Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 10,651
- 22,817
Simp ni aina ya mwanaume asiyejiweza mbele ya wanawake na ambaye yupo tayari kujitoa kifedha,muda,na jitihada bila mipaka ili tu kumfurahisha mwanamke bila mrejesho wowote kutoka kwa huyo mwanamke akiwa na matumaini ya kupewa attention kama shukurani.
Mahusiano haya yanaweza kuwa kiuchumba,na hata yakifikia eneo la ndoa bado mwanaume anakuwa anatumika na mahusiano hudumu kwa huruma ya mwanamke sio upendo au commitment ya pande zote.
It’s not about generosity, it’s about over-giving to the wrong woman for the wrong reasons.
M’simp wengi hawakuzaliwa masimp bali hutengenezwa na mazingira especially wazazi na walezi wanaowakuza na idea za kisimp na pia vitu wanavyoona katika jamii kama ifuatavyo;
-Ulimwengu wa burudani na overdose ya mahaba ya kiume: katika filamu,music video,hadithi idea ya mapenzi imelenga katika mwanaume kumtafuta, kumtaka, kumonyesha, kumbembeleza na kumshawishi mwanamke kwa nguvu nyingi. Utaona kwenye stories mwanaume anatakiwa kumganda mwanamke na kukataliwa mara kadhaa ndio ampate,au kumpeleka restaurant ya bei sana ili kumuimpress, au kuvua koti na kumtandikia kwenye matope avuke, au kuacha kazi ili kwenda kumkumbatia mke anaejisikia upweke.
-Low self-esteem. Kwa Kiswahili hii kutojikubali wewe na swaga zako hadi kuwepo na mtu mwingine katika maisha yako ili akuhalalishie kuwa wewe upo fresh. Vijana wengi wanaamini wanatakiwa kukimbiza mapenzi na sio kuingia kwenye mapenzi na mwanamke. Kitendo cha mwanamke anapotongozwa kwa mara ya kwanza akaonyesha hana interest inatakiwa kuwa mwisho wa kuapproach na sio sababu ya kuongeza bidii ya kubembeleza kukubaliwa. Kwanini umfosi mtu ambaye tayari ameonyesha hayupo tayari kukukubali kuwa na wewe,muache aende zake.
-Kukosekana kwa role-model wa kiume. Vijana wengi wa sasa wanakulia katika mazingira ya kukosa wanaume mfano wa kuwafundisha misingi ya kiume na kuishiakufuata kila wanachokiona zikiwemo filamu za kisasa ambazo wanaume huonyeshwa kwa wasifu au character dhaifu mbele ya mwanamke. Wanafundishwa kuwa wao ni second class baada ya wanawake.
-Social media validation. Vijana wengi utawakuta mitandaoni wakilike picha za wadada wanaojipost utupu na mitego,hii tabia ikiendelea vijana huhamisha hiyo culture ya kupenda kutafuta attention na kufollow wanawake katika maisha ya kawaida mtaani. Chunguza wewe account yako umefollow watu wa namna gani na je mnamahusiano yapi na hao watu. Kama unafollow wadada wengi pisikali na kazi yako ni kulike picha zao na kuwasalimia inbox ukisema “hello” then jua umeanza au umeshakuwa simp na umeshajiambukiza hili tatizo.
-Internet imechangia sana kukuza masimp : Online simping ni nafuu na haina gharama kama simping ya ground. Katika simping ya macho kwa macho mwanaume lazima utumike ili kuweza kupewa attention na mwanamke unaye simp kwake.
Internet imekuza masimp kupitia website za ngono kama Pornhub,XXNX,Blaizers,Xhamsters etc, mahusiano ya kimtandao (parasocial relationship) hii utaona mtu anamfuatilia mfano Sanchoka na kucomment akitaka Sanchoka amuone na pengine kuvutiwa nae na amtafute wawe wapenzi kwa bahati, na pia “white-knighting” ambapo unakuta kijana anajitoa ufahamu kuingilia na kumtetea mwanamke ambaye hata hamjui akitumainia kuonekana na kumuimpress huyo mwanamke kimapenzi kama shujaa wake.
Masimp wengi hunyonywa na kutumika kwa namna nyingi sana na wanawake kiasi kwamba kuwalezea ni kusema ni sawa na ATM zinazotembea kwaajiri ya wanawake wasio na account za bank,na ego booster kwa wanawake wenye tatizo la tabia la Narcissism.
Mbinu zinazotumika na wanawake kuwanyonya na kuwaweka simps kwenye control yao zinahusisha matendo yafuatayo:
-Mbinu ya chenga za mkate (bread crumbing technique): katika hii mbinu mwanamke huwa nafanya kitu ambacho kwake ni kidogo sana ukilinganisha na anachotegemea toka kwa mwanaume simp anae mrubuni. Mfano anaweza jibu sms kwa alama ya kopa na simp akajiona ameanza kufanikiwa kisha simp akajikuta anamtumia huyu mwanamke laki mbili ili kumshika zaidi kumbe anatumika.
-Love bombing technique: katika technique hii mwanamke atamuaktia na atamjaza simp na sifa za uongo na kuonyesha kuwa ana interest nae kisha kuanza kuomba mahitaji na simp akionyesha hayupo tayari basi ataanza kumpa lawama na kumfanya ajiskie sio mwanaume kwa kutomfanyia mambo anayotaka.
-Kumnyonya kiuchumi;kuomba misaada ya mara kwa mara, pesa za dharula na kutaka simp agharamikie lifestyle anayoitaka mfano mitoko,kuvaa nguo mpya kila wiki,kununuliwa simu mpya kwa kila toleo, kusafiri kwa ndege na kutumia usafiri wa private kama Uber. Akionyesha kushindwa kuyafanya haya atamuonyesha kuwa ameshindwa kumuonyesha mapenzi ya kweli na kumtunza.
Ni muhimu vijana wakajua madhara na namna wanaweza kuingia mkumbo huu wa kuwa masimp. Usimp sio sifa wala ujanja ni uzembe,ushamba na udhaifu mkubwa sana kwa mwanaume. Nakukumbusheni tena, kuwa mkarimu,kujali, kumpa attention mwanamke, sio udhaifu ni matendo ya kiutu na ni kawaida, ila kuyafanya haya matendo kwa mtu ambaye amekwisha onyesha tokea siku ya kwanza kuwa hana interest na wewe bila mipaka, bila kulinda heshima yako, bila mrejesho wa kujaliwa upande wa pili na kuyafanya kwa kiwango cha kupitiliza ndio usimp unapoanzia.
Tiba ya kutokuwa simp sio kuwa na roho mbaya kwa wanawake na kuwakazia kiroho mbaya au kuwa na kisasi nao kwa kuacha kuwajali na kuwasaidia haja zao, hapana. Tiba ya usimp kwa vijana ni kuanza kujifunza namna ya kujitambua na kuielewa thamani yao kama wanaume katika jamii na wanatakiwa kuwa vipi na kujua namna ya kuwekeza muda,pesa,jitihada,attention na upendo kwa wale ambao watawapa mrejesho wa vitu hivyo kwa moyo wote kwaajiri ya kujenga nao maisha.