Usimuudhi Mke wako ana Siri kubwa sana

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
2,809
2,000


WANAUME KUNA VITU LAZIMA TUVIELEWE KWA WANAWAKE.

Biblia inasema:
MWANAMKE NI KIUMBE DHAIFU

Hapo hapo inasema;
TUKAE NAO KWA AKILI.

Na bado inasema;
MWANAMKE NI JESHI KUBWA

Swali?
Walijifunza saa ngapi uwanajeshi na ili kudhibitisha kwamba ni Mwanajeshi Mungu anamtuma kwa Mwanamme akamlinde.

Yeremia 31:22 ....
Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya Duniani; Mwanamke atamlinda Mwanamume.

KUMBUKA HILI MWANAUME MWENZANGU.

●Mtu wa Kwanza kukutana na SHETANI live ni Mwanamke pamoja na kwamba walizungumza mengi na kula tunda kiukweli hatujui mengine waliozungumza mbali na kula tunda.

●MWANAMKE aliumbwa ukiwa usingizini wewe MWANAUME hujui ni kitu gani walichozungumza na Mungu kabla ya wewe kuzinduka.

●MWANAMKE ndiye aliyemwelewa Mungu alipoambiwa ana mimba ya Roho Mtakatifu wewe MWANAUME ulitaka kumkimbia badala ya kukabiliana na changamoto hiyo.

●MWANAMKE ndiye Mtu wa kwanza kwenda kuhakikisha kama kweli Yesu amefufuka na kusambaza habari.

●MWANAMKE ndiye anayeongoza kwa ushawishi mkubwa, Mwanaume huna ujanja mfano.
■Eva kwa Adamu
■Delila kwa Samson
■Ester kwa Ahasuero
■Raheli kwa Labani n.k

Usimuudhi Mke wako ana Siri kubwa sana usione kakaa na wewe anakuvumilia pamoja na ukatili wako.

Anaweza akatekeleza walichozungumza na Mungu au anaweza kutekeleza pia alichozungumza na shetani

Oohoo!
Tafakari Ndugu yangu ngoja na mimi niendelee Kutafakari....

 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,710
2,000
Naona leo nyuzi za kujadili wanawake zimekua mfululizo kana kwamba sio siku kuu...😂😂
 

tracebongo

JF-Expert Member
Nov 18, 2018
1,690
2,000
Toka nje ya box mkuu, wanaume tuna siri nyingi zaidi za wake zetu. Usifungwe na vifungu vichache vinavyozungumzia nguvu za mwanamke ukaacha vifungu lukuki vinavyozungumzia nguvu ya mwanaume.
 

skillers

Member
Dec 18, 2020
59
125
Sasa siri ya mtu na kumuudhi vinahusiana nini?

Kwamba tukiwaudhi ndo watatoa hizo siri?

Na vipi kuhusu samson, alimuudhi nini delila mpaka akavujisha siri yake kwa wafilisti wenzie?
 

kibabu cha jadi

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
2,362
2,000
ungemalizia na "merry xmass mwanamke" kabisa maana nahisi ata hii sikukuu watakua wanaifaidi wanawake tu
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
8,324
2,000
Hapo kwenye kuvumilia ukatili wako ni kwa sababu wanaamini utakufa mapema tu kabla yake, hasira hukaa kifuani mwa mtu mpumbavu... hivyo atakuhesabia tu udondoke.
 

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
6,972
2,000
Kiafya unashauriwa siku moja moja mchukize mke wako uone akiropoka maneno hayo unayoita siri..

Nishawahi jaribu nikaambiwa "hafu siku hizi ukinikiss sekunde mbili unataka kuingiza hauna romance.."
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom