Usimwamini mtu yeyote, pia nahitaji ushauri

nimejua leo ndo nimeshugulikia ruhusa niende mkuu

12m? Unacheza na maisha aisee, kwa watu tulivyo hustle na ya maisha? Huwa atucheki kabisa na pesa.

Mkopo wa 12m kwa mfanya kazi aisee ni mateso sana kurudisha, wacha masihara na pesa dogo.

Nenda na usicheke na Kima, kama unayosema ni kweli ujue jamaa kajiandaa na vita kali sana, na ashajua tabia yako ya upole.
 
Mimi kwa sasa nafanya biashara, biashara yangu nitakuja mshirikisha mke wangu na watoto wangu tu. Nimeombwa saana kuingia ubia na watu ila nimegoma kufanya hilo kosa.
Usijaribu kuingia ubia na watu.

Watu ni washenzi sana kwenye hii Dunia.
 
kwel8 mkuu, ujue unaweza kufanya maamuz magum ukaharibu kabisa, nimewaza mengi sana
Na ukitaka kweli upate haki yako kwenye hiyo gari ni lazima ujivike ujasiri ambao utatafsiriwa kama roho mbaya, vinginevyo inakula kwako.

Ni lazima umfumbie macho ,masikio yazibe na utu wako ufunike
 
12m? Unacheza na maisha aisee, kwa watu tulivyo hustle na ya maisha? Huwa atucheki kabisa na pesa.

Mkopo wa 12m kwa mfanya kazi aisee ni mateso sana kurudisha, wacha masihara na pesa dogo.

Nenda na usicheke na Kima, kama unayosema ni kweli ujue jamaa kajiandaa na vita kali sana, na ashajua tabia yako ya upole.
nakuelewa mkuu
 
Naitwa x,natokea mkoa x, kwanza kabla ya yoye nipende kuishukuru jamii forum, kiukweli mimi binafsi imenisaidia sana kupitia kuomba ushauri mbalimbali,

Najua kunabaadhi ya watu watanitukana kutokana na hiki kisa changu,kutukana ni ruksa kwani mimi pia baada ya kuamka kwenye usingizi mzito nimejitukana sana,nakiri kufanya kosa kubwa la kumuamini mtu wa karibu.

Lakini pia najua kuna watu huwa sio wabinafsi japo hatujuani ila utaona wanapoteza mda wao kukushauri vizuri,kama huwa mnajiuliza mbinguni ataenda nani, mimi hua nawaza ni watu wa aina hiyo,lakini motoni ni hao watukanaji.

Sasa ndugu zangu mimi ni mtumishi wa halmashaur ya wilaya flani, japo ajira yangu ni ya mkataba,Kutokana na mshahara usiokizi mahitaji,Tukakubaliana na jamaa yangu ambaye tulikua tunaelewana na kuaminiana sana.

Nilijidanganya kumjua tabia jamaa kwamba hangenizuru kumbe binadam sivyo umuonavyo kwa nje binadam yupo ndani ya huu mwili unaouona,kazi zetu ni za site hivyo huwa tukienda tunakaa wiki moja halafu wanakuja wengine sisi tunarudi hom.

Kulingana na tupo pamoja mda mrefu niligundua jamaa hana tamaa ya fedha ana utu,maana ilikua unaweza kuondoka ukarudi hata kesho yake,lakini jamaa atakwambia ulivoondoka ilitokea dili hii na hii na hela zako hizi hapa anakukabidhi fresh tu.hivyo jilimuamini sana.

Pia kulingana na ubinadamu niliowahi kumfanyia sikuamini kama kuna siku angenigeuka, maana alishawahi kuumwa korona nusu kufa, alikua hoi watu wakawa wanamuogopa lakin nilimnyanyua na kumpeleka hospitali na mambo mengi tu ya kibinadamu ambayo nilimfanyia ikiwemo kutatua shida mbalimbali za kifedha alizokuwa akipata.

