa.
 
Mmmmmh sio wanawake wote wenye hzo tabia, wapo wastarabu na hao wasio na uelpewa. Lkn asikate tamaa malipo ni hapa hapa dunian
 
Imekula kwake kivyake huyo mi ntamuamini tu maana hakuna namna nyingine usipomuamini utaishi kwa mashaka na presha juu
 
Haya nayotaka kuwashirikisha wadau humu ndani, yamemkuta rafiki yangu wa karibu kabisa. Wanajua wapo watakaokwazika ila ukweli lazima usemwe tu, hakuna njia nyingine.

Rafiki yangu alitokea kumpenda sana msichana mmoja waliishi jiran. Binti alikuwa anaishi kwa mjomba wake. Binti akazidi kumchota jamaa, kwa penzi fake. Binti akamuomba jamaa pesa amtumie mama ake kijijini ya kulimia. Jamaa kwa sifa akatuma mpaka ya kupalilia. Binti akachonga na mama ake kuwa amshukuru jamaa.

Baada ya miezi 2 binti akamuomba jamaa aende kijijini kwao akamsalimie mama ake mzazi na kuangalia maendeleo ya kilimo. Huku Dar anaishi kwa mjomba ake. Jamaa akamuandalia zawadi nying zake na za mama ake(mkwe).

Siku anayoondoka binti analia machozi kisa atammiss jamaa kwani kamzoea na anampenda sana. Binti alipofika kijijin kwao simu kabadili number jamaa hana, hakuna mawasiliano.

Jamaa kapeleleza kaambiwa binti amechumbiwa tayari. Jamaa kwenda alichoambulia ni shukrani toka kwa mama kwa ufadhili.
Mapenzi munayaaanza karibuni eeeh? watu wameachwa na kutemwa na kugharamia zaidi ya million 50 sembuse buku 5 hata kama ni yako kula jiwe tu,ndio uanaume huo somooo'
 
Back
Top Bottom