hakuna ila akiniruka ntamwachia, itabid nijilaum mwenyewe kwa upumbavu niliofanya
Pole sana mkuu,
kama hakuna hata mkataba au papers za kuonesha ushiriki wako wakununua hiyo gari basi kuna nafasi kubwa sana ya kutapeliwa mazima na huyo rafiki yako. Kuepuka kutapeliwa fanya hivi kama utaweza,
Kwanza, endelea kuwasiliana na rafiki yako kuhusu kuliuza gari jitahidi usioneshe emotions zozote, hii itampa kuamini hujui kitu. Pia wasiliana tena na yule aliyewauzia gari umwambie akae kimya asimwambie rafiki yako chochote kama wewe unajua gari inapiga kazi. Hii itasadia jamaa atakuwa kwenye zone ya kurelax na itakusaidia wewe kupata muda zaidi kutuliza akili, kupanga mashambulizi ukiwa unaelewa mchezo unaenda vipi
Pili, wakati unaendelea kuwasiliana na huyo rafiki tapeli, Omba likizo kazini au tafuta namna yoyote upate angalau wiki tu uchomoke kazini. Ukiweza kuchomoka kazini hata kwa wiki tafuta dereva anayeweza kuendesha iyo gari ongozana naye nenda mkoa gari lipo ulitafute kimya kimya bila rafiki yako kujua, ukifanikiwa kulipata gari hapo unabidi uwe mkuda kidogo weka sura ya kazi toa maelezo kuwa wewe pamoja na rafiki yako ni wahusika wa hiyo gari hivyo unalitaji uondoke nalo kwa muda huo, au utajua wewe nini cha kuongea hapo lakin hakikisha gari unaondoka nalo na dereva wako.
Tatu, ukiweza kuondoka na gari ukiwa na dereva wako nenda nalo mpaka mkoa uapopiga kazi sasa hapo utaamua wewe ukalifiche sehemu alafu ndio umchane rafiki yako kuhusu madudu yake. Ama unaweza kuamua kuwa na roho mbaya gari ipige kazi na pesa unachukua wewe tu, ama unaweza kuliuza wewe sasa alafu rafiki yako unampa pesa yake kistaarabu na wewe unachukua chako.
ZINGATIA.
hii utafanya yote ikiwa kama utaweza kumuaminisha rafiki yako kuwa ujui kitu na kuendelea kumuonesha trust kwa anachokwambia yeye.
sometimes you have to play a role of a fool to fool the fool who thinks is fooling you.