Herbert Nkuluzi
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 2,430
- 2,436
Ipo hivi ,Mm pia ninahitaji sana kujua njisi ya kupata commision , kwa wenye ufahamu tupatieni elimu jamani.
Commision inatokana na miamala uliyoifanya kwa mwezi mzima na miamala hiyo iwe halali (miamala mingine hulipwi kwa kuwa uliweka ujanja , kwa mfano mtu mmoja atume elfu 20 kwa wewe wakala kuigawa mara nne yaani elfu 5 kwa kila muamala tena ndani ya muda huohuo kwenda kwa mtu mmoja ) hapo utalipwa muamala wa kwanza tu mingine mitatu hulipwi.
Sasa commision ipo hivi
Ukimtolea mteja 100,000 unalipwa tsh 600
1,000,000=2000 that means kwa miamala hiyo tu utalipwa tsh 2600 kwa hivyo endapo kila siku utapata wastani huo tajwa maana yake utalipwa tsh 78,000# sasa ni vema kuelewa kuwa kuna kiwango maalumu cha malipo kwa miamala kwa mfano kuanzia Tsh 1000-4999 ina malipo yake katika kutoa na kuweka ambayo ni madogo vivyo ukianzia 5000-9999 kuna kiwango chake maalumu inaendelea hivyo hivyo hadi kufika mwisho na kadri hela inavyoongezeka ndivyo malipo yake huwa makubwa , kwa hivyo endapo upo sehemu yenye mzunguko mkubwa kwa maana ya watu wengi kutoa pesa na kuweka pesa let say kwa siku una wastani wa kuhudumia watu 50 tena wa kiwango cha fedha cha wastani wa 80,000 unaweza kujikuta umelala na tsh 25,000 kwa siku au zaidi. Sasa hayo malipo ya kila siku unayopata hayaji kuwa pesa wakati huo huo hadi kampuni iyajumlishe yote kwa mwezi mzima then ikate asilimia 10 yake kinachoki ndo chako ambacho sasa inakuwa ni pesa yako kabisa.
Kumbuka watu wengi wakitoa pesa kwako na kwa mwingine wakaweka sana maana yake ni kuwa wewe utapata faida zaidi kwa kuwa miamala ya kutoa pesa ina faida zaidi kuliko ya kutuma pesa hata kama ikilingana kwa idadi.
NB: Vodacom ndiyo kampuni inayolipa kamisheni nzuri zaidi kwa mawakala wake japokuwa imepungua kiasi kutokana na sheria yao mpya ya kwamba pesa inayotumwa na wakala haipaswi kuvuka mnara ambao wakala ameutumia kutuma pesa (namaanisha , ikitokea upo Dar ila wewe wakala mnara uliokuhudumia mawasiliano ni wa Ukonga mombasa lakini pesa umeituma kwenda kwa mtu ambaye anatumia mnara wa Ukonga mazizini , faida ya muamala huo hutolipwa kabisa yaani ni sawa na umetoa sadaka tu)
Airtel ni kampuni inayofuatia kwa malipo mazuri na Halotel japo halotel haina wateja hivyo malipo yao yapo chini mno.
Kwa maeneo ya Pwani Tigo inalipa vizuri kutokana na wingi wa wateja si ubora wa malipo yao kwa mawakala.
By the way ukiwa serious na ukawa eneo lenye watu wengi biashara hii ni bora zaidi na itakuwezesha
Kwa ufafanuzi wa kina zaidi nitafute kwa namba hii 0755346718