Sasa rafiki angu huyu ambae alinizidi umri na mambo mengi ya kazini na mambo tu ya kimaisha alionekana anauelewa mpana sana, hivyo nilimuweka kama mtu wa kunishauri mambo mbalimbali.

Tuendelee sasa baada ya kuona hatuwezi kutoboa kwa mshahara ilibidi tuingie mikopo tukachanga milioni kumi na mbili kila mmoja tukanunua gari ya kazi ambayo ni mitsubishi fusso, tulinunua 24milion.maisha yakaanza kuwa magum sababu asilimia kubwa ya mshahara ulirudi kwenye marejesho.

Sasa mistake niliofanya ni kwamba siku ambayo tunanunua aliandika jina lake nikashtuka ila nikaona nitulie tutaweka sawa pindi tutakapokuwa tunabadirisha jina maana jina lilikua bado linasoma la yule alietuuzia.

Haikupita hata wiki moja toka tumenunua ile gari nikapata barua ya kuhamishwa kikazi hivyo nikahamia mkoa mwingine, hio ndo ikawa another big mistake, sababu nikawa mbali na gari yaani nikawa sipewi taarifa nini kinaendelea mpaka niulize, na ikitokea kanipigia yeye ni matatizo tu,mara imeharibika ipo gereji, mara imekamatwa na trafik imepigwa faini,yaani ilifika kipindi yeye ndo yupo na gari ila akawa ananiomba hela mimi ya matatizo ya gari.

Hiyo gari tulinunua mwaka juzi, kila ukimwambia akutumie hela inayopatikana, ni matatizo matupu atakwambia hiki,mara kile,ushirikiano wa mwanzo ukapotea kabisa.

Mimi kuona hivo nikamwambia basi sababu haitulipi tutafute mteja tuuze ili irudi tu hela yetu,akakubari tuiuze, nikamwambia tutafute mteja, akanambia kuna mteja alishakua anamsumbua ila anataka kutoa mil 18,mi nikasema sawa japokua bei ya hasara, nikaona bora nipate hela yoyote kuliko kutopata kitu kabisa,

Ikapita kama siku mbili akanipigia cm akasema, jamaa amekubari kutoa hela ila anataka aende nayo gari mkoa flani kuna milima mikali, apime kama gari itaweza kupanda na mzigo,nikamwambia asifanye hivo tumalizane kwanza maana ikipata matatizo atasema tupunguze bei tena sababu kagundua mbovu kitu ambacho anaweza akawa kasababisha kwa uzembe.akaniambia alikua ananipa taarifa tu ila kashampa, roho iliniuma sana nikawa sina jinsi.

Kama nilivyotabiri ikapita kama siku mbili nikampigia nikamuuliza jamaa kashafika, akaniambia, hajafika kuna kijiji flani kafika gari ikakatika chesesi, hivyo ilibidi aite gari nyingine afaulishe mzigo, nikapanic kidogo nikamwambia si nilikwambia itakavyokua, yeye akasema nisiwe na wasiwas, hawez kwenda kinyume na makubaliano, kama kaharibu ni yeye sisi haituhusu lazima atupe hela yetu ipo palepale, kwahiyo akasema jamaa ataporud kutoka shamba alikokwenda na mzigo baada ya kukodi gari nyingine ndo atakuja kumalizana na sisi.

Baada ya kama wiki hivi, akanambia jamaa karudi mafundi wamemwambia itabidi abadilishe cheses nzima ambapo used milioni saba, ila mpya hajauliza bei ila ni zaidi ya milioni kumi, nikamwambia si unaona sasa mi nilikwambia itakua ngum kutupa hela yetu,akasema kweli inabidi tuwe na ubinadam, maana kapata matatizo, tusubir ashughulikie gari ipone ndo atulipe.

Alivosema hivo tu ndo akili ikarudi fasta kutoka gizani, nikasema huyu jamaa kwann anakaa upande wa alienunua gari, wakati hizo hela tukilipwa ni zetu wote, kuna namna hapa sio bure, nishapigwa hapa, nikahisi mapigo ya moyo yanaenda mbio,kijasho chembamba kinanitoka,roho ikawa inaniuma sana.

