Usimba, Uyanga na tamaa ya mafanikio binafsi yanaua ligi la Tanzania

shahazady mustafa

Senior Member
Oct 1, 2018
110
56
Kwanza natangulia kuomba msamaha kwenu wapenzi wa mpira wa miguu wa simba na yanga lakini pia naomba ukweli huu uwapenye.
Inauma sana pale tunapojivuna kwa watani zetu kuwa watani zetu hawachomoi wakimaanishwa simba na yanga wakati ligi ina vilabu 20, hadi natamani watengwe na shirikisho basi mechi ya leo iwe simba vs yanga ,, mechi ya kesho iwe yanga vs simba,, na kesho kutwa hivyo hivyo hadi wachoke wenyewe.
Inafikia hatua mtu anatamani simba na yanga zina futiliwa mbali na wachezaji wagawanywe mmoja mmoja ktk vilabu 18 vinavyo shiriki ligi ya Tanzania .

Natamani katiba ya TFF iweke kipengele cha kuweka ukomo wa kusajili wachezaji wa inje ya nchi kwakuwa hawatusaidii ktk ligi ya taifa bali tunakuwa tunajitengenezea bomu litakalo tulipua wenyewe ktk timu ya taifa, angalieni Emmanuel okwi tunaejidai nae ktk club ya simba anayoyafanya kwao kwenye timu yake ya taifa, kagere ?, paskali wawa je? , chama je?, Tshimbi je?, niyonzima je?,....!!

TFF amkeni bwana
Mimi sasahv tukiwa na mchezo ligi ya taifa tayari matokeo yanakuwa yameshajulikana kuwa tunafungwa tu kwakuwa hatuna mzizi wa ligi yetu. Faraja tu inakuja ktk vijana wetu Serengeti boys, mpaka naona ikiwekwa mechi ya Serengeti boys na taifa stars basi watoto watawachapa mabraza.

Sheria ziwekwe, lazima tuwe na vipaji vidogo kusudi tuviinue vitusaidie ktk ligi za ndani na ktk ligi ya taifa.

Kama nmewakwaza mnisamehe lakini ukweli ndo huo usimba na uyanga unaua mpira wa taifa
Kama mnanibishia ngojeeni mtaona okwi atakacho tufanyia mwakani japokuwa saiv tunalinga tu ooh this is simba or yanga yanga lakini tunashindwa kusema this is Tanzania stars.

Nimemind kinoma yani na lawama zote kwenu TFF.

Wekeni sheria kuulinda mpira wa taifa.

Sheria ya kusajili wachezaji wa inje wasizidi wawili.

Kila club ihakikishe ina academy.

Hamuoni Raisi wa nchi anavyo nyoosha taifa kuleta maendeleo?

Nyie TFF chini yako Raisi wake unashindwa nini kuweka uongoz wa jihistoria wa sheria kama hizo kuokoa Taifa stars?

Halafu tuachane na dhana ya tuombe mungu yule afungwe ili tupate kufuzu kwakuwa nao wanamuomba mungu hivyo hivyo, chamsingi ni mazoezi, kukuza vpaji kwa kufuata mambo hayo.

Mnisamehe lakini ni bora iwe hivyo kwa maslahi mapana ya taifa.

Povu ruksa maana itakuwa imepenya.
 
Mpira na siasa haviendani. Kocha anapangiwa kikosi kabla ya kambi ya national team. Viongozi matumbo makubwa kama viroba vya ngwara. Hawawazi kitu ila kuhudumia mitumbo tu.

Ningekuwa raisi kwanza nchi hii hakuna kumpa cheo mtu mwenye mtumbo mkubwa.

Wenye matumbo wote povu ruksa sheenz.. 😈
 
Inauma ila basi tu.
Mwenye uwezo na maamuzi thabiti hapati nafasi
Mpira na siasa haviendani. Kocha anapangiwa kikosi kabla ya kambi ya national team. Viongozi matumbo makubwa kama viroba vya ngwara. Hawawazi kitu ila kuhudumia mitumbo tu.

Ningekuwa raisi kwanza nchi hii hakuna kumpa cheo mtu mwenye mtumbo mkubwa.

Wenye matumbo wote povu ruksa sheenz..
 
Jamaa uliandika kwa uchungu sana sema tu watu hawakukuelewa ila huo ndo ukweli. Vilabu hivi viwili ni kansa kwa soka letu pia ndo nguzo ya mpira wa nchi hii. Yaani kotekote wapo, wanaua soka na pia wao ndo soka la nchi hii.

Tufanyeje sasa, tuwafutilie kukata nguzo la mpira wa nchi hii?
 
Back
Top Bottom