Usimtoe mpumbavu katika upumbavu wake

Hekima ni Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2015
Posts
457
Reaction score
792
Kuna watu ni wapumbavu hawafundishiki yaani kujaribu kuwafundisha ni sawa na kuzungumza na upepo.

Mpumbavu anaweza akajua njia sahihi ya kufanya jambo fulani lakini yeye akafanya kwa kuongozwa na hisia zake .

Mpumbavu hushikilia alicho kiamini kwa akili zake .

Bila kuwa na evidence kutoka kwenye chanzo cha hekima chochote.

Ndiyo maana nika andika nukuu inayo sema

Ni rahisi kumtoa ng'ombe aliye nasa kwenye matope kuliko kumtoa mpumbavu katika upumbavu wake

Usisahau ku download Quotes hiyo mpendwa all the best.
 

Attachments

  • 1792221478977.jpg
    142.4 KB · Views: 7
Kweli.. Elimu ni mfumo uliokusudiwa kunyanyua wajinga

Lakini mtu mpumbavu Wacha akafie mbele
 
Tofaut ya mpumbavu na mjinga ni nn?
Ujinga (ignorance) ni kutojua kitu sababu ya kukosa elimu yake au kutofundishwa au kujulishwa kuhusu hicho kitu. Ukikijua unakuwa siyo mjinga tena wa hicho kitu.

Upumbavu (foolishness) ni kutojua kitu lakini ukifundishwa au ukijulishwa bado unapinga au kama kibaya bado unakifanya makusudi ukijifanya mjuaji.
Kufanya kitu unachojua kibaya au haujui ila umeambiwa kabla hicho hakifai huo ni upumbavu. Kubisha usichojua huo upumbavu.

Kizungu:
Fool = mpumbavu
Mjinga = ignorant
Mjinga siyo tatizo bali mpumbavu.
 
nadhani hata kujaribu tu kumfundisha mpumbavu nadhani ni upumbavu tu gentleman, ila kua mchoyo wa maarifa au ujuzi kwa wengine ni upumbavu zaidi 🐒
 
utamjuaje mpumbavu bila kumfundisha?
Gentleman,
mpumbavu ana akili vizuri tu, ila kwa makusudi hupuuza mambo kama hayo ya kufundishwa. Na kwahiyo, uking'ang'ana kumfundisha that means mpumbavu anakua wewe sasa.

Mpumbavu ana ujuzi na daima ana asili ya ujeuri tu wa makusudi, tofauti na mjinga ambae hajui kitu na yuko tayari kufundishwa na kuelewa asilolijua na likambadilisha.


mfano mzuri ni vijana wapumbavu ambao ni graduates kabisa, lakini kwa makusudi wanakubali kutapeliwa Q-NET daily. Utamfundisha nini sasa graduates mpaka akakubali mafundisho yako zaidi ya kukupuuza tu kukuona wewe mfundishaji kua mpumbavu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…