Sasa nikaacha kuwasiliana nae nikaona ntamropokea kwa ukali bure vitu ambavyo vipo moyoni nikaaribu mambo kabisa akazidi kujipanga zaidi,maana nna hasira sana mpaka mda huu.

Leo sasa ndo nikapata akili ya kumpigia yule alotuuzia maana namba nnayo,na sijui kwann nilikua simpigii nimuulize au nimuombe ushauri maana yeye ndo ananijua vizuri maana tulionana siku ile tulioenda kununu, ndo akanambia kwanini nilikua simpigii siku zote angeniambia, gari ipo kijiji flani na inapiga kazi vizuri tu, jamaa hajamuuzia mtu amenidanganya.kwakweli toka asubuhi mida ya saa tano hivi hadi saivi nimechanganyikiwa cjui cha kufanya ndo maana nimekimbilia huku naombeni mnishauri, navukaje hapa jamani, cjui cha kufanya,yaani sielewi,ntashukuru sana kwa ushauri wenu, nia yangu nirudishiwe tu hata hela ambayo nilichangia basi nimuachie gari,
HIZI PESA SIJUI ZIMEWEKWA KITU GANI AU ZIMESOMEWA MANENO GANI?

MACHO KWENYE FEDHA.
 
Kuna watu ni wabinafsi na Wana roho mbaya mnoo pole sana chakukushauli mfate jamaa mkae chini muongee muulize yeye anataka nini kwenye uo muungano wenu haswa
 
mtumie message mwambie ulipo umepata mtaalam mmoja matata sana weekend utaenda kuonana nae ili mteja apatikane chap na yeyote anaye ifunga hiyo gari mtaalamu atamuharibu akili yake mara moja..
mkuu Tanzania ina matapeli lakini wapumbavu, unaweza ukawa umeandika hili kwa utani ila nakwambia njii hii inaweza msaidia
 
Hilo la ubia halijawahi nikuta na sitoruhusu, ila nina experience ya washakaji walilima pamoja, Siku wamepatana kesho wanaenda kuvuna, Asubuhi anafika anakuta mabua, kumbe mwenzake Alituma team usiku,
La kumkopesha mtu ndio nina experience nalo.
 
Naitwa x,natokea mkoa x, kwanza kabla ya yoye nipende kuishukuru jamii forum, kiukweli mimi binafsi imenisaidia sana kupitia kuomba ushauri mbalimbali,

Najua kunabaadhi ya watu watanitukana kutokana na hiki kisa changu,kutukana ni ruksa kwani mimi pia baada ya kuamka kwenye usingizi mzito nimejitukana sana,nakiri kufanya kosa kubwa la kumuamini mtu wa karibu.

Lakini pia najua kuna watu huwa sio wabinafsi japo hatujuani ila utaona wanapoteza mda wao kukushauri vizuri,kama huwa mnajiuliza mbinguni ataenda nani, mimi hua nawaza ni watu wa aina hiyo,lakini motoni ni hao watukanaji.

Sasa ndugu zangu mimi ni mtumishi wa halmashaur ya wilaya flani, japo ajira yangu ni ya mkataba,Kutokana na mshahara usiokizi mahitaji,Tukakubaliana na jamaa yangu ambaye tulikua tunaelewana na kuaminiana sana.

Nilijidanganya kumjua tabia jamaa kwamba hangenizuru kumbe binadam sivyo umuonavyo kwa nje binadam yupo ndani ya huu mwili unaouona,kazi zetu ni za site hivyo huwa tukienda tunakaa wiki moja halafu wanakuja wengine sisi tunarudi hom.

Kulingana na tupo pamoja mda mrefu niligundua jamaa hana tamaa ya fedha ana utu,maana ilikua unaweza kuondoka ukarudi hata kesho yake,lakini jamaa atakwambia ulivoondoka ilitokea dili hii na hii na hela zako hizi hapa anakukabidhi fresh tu.hivyo jilimuamini sana.

