Usimfananishe mkeo na milupo pls | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usimfananishe mkeo na milupo pls

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 5, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  [h=3]Usimfananishe na wengine![/h]

  [​IMG]James (si jina lake halisi) ana mshangaa mke wake ambaye baada ya kuzaa mtoto ambaye sasa ana miaka miwili amekuwa akikwepa kuvua nguo na kubaki uchi wakiwa pamoja chumbani wakati haikuwa kawaida yake.
  Bila kusita James anaamua kumuuliza mke wake mpenzi
  “vipi mbona siku hizi ni kama unanikwepa nisikuone upo uchi
  Mke wake Beatrice anajibu
  “ Naogopa utaniona nilivyo na umbo baya kwani nimenenepa sana na najisikia hutanifurahia kuniona na hizi nyama uzembe nilizonazo”

  James kwa mshangao huku ana tabasamu anamjibu
  “Sikutegemea kama unaweza kuwaza hivyo kwani mwili wako ni wa thamani sana kwani umenizalia mtoto mzuri sana hivyo ni faraja na najisikia fahari sana kuuona mwili wako katika umbo lolote kwani nikiuona mwili wako najiona fahari kwani kwa mwili wako tumepata mtoto mzuri sana duniani"


  Je, ni wanawake wangapi wanaweza kutegemea majibu ya hekima kama ya James kutoka kwa waume zao hasa pale wakiwa wamebadilika maumbo yao?

  John baada ya kuona mke wake amenenepa ghafla baada ya kuzaa watoto wawili akaaamua kununua jarida (magazine) linaloonesha wanawake wembamba wanamitindo na akaliweka kitandani ili akiona asome na ajifunze na kama inawezekana aweze kufanya juhudi kuiga au kurudi kwenye umbo lake zamani na kuonekana sawa na wale wanawake kwenye jarida.

  Je, unadhani approach aliyotumia John kuweka jarida ambalo litaonesha wanawake wembamba itasaidia mke wake kujirekebisha?

  Jambo la msingi si kutaka kuwaridhisha au kuwapa kichwa wanawake ambao hunenepa baada ya kuzaa na kwamba waridhike na kujiachia, hapana jambo la msingi ni kwamba approach ambayo mwanaume hutumia inaweza kufanya mwanamke kujisikia amedharauliwa na huishia kuumia na kukwazika.

  Kutumia kipimo cha wanawake wa kwenye majarida si sahihi kwani wengi hawajawahi kuzaa hata mtoto mmoja na wengine wamefanyiwa plastic surgery baadhi ya viungo vyao kama matiti na hips, na pia picha zao hupitia processs za kuzisafisha ili zionekane nzuri zaidi na kuvutia hivyo ukitaka mke awe kama hao una kazi ya kufanya na si kumsukumia gazeti asome awe kama wao.

  Pia ifahamike kwamba ukitaka kufikisha ujumbe mara nyingi kwa mwanamke jambo la msingi ni jinsi unavyowakilisha ujumbe wako unaweza kuwa na nia nzuri hata hivyo jinsi unavyowakilisha huweza kufikisha ujumbe mwingine ambao matokeo ni kuumizana hisia.

  Wapo wanaume ambao huenda mbali zaidi kwa kuwalinganisha na wanawake wengine kwa mfano
  "Huoni mwenzako Anna sasa amepungua na wewe bado umebaki umenenepeana"
  Hakuna kitu kinaumiza kama hicho!

  Kuwa positive huweza kusaidia kutatua tatizo kuliko kuwa negative au kulalamika tu,
  anyway kwanza ni mke wako hata aweje ni wewe uliyekubali kusema "hadi kifo kitakapo tutenganisha!"
  Hivyo kitunze kidumu na kipendeze na si kwa kulaumu na kumlalamikia tu bila kusaidiana.

  "Usione vinaelea vimeundwa kwa mawazo positive na kwa upendo wa kweli"


  Posted by Lazarus Mbilinyi at 1:09 AM [​IMG] [​IMG]
   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  guuuuuuuuuuuuuuuuuuuud!!!!!
   
 3. MaVa

  MaVa Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  U re right Pdidy... Thanx much
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  SAME TO YOU ROSE
  [​IMG]
   
 5. A

  Aine JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana Pdidy, wanaume kama James ni wachache kiukweli
   
 6. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #6
  Jul 5, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Noted with thanks...
   
 7. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  DA!.....SAFI SANA PDIDY,
  Jibu kama la JAMES likipenya masikioni yaani ni raha na furaha tele moyoni.
  SHUKURANI NYINGI SANA.
   
 8. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mi naona ningepata mume kama james ningekuwa naringa sana barabaran
   
 9. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wanaume ina maana hii topic hamjaisoma? manake naona mko kimyaaaa
   
 10. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Imekaa vizuli nibola kimywaa kuliko kuchafuwaa hali ya hewa
   
 11. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  P Didy umeongea kitu ya maana sana. Kama hupendi manyama uzembe unatakiwa msaidiane na wife kuyapunguza. Mnaweza nunua vifaa vya mazoezi hata vya bei poa kama kamba na kufanya mazoezi pamoja. Ni wanaume wachache wenye busara kama hiyo kwa kweli. Wengi ndio kwanza wanatafuta vimada kusema hao vimada waliambiwa ni tasa hawatazaa. Au ndio unakuta mwanaume anabadili mabibi tu akishazalisha anasonga mbele.
   
Loading...