Pia kulingana na ubinadamu niliowahi kumfanyia sikuamini kama kuna siku angenigeuka, maana alishawahi kuumwa korona nusu kufa, alikua hoi watu wakawa wanamuogopa lakin nilimnyanyua na kumpeleka hospitali na mambo mengi tu ya kibinadamu ambayo nilimfanyia ikiwemo kutatua shida mbalimbali za kifedha alizokuwa akipata.

Sasa rafiki angu huyu ambae alinizidi umri na mambo mengi ya kazini na mambo tu ya kimaisha alionekana anauelewa mpana sana, hivyo nilimuweka kama mtu wa kunishauri mambo mbalimbali.

Tuendelee sasa baada ya kuona hatuwezi kutoboa kwa mshahara ilibidi tuingie mikopo tukachanga milioni kumi na mbili kila mmoja tukanunua gari ya kazi ambayo ni mitsubishi fusso, tulinunua 24milion.maisha yakaanza kuwa magum sababu asilimia kubwa ya mshahara ulirudi kwenye marejesho.

Sasa mistake niliofanya ni kwamba siku ambayo tunanunua aliandika jina lake nikashtuka ila nikaona nitulie tutaweka sawa pindi tutakapokuwa tunabadirisha jina maana jina lilikua bado linasoma la yule alietuuzia.

Haikupita hata wiki moja toka tumenunua ile gari nikapata barua ya kuhamishwa kikazi hivyo nikahamia mkoa mwingine, hio ndo ikawa another big mistake, sababu nikawa mbali na gari yaani nikawa sipewi taarifa nini kinaendelea mpaka niulize, na ikitokea kanipigia yeye ni matatizo tu,mara imeharibika ipo gereji, mara imekamatwa na trafik imepigwa faini,yaani ilifika kipindi yeye ndo yupo na gari ila akawa ananiomba hela mimi ya matatizo ya gari.

Hiyo gari tulinunua mwaka juzi, kila ukimwambia akutumie hela inayopatikana, ni matatizo matupu atakwambia hiki,mara kile,ushirikiano wa mwanzo ukapotea kabisa.

Mimi kuona hivo nikamwambia basi sababu haitulipi tutafute mteja tuuze ili irudi tu hela yetu,akakubari tuiuze, nikamwambia tutafute mteja, akanambia kuna mteja alishakua anamsumbua ila anataka kutoa mil 18,mi nikasema sawa japokua bei ya hasara, nikaona bora nipate hela yoyote kuliko kutopata kitu kabisa,

Ikapita kama siku mbili akanipigia cm akasema, jamaa amekubari kutoa hela ila anataka aende nayo gari mkoa flani kuna milima mikali, apime kama gari itaweza kupanda na mzigo,nikamwambia asifanye hivo tumalizane kwanza maana ikipata matatizo atasema tupunguze bei tena sababu kagundua mbovu kitu ambacho anaweza akawa kasababisha kwa uzembe.akaniambia alikua ananipa taarifa tu ila kashampa, roho iliniuma sana nikawa sina jinsi.

Kama nilivyotabiri ikapita kama siku mbili nikampigia nikamuuliza jamaa kashafika, akaniambia, hajafika kuna kijiji flani kafika gari ikakatika chesesi, hivyo ilibidi aite gari nyingine afaulishe mzigo, nikapanic kidogo nikamwambia si nilikwambia itakavyokua, yeye akasema nisiwe na wasiwas, hawez kwenda kinyume na makubaliano, kama kaharibu ni yeye sisi haituhusu lazima atupe hela yetu ipo palepale, kwahiyo akasema jamaa ataporud kutoka shamba alikokwenda na mzigo baada ya kukodi gari nyingine ndo atakuja kumalizana na sisi.

Baada ya kama wiki hivi, akanambia jamaa karudi mafundi wamemwambia itabidi abadilishe cheses nzima ambapo used milioni saba, ila mpya hajauliza bei ila ni zaidi ya milioni kumi, nikamwambia si unaona sasa mi nilikwambia itakua ngum kutupa hela yetu,akasema kweli inabidi tuwe na ubinadam, maana kapata matatizo, tusubir ashughulikie gari ipone ndo atulipe.

Alivosema hivo tu ndo akili ikarudi fasta kutoka gizani, nikasema huyu jamaa kwann anakaa upande wa alienunua gari, wakati hizo hela tukilipwa ni zetu wote, kuna namna hapa sio bure, nishapigwa hapa, nikahisi mapigo ya moyo yanaenda mbio,kijasho chembamba kinanitoka,roho ikawa inaniuma sana.

Sasa nikaacha kuwasiliana nae nikaona ntamropokea kwa ukali bure vitu ambavyo vipo moyoni nikaaribu mambo kabisa akazidi kujipanga zaidi,maana nna hasira sana mpaka mda huu.

Leo sasa ndo nikapata akili ya kumpigia yule alotuuzia maana namba nnayo,na sijui kwann nilikua simpigii nimuulize au nimuombe ushauri maana yeye ndo ananijua vizuri maana tulionana siku ile tulioenda kununu, ndo akanambia kwanini nilikua simpigii siku zote angeniambia, gari ipo kijiji flani na inapiga kazi vizuri tu, jamaa hajamuuzia mtu amenidanganya.kwakweli toka asubuhi mida ya saa tano hivi hadi saivi nimechanganyikiwa cjui cha kufanya ndo maana nimekimbilia huku naombeni mnishauri, navukaje hapa jamani, cjui cha kufanya,yaani sielewi,ntashukuru sana kwa ushauri wenu, nia yangu nirudishiwe tu hata hela ambayo nilichangia basi nimuachie gari,
Pole sana na yaliyokukuta. Kabla ya yote, jiweke karibu na Mungu, upige sala za kutosha, maana hiyo ni vita.

Halafu fanya yafwatayo:

1. Kusanya taarifa za kutosha za wapi gari ipo na inafanya kazi

2. Ongea na huyo jamaa aliyewauzia hiyo gari, umuombe awe tayari kwenda kutoa ushahidi kwenye mkono wa sheria. Kama kuna documents zozote za kuthibitisha uwepo wako kwenye manunuzi, ziandae. Inaweza kuwa deposit slip, na document za mkopo ambazo tarehe zake zitafanana na documents zake za kuchukua mkopo.

3. Omba likizo bila malipo, nenda mkoa husika, fungua jalada polisi, omba RB.

4. Ukishapata RB yako, nenda huko ambako hiyo gari ipo, kwa ushirikiano na polisi, kamata hiyp gari ipelekwe polisi.

5. Shauri liende mahakamani, then pambana mpaka upate haki yako. Jamaa akiona anashindwa atakuomba mmalizane nnje ya mahakama, usikubali. Omba mahakama gari iuzwe mgawane kitakachopatikana.

Mengine watajazia wadau wengine. Kila la kheri.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
asante sana
 
Anza kuyajenga na aliye wauzia...

Fatilia upate uhakika wa alichosema jamaa na ulichoambiwa..

Nenda polisi gari iletwe kituoni izuiwe..

Kisha mtafute jamaa.. kistaarabu tuuongee nae ... mkiwa kituo cha polisi au kama kuna watu wa karibu watumie hao!
 
Mimi nipo tofauti kidogo kwenye business zangu nikifanya ubia au deal na mtu huwa Sina tamaa kwenye mgao..

Ujanja ujanja udhulumati utapeli uongo na uzandiki sio powaa

So kwenye Hilo inategemea na mtu kwanini? Watu hawapo real kwenye SoMo la sales & marketing nililo jifunza mtaa pesa ya marketing and sales ukilipwa fasta ingiza kwenye account ya ofisi usikae nayo mfukoni au kwenda nayo home..

Stand as a man mchane waziwazi na akikataa acha nae MAANA

Hasara roho pesa makaratasi..

karma is bitch

Tujifunze kua genuine & Real
karma is real
 
Back
Top Bottom